Mkombozi Bank: Miamala iliyofanywa kupitia Akaunti ya VIP Engineering ilikuwa halali

Utetezi wa ajabu,nafunga account yangu iliyo stanbic na nikisikia hii hela chafu imehamia pia CRDB nafunga acc pia
 
They are dirty as the Vatican the holy sea!
I respect Catholicism buy for what Mkombozi Bank did, out of ethics!

Wewe ni alshababu, mtabaki duni daina hata mfanyeje.Ujinga wenu na kukaa mnachora kiarabu na kufuga mapepo yatazidi kuwafanya kujitoa mhanga na hamtakaa kuwa na utulivu popote mlipo.
 
Escrow ni kizunguzungu.

huyu mkurugenzi anachokisema hapa ni kwamba Zitto kalidanganya Bunge kwa kusema kwamba pesa zililipwa cash na watu walienda na viroba, sandarusi, lumbesa na mifuko ya rambo na kugawana pesa za escrow! zitto anasema kamati iliambiwa na Mkurugenzi wa PCCB. Hapa panataka umakini kwa kuwa PCCB haijatoa report yake

Kila kukicha inakuja taarifa mpya.
 
Uwongo tulishausikia kwa sababu ulipanda lifti, ukweli huwa unapanda kwa ngazi kwa ngazi, ndio huo sasa unakuja
 
Escrow ni kizunguzungu.

huyu mkurugenzi anachokisema hapa ni kwamba Zitto kalidanganya Bunge kwa kusema kwamba pesa zililipwa cash na watu walienda na viroba, sandarusi, lumbesa na mifuko ya rambo na kugawana pesa za escrow! zitto anasema kamata iliambiwa na Mkurugenzi wa PCCB. Hapa panataka umakini kwa kuwa PCCB haijatoa report yake

Kila kukicha inakuja taarifa mpya.
Mkuu...c unaweza kusoma bank statement... Angalia bank statement ya mkombozi...inajieleza kbsa...tena ipo humu humu JF...

Mode naomba uweke ile bank statement ya mkombozi kuujuza umma
 
Huge transaction to Politically Exposed persons is suspicious transaction and ought to be reported to FIU according to Ant Money Laundering Act. what about this
Ure very right but all measure taken...and due deligence...
 
Huwezi kumuuliza muumini fedha umepata wapi wakati unajua ana shughuli zake.
 
Mbona huyu Mwanasheria wamejibu vipi wajumbe wa bodi Maskofu hawajasema.

Stanbic Bank na Mkombozi Bank wote wameshiriki kutorosha pesa za umma.

Stanbic Bank wameishimfukuza meneja wao.
Mbaya zaidi ni kwamba hela hizo zilianza kutoroshwa na BoT kwa amri ya mwanasheria wa CCM
 
Huge transaction to Politically Exposed persons is suspicious transaction and ought to be reported to FIU according to Ant Money Laundering Act. what about this

Kwa lugha ya kibenki wanasiasa wanaitwa PEP yaan Politically exposed persons na treatment yao ni ya tofauti sana as bank zinatakiwa ziwe makini sana na transactions za hawa PEP! Pesa yoyote inayoingia kwenye acc ya mwanasiasa lazima bank ijiridhishe kuwa ni halali! Kweli wanasiasa wamelipwa pesa zote hizo kutoka kwenye acc ya mtu mmoja then mnasema mlijiridhisha kuwa transactions hizo zilikuwa halali?A big No to that! Hii bank kweli wanajua AML act na policy?mbona iko very strict kwa vitu kama hivi?This bank has to be sanctioned! Hili linaonyesha kuwa kuna madudu mengi sana ndani ya hiyo bank.napendekeza BOT waende wakafanye a very deep inspections kwenye hii bank watagundua mengi! Kwanza sidhan hata kama wana MLO hawa
 
Hakuna anayetetea kosa ila Askofu kilaini hana kosa kwa vile pesa alizopewa ni kutoka kwa mhisani aliyezoea kufanya hivyo mara nyingi. Hakuna anayemwuliza mfadhili wapi amepata pesa. Kama Askofu Kilaini angejua kwamba pesa hizo makandokando yake ndio hayo naamini kabisa asingepotea, ila ni jambo ambalo huwezi kumwuliza mfadhili alikopata pesa, hilo linaeleweka.

