Mkuchika na Pumba Zake: Aifananisha Timu ya Sudani na Idd Amin..!

akilimtindi

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
421
83
Wakuu Samahanini nilipotea kwa muda kwenye kutafuta katika hali yetu ya kawaida. Nimerudi na naomba mniruhusu kuendelea kuchangia, yangu leo machache.

Hivi ni kweli huyu ajulikanaye kama Mheshimiwa Captain Kamanda Mkuchika ndiye Waziri wetu wa Habari tunayemtegemea? Nimemshangaa kwa muda maana namsikia kwa muda akiongea mambo ambayo siyaelewi. Kwanza nilimsikia akisema anapiga marufuku wimbo wa Taifa kwenye simu, pili leo namsikia akitema pumba nyingine wakati anakabidhi bendera ya taifa kwa timu yetu kwenda Sudani, kasema Baba wa Taifa alivyofanikiwa kumtoa Idd Amin alienda hadi kwake Uganda kumchapia hukohuko. Je, huo ndio mfano halisi wa kuwapa timu yetu ya taifa? Je, timu ya Sudani yaweza kufananishwa na Idd Amin?

Swali langu la msingi hili hapa, hivi haya yote ni matamshi ya Serikali au Mheshimiwa Captain Kamanda Mkuchika?
 
pili leo namsikia akitema pumba nyingine wakati anakabidhi bendera ya taifa kwa timu yetu kwenda Sudani, kasema Baba wa Taifa alivyofanikiwa kumtoa Idd Amin alienda hadi kwake Uganda kumchapia hukohuko. Je, huo ndio mfano halisi wa kuwapa timu yetu ya taifa? Je, timu ya Sudani yaweza kufananishwa na Idd Amin?

Swali langu la msingi hili hapa, hivi haya yote ni matamshi ya Serikali au Mheshimiwa Captain Kamanda Mkuchika?
Kamanda mikwara kwenye football ndio mwake... hakuna cha kushangaa hapo! Sasa wewe ulitegemea aseme nini?
 
Back
Top Bottom