Zacht
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 1,009
- 2,197
Wakulima wengi wa nyanya wanapata hasara kutokana na kuzalisha nyanya ambazo zimezidi mahitaji ya soko au Sababu nyingine ni uhaba wa masoko ,Kiasi kikubwa cha nyanya zinaoza shambani au sokoni ni kwa sababu wakulima wengi hawana/hawajui jinsi ya kuhifadhi nyanya zao
Kwa utafiti wangu usio rasmi nimebaini Wakulima wengi wanapoteza zaidi ya nusu ya nyanya zinazozalishwa.
Hasara kubwa wanaipata Kipindi Cha msimu wa mavuno , nyanya nyingi zinaharibika kwa kusubiri wanunuzi na zingine zinaharibika tu kutokana asili ya zao lenyewe lilivyo(laini) hivyo inawalazimu wakulima wengi kuuza kwa bei ya hasara wengine wanazitupa kabisa kwa kukosa wateja.
Sasa Njia nzuri ya kuzihifadhi na kuongeza thamani nyanya zako zilizoharibika (sio kuoza) na ambazo zimekosa soko ni kuzifanya kuwa unga (tomato powder).
Njia hii ni nyepesi Wala haiitaji gharama kubwa , unachotakiwa kufanya unazikatakata nyanya zako kisha unazianiaka juani, baada ya kukauka utazisaga kwa blenda au kwa kutumia kifaa chochote ilimradi iwe unga
kutengeneza tomatoe powder inasaidia kupunguza upotevu wa nyanya baada ya mavuno lakini pia inasaidia kendelea kutumia nyanya nyakati za uhaba wa nyanya,
hivyo ni wazo Bora pia ukiamua kufanya kibiashara , na uzuri ni kwamba tomato powder ikihifadhiwa vizuri inakaa kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita kwahiyo kazi kwako mkulima ulifanye kuwa wazo kamili au ulitume pindi nyanya zikishindwa kutoka sokoni.