Sasa askofu amejua kuwa pesa hizo sio safi ksbu palikua na ukwepaji kodi (tax fraud) anasuburi nini kurudisha fedha kidogo kiasi icho. Ni aibu kwa askofu wa kaliba ya Kilaini kuendelea kukuaa kimya. Ni sh. 80 million tuu. Arudishe kwa heshima yake na kanisa.
 
Kwa lugha ya kibenki wanasiasa wanaitwa PEP yaan Politically exposed persons na treatment yao ni ya tofauti sana as bank zinatakiwa ziwe makini sana na transactions za hawa PEP! Pesa yoyote inayoingia kwenye acc ya mwanasiasa lazima bank ijiridhishe kuwa ni halali! Kweli wanasiasa wamelipwa pesa zote hizo kutoka kwenye acc ya mtu mmoja then mnasema mlijiridhisha kuwa transactions hizo zilikuwa halali?A big No to that! Hii bank kweli wanajua AML act na policy?mbona iko very strict kwa vitu kama hivi?This bank has to be sanctioned! Hili linaonyesha kuwa kuna madudu mengi sana ndani ya hiyo bank.napendekeza BOT waende wakafanye a very deep inspections kwenye hii bank watagundua mengi! Kwanza sidhan hata kama wana MLO hawa
Excellent point! Halafu kitu ambacho watu hawakifahamu ni size ya benki ya Mkombozi. Hii benki ni ndogo sana kwa aina ya miamala iliofanya ktk hii kashfa. Hela ya Ruge ilikua kubwa kuliko total assets za mkombozi. Hawakupaswa hata kupokea kiasi icho. Najaribu kufikiri iyo siku wamepokea deposit ya $ walisquare vipi position yao! Ndio maana tunasema BOT wakiwachunguza vizuri lazima watafichua mengi kuhusu mkombozi.
 
Huge transaction to Politically Exposed persons is suspicious transaction and ought to be reported to FIU according to Ant Money Laundering Act. what about this

Ngoja tuone hiyo 'Anti-Money Laundering Act inasemaje..!!!!

Hiyo ya Politically Exposed Person' iko wapi..???

Weka nukuu yako hapa tuione..!! Hii ni JF, sio FB..!!

 17.-(1) Where a reporting person suspects or has grounds to suspect
that funds or property are proceeds of crime, or are related or linked to
or are to be used for commission or continuation of a predicate offence or has knowledge of a fact or an activity that may be an indication of money laundering or predicate offence
he shall within twenty four hours, after forming that suspicion and, wherever possible, before any transaction
is carried out:-
(a) take reasonable measures to ascertain the purpose of the
transaction or proposed transaction, the origin and ultimate destination of the funds or property involved, and the identity
and address of any ultimate beneficiary; and
(b) prepare a report of the transaction or proposed transaction in accodance with subsection (2), and communicate the
information to the FIU by any secure means as may be
specified by FIU.
 
Kwa lugha ya kibenki wanasiasa wanaitwa PEP yaan Politically exposed persons na treatment yao ni ya tofauti sana as bank zinatakiwa ziwe makini sana na transactions za hawa PEP! Pesa yoyote inayoingia kwenye acc ya mwanasiasa lazima bank ijiridhishe kuwa ni halali! Kweli wanasiasa wamelipwa pesa zote hizo kutoka kwenye acc ya mtu mmoja then mnasema mlijiridhisha kuwa transactions hizo zilikuwa halali?A big No to that! Hii bank kweli wanajua AML act na policy?mbona iko very strict kwa vitu kama hivi?This bank has to be sanctioned! Hili linaonyesha kuwa kuna madudu mengi sana ndani ya hiyo bank.napendekeza BOT waende wakafanye a very deep inspections kwenye hii bank watagundua mengi! Kwanza sidhan hata kama wana MLO hawa

Sasa mbona unajipinga wewe mwenyewe???

Angalia hapo kwenye blue...!!!

Yaani umesema benki inatakiwa ijiridhishe..... Halafu unasema benki haikujiridhisha, wakati benki wenyewe wameshasema kuwa wamejiridhisha...!!
Soma vizuri taarifa ya benki, wamesema wazi-wazi kuwa wamejiridhisha... Sasa kama wewe huamini, nenda FIU, katoe taarifa.
FIU wataenda benki na watafanya uchunguzi wao kwa makini kabisa.

Na hapo kwenye red, inaonyesha kuwa hujui mabo ya AML.
Hakunaga AML policy, kuna AML regulations.
 
