Mkokoteni wa kubebea wagonjwa.

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Katika taarifa ya habari ya ITV ya saa 2 usiku huu, nimeona habari ya zahanati moja iliyoko Mtwara pamoja na shida ambazo zinaikabili zahanati hiyo. Mojawapo ya matatizo yaliyoelezwa ni ukosefu wa mawasilaiano na vilevile ukosefu wa usafiri kwa wagonjwa. Katika habari hiyo ulionyeshwa mkokoteni wa kubebea wagonjwa uliotolewa na serikali, ukiwa umeharibika.

Taarifa hiyo ya habari imenifanya nifikirie ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali unaofanywa na viongozi pamoja na baraza kubwa mno na watumishi wa serikali ambao hawana lazima. Fedha hizo zingetumika kutatua matatizo hayo ya wananchi.

20120508_201521.jpg
 
hiyo itv wameonyesha zahanati moja yenye hali mbaya ila zipo nyingi kiukweli, sisi tumezidi ubishi kwani tumeshazoea kudanganywa tukiambiwa ukweli tunaoana uongo. hta dr slaa aliposema elimu bure tulibisha, tukawaamini magamba na uongo wao kuwa elimu bure haiwezekani hii ndo komesha yetu sisi na miaka iliyobaki ni mingi mpaka tutakapoamua kubadili maamuzi
 
Katika taarifa ya habari ya ITV ya saa 2 usiku huu, nimeona habari ya zahanati moja iliyoko Mtwara pamoja na shida ambazo zinaikabili zahanati hiyo. Mojawapo ya matatizo yaliyoelezwa ni ukosefu wa mawasilaiano na vilevile ukosefu wa usafiri kwa wagonjwa. Katika habari hiyo ulionyeshwa mkokoteni wa kubebea wagonjwa uliotolewa na serikali, ukiwa umeharibika.

Taarifa hiyo ya habari imenifanya nifikirie ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali unaofanywa na viongozi pamoja na baraza kubwa mno na watumishi wa serikali ambao hawana lazima. Fedha hizo zingetumika kutatua matatizo hayo ya wananchi.

View attachment 53796
Nimekumbuka milioni mia nne na zaidi zilizo karabati nyumba ya waziri wa afya! By the way baada ya kutemwa juzi bado anaishi humo au kaisha mpisha kijana wa mzee ruksa?
 
Nimekumbuka milioni mia nne na zaidi zilizo karabati nyumba ya waziri wa afya! By the way baada ya kutemwa juzi bado anaishi humo au kaisha mpisha kijana wa mzee ruksa?

huko ndio kwenye kura nyingi za ccm na cuf wao wanpiga kwa dini wakidhani wanachaua mashehe, basi waende miskitini wapewe mahitaji ya hospital!Kinachotakiwa ni kuandalia nani anakemea uovu na demokrasia kuliku kuangalia uslamu zaidi!

acheni kutultea hizo picha hapa!

ila CHADEMA JARIBU KUFANYA ZIARA HUKO TUKIE WAMEPATA AKILI? kama hhmnazo nasi waacheni wandelee na hali hiyo maana huo ni mtaji wa ccm kwa mtu w namna hiyo atanununulikwa kwa sh 500 badala ya khanga na kofia.

then gharama itakuwa ndogo plus wewe ni wa dini gani!
 
sera za ccm ni kandamizi zimeegemea kwa watawala na kwa watawaliwa hatuna kitu.wao na familia zao wakiugua waenda tibiwa nje hawajui adha tunayoipata.
 
Wabunge wote Ntwara CCM na si ndio kwao Nape huko jamani na wao wanaakili saaaana, badala ya kupeleka magari ya kubebea wagonjwa wapeleka fulana za njano na kijani na kanga. Tafakari................
 
Kwenye uzi huu hutamuona Ritz,Rejeo,Mama porojo,Tume ya katiba,Genius brain and co.
Huwa tunawaambia mtabanaweeeee mwisho mtaachia...kusema kweli kazi mnayofanya ni
ngumu sana! kuitetea au kuishabikia ccm yahitaji akili za kiuwendawazimu. Poleni sana
karibu mchangie na habari hii
 
Kwa kweli inatia hasira mnooo!!!

