Mkono kupoteza hisia baada ya ajali ya gari

IGADESA

JF-Expert Member
Jan 15, 2021
298
732
Habari za mida hii.

Nina mdogo wangu wa kiume umri miaka 24 ni dereva, miezi minne iliyopita alipata ajali ya gari, alipata mikwaruzo mwilini pia akavunjika mkono wa kulia (mfupa mmoja wa chini na mfupa wa juu).

Akawekewa POP kwa wiki sita, ila mpaka sasa mkono huo wa kulia hawez kuuchezesha wala vidole pia havichezi.
 
hakikisha anaangaliwa na daktari bingwa wa mifupa baada ya kutoa POP aone muunganiko unaendeleaje kisha atashauri kama aanze mazoezi ya viungo au vinginevyo maana kuna wataalamu wengine zaidi huenda wakahusishwa.
 
Habari za mida hii. Nina mdogo wangu wa kiume umri miaka 24 ni dereva, miezi minne iliyopita alipata ajali ya gari, alipata mikwaruzo mwilini pia akavunjika mkono wa kulia (mfupa mmoja wa chini na mfupa wa juu). Akawekewa POP kwa wiki sita, ila mpaka sasa mkono huo wa kulia hawez kuuchezesha wala vidole pia havichezi. ..Je
Mmh hebu arudi hospital akafanye vipimo upya
 
kwa sasa anaendelea na mazoezi ya huo mkono
 
Mmh hebu arudi hospital akafanye vipimo upya
Ameambiwa baada ya mazoez ya mwezi mmoja akaangalie uungaji wa mfupa unaendaje. Ila hawaongelei swala la kipimo cha kujua status ya mshipa wa fahamu.
 
Nenda kamtafute specialist wa mifupa na mfumo wa fahamu.
Achana na hao waganga wa Zahanati/vituo vya afya asije mdogo wako akapooza mazima.
 
Ameambiwa baada ya mazoez ya mwezi mmoja akaangalie uungaji wa mfupa unaendaje. Ila hawaongelei swala la kipimo cha kujua status ya mshipa wa fahamu.
Hilo halihusiani na mishipa ya fahamu vema arudi hospital kwa ajili ya hilo
 
Habari za mida hii. Nina mdogo wangu wa kiume umri miaka 24 ni dereva, miezi minne iliyopita alipata ajali ya gari, alipata mikwaruzo mwilini pia akavunjika mkono wa kulia (mfupa mmoja wa chini na mfupa wa juu). Akawekewa POP kwa wiki sita, ila mpaka sasa mkono huo wa kulia hawez kuuchezesha wala vidole pia havichezi. ..Je
Pole sana,
Wataalamu wawili watahitaji kuhusishwa:

1: Mifupa: kuangalia uvunjikaji na jinsi sehemu ilivyoungwa na kama POP inaweza kuwa ni sababu ya haya ya sasa.

2: Mtaalamu wa mishipa ya fahamu: kutathimini chanzo cha kukosa mawasiliana, kama ni eneo tofauti na mvunjiko ulipo au ni pale na nini kifanyike.

NB: Ni vyema haya kufanyiwa kazi mapema ili kurudisha mawasiliano na afya ya eneo husika.
 
Back
Top Bottom