Huge transaction to Politically Exposed persons is suspicious transaction and ought to be reported to FIU according to Ant Money Laundering Act. what about this

Hebu weka quotation ya kifungu cha Anti-Money Laundering Act kinachosema hayo hapo juu tuone...!!!
 
Tunataka waliokuwa wanadai kuwa pesa ziligawiwa na kubebwa kwenye magunia aje tena aseme hapa.

Mbona nawe unakuwa kama Lusinde Kibajaji?? Hukusikiliza mchango wa Mhe Wassira jana?? Pesa ziligawiwa na kubebwa kwenye magunia katika bank ya Stanbic siyo Mkombozi bank
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AKAUNTI YA VIP ENGINEERING AND MARKETING ILIYOPO KATIKA BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI

Utangulizi

Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP engineering and Marketing (VIP)

Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.

Nyaraka hizo ni pamoja na kuwepo kwa cheti cha usajili wa kampuni, kanuni za kampuni, idhinisho la kampuni kumruhusu moja kati ya wanahisa wake kuendesha akaunti pamoja na picha na hati ya kusafiria ya mhusika wa kuendesha akaunti hiyo.

2.0 Mauzo ya hisa za VIP

Kampuni ya VIP ilileta mkataba kwenye benki ya Mkombozi wa mauziano ya hisa za asilimia 30 baina ya VIP na kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) ambazo inamiliki katika kampuni ya IPTL. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 19 Ogasti, 2013. Bei ya asilimia 30 ya hisa hizo ilikuwa ni dola za Marekani milioni 75. Katika kifungu namba 2.4 cha mkataba wao kinaelekeza fedha za mauzo ya hisa zilipwe kwenye akaunti ya VIP iliyopo benki ya Mkombozi. Mkataba huo wa mauziano ya hisa baina ya kampuni hizi mbili ulitambuliwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji J.H.K Utamwa tarehe 5 Septemba, 2013.

3. Mchakato wa kulipa kodi ya serikali

Benki ilitambua kwamba katika mauziano hayo ya hisa ni lazima kodi ya Serikali ilipwe na hivyo iliizishauri pande zote mbili kupeleka mkataba husika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanyiwa makadirio ya kodi husika. Tarehe 20 Januari, 2014 TRA iliiandikia barua kampuni ya VIP na nakala ya barua hiyo kuletwa kwenye benki ya Mkombozi. Katika barua hiyo TRA iliitaarifu kampuni ya VIP kuwa makadirio ya kodi yatokanayo na mauzo ya hisa ni shilingi 38,186,584,322.00 ikiwa ni kodi ya mauzo ya hisa ya asilimia 30 za mauzo ya hisa kutoka VIP kwenda kwa PAP.(Capital gains and stamp duty).

TRA pia iliiagiza benki ya Mkombozi kuhakikisha kuwa inalipa kodi hiyo kwa niaba ya VIP mara tu fedha zitakapoingia kwenye akaunti yake.

Malipo ya kodi ya shilingi 38,186,584,322.00 yalilipwa TRA kwenye akaunti 11120100 iliyopo katika Benki Kuu ya Tanzania na TRA ilikiri kupokea kodi hiyo kwa barua yake yenye kumbukumbu namba 3-4/100/100/223/4 ya tarehe 24 Januari, 2014.

4. Ufafanuzi wa mambo mbalimbali

4.1 Benki ya mkombozi kuhusika katika kusafisha fedha chafu

Fedha zote zilizoingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo kwenye benki ya Mkombozi zilitokana na mauziano ya hisa kati ya VIP na PAP kwa mkataba uliotambuliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Chanzo cha malipo hayo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya PAP iliyopo katika benki ya Stanbic na kuingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo katika benki ya Mkombozi.

Fedha hizo zilihamishwa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ilikuwa ni shilingi 73,573,500,000.00 zilihamishwa kwa njia ya TISS kwa kumbukumbu namba 000000050720 ya tarehe 23 Januari, 2014 na fungu la pili ni dola za Kimarekani 22,000,000.00 zilihamishwa kwa TISS kwa kumbukumbu namba 000000050812 ya tarehe 23 Januari, 2014. Malipo mengine ya asilimia kumi ya mauzo ya hisa yalilipwa kwenye akaunti ya Mkombozi iliyopo Benki Kuu ya Tanzania. Kutokana na mchakato huo benki ya Mkombozi ilijiridhisha kuwa fedha hizo ni malipo halali na siyo fedha chafu.