1)Huwezi amini haya mambo yapo kwenye nchi hii(Kisiwa cha Amani?Punda sawa,trolley poa,mkokoteni ndio usiseme)
2)Huko Serikalini magari wanayotembelea ni milioni mia mbili!
3)Serikali ina hela nyingi mpaka inaweza kuwakopesha wabunge Milioni 90 kila mbunge kwa ajili ya usafiri!!

Maswali ninayojiuliza!!
Hawa wananchi wana mbunge?Mkuu wa mkoa,wilaya?
Madaktari walipogoma kutetea hali duni za hospital zetu,waliwaunga mkono?

Kweli kuishi kwingi,Ni kuona mengi!!!
 
INANIUMA SANA!!!!

Kwa kweli binafsi niliangalia ITV jana usiku sa mbili nilisikitika sana.

Nikafikiria:-

(1) miaka 50 ya Uhuru jinsi Serikali ilivyotumia pesa nyingi kwa sherehe.
(2) Mafisadi wanavyokula pesa za nchi na wananchi wanaishi maisha yale.
(3) Jinsi taasisi za Serikali wanavyojiuzia magari kwa kisingizio yameisha muda wake.
(4) Kwa nini magari ya serikali yanayoisha muda wasiyapeleke katika hospitali zitumike kubeba wagonjwa,
(5) Jinsi Raisi na viongozi wanavyokwenda nje kutembea ikiwa wananchi wananishi maisha mabovu.
(6) Jinsi Viongozi wa serikali wanavyokwenda kutibiwa nje ikiwa wananchi hawana hata baiskeli ya kubeba wagonjwa.
(7) CCM walivyotumia pesa nyingi kule MWanza katiak sherehe ya kuzaliwa CCM
(8) Madakitari walivyogoma kwa kudai kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na hospitali.
(9) Wananchi tuliokunywa maji ya Bendera jinsi tulivyoupokea mgomo wa madakitari hata kutaka kuwafikisha mahakamani (Eti tulijiita ni wanaharakati wa CCM)

(10) Ikanijia picha hii hapa chini ya katika Hospitali moja huko KISAKI Morogoro kwani mambo haya si Mtwara tu, hata kwetu YAPO:-

View attachment 53845
Hapa ni Wodini na hawa ni Wagonjwa wamewekewa DRIP.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
TAtizo watu hamuamini kuwa sera ya CCM kuhusu afya imeshindwa; bado mna matumaini kweli!
CCM ilishashindwa siku nyingi tuu, tuombe Mungu kungojea uongozi mpa wa CHADEMA!!! Mtu kabadili baraza la mawaziri badala ya kufikilia kupunguza matumizi ya serikali yeye ndio mwanzo anaongeza matumizi from 50 Ministers up to 55 kweli huyu mkulu ana huruma na Watazania?????

Kwa kweli inatia hasira mnooo!!!

1)Huwezi amini haya mambo yapo kwenye nchi hii(Kisiwa cha Amani?Punda sawa,trolley poa,mkokoteni ndio usiseme)
2)Huko Serikalini magari wanayotembelea ni milioni mia mbili!
3)Serikali ina hela nyingi mpaka inaweza kuwakopesha wabunge Milioni 90 kila mbunge kwa ajili ya usafiri!!

Maswali ninayojiuliza!!
Hawa wananchi wana mbunge?Mkuu wa mkoa,wilaya?
Madaktari walipogoma kutetea hali duni za hospital zetu,waliwaunga mkono?

Kweli kuishi kwingi,Ni kuona mengi!!!
Hiyo ndiyo serikali ya maghamba's, hawana mpango kabisa ya kujua wanachi wao wanaishi vipi??? Kila kukicha gharama za maisha zinapanda, hivi kweli hiyo dispensary inazo dawa?????

Hiyo ndiyo serikali ya maghamba's, hawana mpango kabisa ya kujua wanachi wao wanaishi vipi??? Kila kukicha gharama za maisha zinapanda, hivi kweli hiyo dispensary inazo dawa?????

Yaani ile Dispensary ukimuangalia Mganga mkuu jinsi alivyo utapata picha kamili. Na nesi aliyehojiwa inatosha, huenda hata mishahara kupata kwao ni kitendawili wanafanya kazi kwa kuhurumia wagonjwa.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom