Mke wa Baba yako kwenye ndoa yako..

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Maisha ya ndoa pengine ni "komedi" (usanii).. Kwa mfano zipo kauli huwa zinatolewa siku ya harusi zinaitwa "Nasaa za wazazi (wengine wanaita wosia kama kauli ya mtu anayekufa)" ambapo wazazi huwa wanasimama na kuwahusia wanandoa kuwaeleza pamoja na mengine kama ifuatavyo:

Mzazi wa mume: kuanzia leo baba na mama wa mkeo ndio wazazi wako na sisi tena hatupo huko, ikitokea shida yeyote usije kwetu uende kwa mshenga au "best man" wako".uende ukaishi na mkeo kwa raha na mstarehe kama ambavyo umeona mimi na mama yako tulivyoishi mpaka tumefikia hapa.. sisi hatutakikusikia mnagombana na hatutaingilia kabisa huko kwenu...(hapo mama kama yupo nae anakuwa amejibanza pembeni mwa baba na ndugu wa upande wa kiume wakiitikia "sema baba sema baba aaaaa"..

Mzazi wa bibi Harusi nae: Nami nakuhusia mwanangu, kama alivyosema mwenzangu (baba wa Mumeo) , wewe sasa ni wa ukoo wa mumeo, sisi hatukujui tena. Tatizo lolote usituletee sisi , wajibu wetu wa kukuzaa na kukulea tumetimiza. na mama yako huyu naweza kukushuhudia ......ukimkorofisha wenzio usije ukasema ndugu wamewavuruga, ni wewe mwenyewe ndo utakuwa mke mpumbavu na kuvunja nyumba yako kwa mikono yako....

Cha ajabu utakuta karibia asilimia 55 -60 ya sababu za kuvunjika au matatizo ya ndoa huwa ni kutokana na wazazi au ndugu wa karibu kabisa wa mume na mke.

Kwa kawaida, siku zote japo wanandoa huwa napooana wanatengeneza familia yao, lakni bado unakuta Mume au Mke anaishi kwa kukumbuka zaidi na kujali wale ambao walimzaa au alizaliwa nao pamoja (ndugu zake) ....kwa waliooa au kuolewa anaweza kues emejifunza na kuelewa hilo.

Mara nyingi inapotokea ugomvi kati ya wanandoa, maneno kama "ndugu zako, mama yako, baba zako, wadogo zako", dada zako, kaka zako nk huwa hayakosi kutumika...na hivyo kuvunja maana ya "halisi ya ndoa" ( Mke ns mume wameungana na kuwa mwili mmoja).

Pengine unakuta mama wa mume ambaye ni "mke wa baba wa mume" au dada wa mume (wifi) huwa wanajisahau kuwa nao wameolewa, na huwa wakati wote wanaishi kwa kutegemea Mume lazima awasaidie tu, na wanachukia kuona ndugu za upande alikotokea mke wakiwa karibu na familia ya huyo wanaoendelea bado kumwona "wakwao"(MUme). Pengine unakuwa wakija kutembea, huwa wanataka kupewa uhuru na usio na mipaka na hata kufikia kuona "hapa kwa mwanetu, kaka yetu, nk"....wanachunguza makosa ya "mke " ili kujaribu kumkosoa na kumweleza Mume kuwa huyo mke hafai na wanaume wachache sana huwa wanakuwa na misimamo wa kutosikiliza yale wanayosikia toka kwa wale wanaohusiana kwa damu (baba, mama, dada, wadogo zake nk).

Kwa upande wa Mke, japo ni mara chache, lakini wazazi huwa nao wapo makini sana kuangalia upande wa mume una nafasi gani kwenye ndoa ya binti yao, unapata misaada gani nk nk ....na inapokuwa katika hali ngumu zaidi, unaweza kukuta Baba au Mama wa Mke kama si ndugu wengine udiriki kumweleza Mke kuwa aangalie sana familia ya mumewe kwa kuwa inambana Mume kiasi kwamba upande wa mke wanashindwa kusaidiwa wala kuwa na sauti kwao (zipo familia nyingine ambazo wahusika mwameona jirani huwa husababisha mpaka ugomvi wa kifamilia)...

Shida inakuja kupata tafisri halisi ya ndoa.., kama unahitaji kutimiza yote kwa usawa au lah??. inakuwaje ufikiri mama yako ni bora zaidi katika ndoa yako wakati yeye nae kaolewa na baba yako??
 
Ndoa ni ya wawili tu!! ila kuna wanaojisahau na kudhani bado wako kwenye maisha yao ya zamani. kama walizoea kusimulia kila kinachowakuta huwa wanaendelea kusimulia hata yatokeayo ndani ya ndoa zao...
 
Back
Top Bottom