Benki ya Mkombozi haijihusishi na utakasishaji wa fedha chafu na haramu katika uchumi wa Tanzania.

4.2 Malipo yatokanayo na akaunti ya VIP

Malipo toka kwenye akaunti ya mteja hufanywa kutokana na maelekezo ya mteja. Benki ikishajiridhisha kuwa fedha ya mteja ni halali na ipo kwa mujibu wa sheria na hamna zuio lolote toka katika mahakama hapa nchini hutekeleza malipo kwenye akaunti ya mteja kutokana na maelekezo yake.

Benki ilijiridhisha kuwa malipo yote yaliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya VIP ni halali kwa kuwa chanzo cha pesa hizo ilikuwa ni halali kutokana na mauzo ya hisa na ulipwaji wa kodi ya Serikali kama ilinyoelezwa hapo juu. Kutokana na sababu hiyo benki haikuwa na shaka juu ya malipo hayo.

4.3 Malipo taslimu kwa wateja na kubeba fedha kwenye viroba, mifuko ya rambo na magunia

Benki inatoa tamko kuwa malipo yote yaliyofanywa katika akaunti ya VIP yalilipwa kupitia akaunti za walipwaji. Hakuna fedha zilizolipwa taslimu kwa wateja na kubebwa kwenye viroba au magunia kama ilivyoripotiwa Bungeni. Pesa iliyotoka kwenye akaunti ya VIP tarehe 6 Februari, 2014 kiasi cha shilingi 3,314,850,000.00 ililipwa kwenye akaunti nane za wateja tofauti na siyo kubebwa kwenye viroba au magunia.

Na zile zilizotoka toka benki ya Stanbic zilizotajwa hapo juu zilitumwa kwa njia ya TISS na siyo kubeba kwenye magunia au viroba.

4.4 Malipo kwa mfanyakazi wa benki ya Mkombozi

Gazeti la Mawio la tarehe 20-26, Novemba, 2014 tolea namba 0122 liliandika kuwa mwanasheria wa benki ya Mkombozi ajulikanaye kwa jina la Rweyengeza Alfred alipokea malipo toka akaunti ya VIP ya shilingi milioni 40.2.

Benki inatoa tamko kuwa haina mfanyakazi anayetambuliwa kwa jina hilo na wala hakuna mfanyakazi yeyote wa benki aliyelipwa fedha toka kwenye akaunti ya VIP.

Wito kwa umma

Benki ya Mkombozi inachukua fursa hii kuwatarifu wateja wake na umma kutopotoshwa na taarifa au tuhumma zilizofafanuliwa hapo juu na kuwataka wateja wake wote kutokuwa na hofu yeyote kwani benki ipo imara na inafanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania. Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kutoyumbishwa na tuhumma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu.

Pamoja tunajenga nchi na uchumi wa nchi yetu.

Hitimisho

Benki ya biashara ya Mkombozi haijihusishi na haitajihusisha na utakasishaji wa fedha chafu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA BIASHARA YA MKOMBOZI

Kuna miamala mikubwa kama ya akina tibaijuka ambayo iwe ilifanyika kwenye akaunti au kwa cash ilikua ni lazima ishirikishwe benki kuu mbona haijatotelewa ufafanuzi kwanini kigezo hicho hakikufikiwa?
 
Ngoja tuone hiyo 'Anti-Money Laundering Act inasemaje..!!!!

Hiyo ya Politically Exposed Person' iko wapi..???

Weka nukuu yako hapa tuione..!! Hii ni JF, sio FB..!!

 17.-(1) Where a reporting person suspects or has grounds to suspect
that funds or property are proceeds of crime, or are related or linked to
or are to be used for commission or continuation of a predicate offence or has knowledge of a fact or an activity that may be an indication of money laundering or predicate offence
he shall within twenty four hours, after forming that suspicion and, wherever possible, before any transaction
is carried out:-
(a) take reasonable measures to ascertain the purpose of the
transaction or proposed transaction, the origin and ultimate destination of the funds or property involved, and the identity
and address of any ultimate beneficiary; and
(b) prepare a report of the transaction or proposed transaction in accodance with subsection (2), and communicate the
information to the FIU by any secure means as may be
specified by FIU.

Mkuu ..kwel hapa cyo FB , nimependa nyanga zako
 
Back
Top Bottom