Ufunguo
JF-Expert Member
- Aug 18, 2012
- 330
- 231
1. Tuwe na vyama vya siasa visivyozidi 3.
2. Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi marufuku kuwa wanasiasa wala kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali.
3. Tubadili mfumo wetu wa elimu kutoka huu wa kinadharia kwenda wa kivitendo zaidi ili tuondoe utegemezi wa kitaalamu hasa katika sayansi na teknolojia.
4. Elimu ya Uraia ipewe kipaumbele ili wananchi wote wajue haki na wajibu wao kama raia wa Tanzania.
5. Makosa yote ya Rushwa adhabu yake iwe kifo (am serious), maslahi ya Taifa mbele..
6. Nafasi zote za taasisi za serikali, mikoa, wilaya, ukatibu mkuu, n.k zitangazwe na watu wote wenye sifa waombe na wafanye kwa mikataba ya miaka 3 baada ya hapo wapimwe utendaji kazi wao, wasipokidhi malengo yaliyowekwa wawekwa pembeni.
7. Kila mtanzania awe na kadi ya kupiga kura maana hiyo ndo nguvu yake pekee na ashiriki kikamilifu zoezi la kupiga kura mahali popote alipo ili mradi tu kadi yake imethibitishwa kuwa halali (kumlazimisha mtu apige kura mahali alipojiandikisha ni kuingilia haki na uhuru wa mtu binafsi, ibara ya 15 ya katiba).
8. Kuwe na kura ya maoni ya watanzania wote hasa tunapoona utendaji wa Rais hauridhishi kama ulivyo kwa sasa ili kumwadabisha.
9. Kuwe na mgombea binafsi maana wagombea wa vyama wengi wanaingizwa kwa fedha za mafisadi, hivyo uwezo wa kuwashughulikia mafisadi wanakuwa hawana (Mkono unaokulisha huwezi kuungata, vinginevyo utakuwa kichaa).
10. Apatikane kiongozi ambaye atakuwa tayari kufa kwa ajili ya maslahi ya nchi (awe tayari kufumua mizizi yote ya chama tawala ndani ya taasisi mbalimbali kama jeshi, usalama wa taifa, mahakama, bunge n.k )
11. Maliasili zote za nchi ziwanufaishe kwanza wananchi wa mahali husika, pia mikataba yote ya wawekezaji ipelekwe bungeni na baadae kwa wananchi husika ili wajue kilichoko ndani ya mkataba kama kina maslahi kwao ama la na wananchi ndo wawe waamuzi wa mwisho.
12. Tanzania kama nchi tuwe na vision, mission, goals n.k ambapo serikali yoyote itakayoingia madarakani lazima itekeleze mambo ya msingi ya nchi. Sio kama sasa ambapo kila anayeingia madarakani anaweza tu kubadilisha mifumo mbalimbali kwa maslahi yake binafsi. Kama ilivyotokea waziri alivyofuta somo la kilimo mashuleni na kuondoa michezo!
13. ..
14. ..
Je wewe mwanajamii unasemaje?, naruhusu mjadala na mapendekezo mengine zaidi .
Aluta continua.