Mke na Mume ni ndugu au Marafiki?

May 28, 2011
63
58
Hivi mke na mume ni ndugu au marafiki?
Na kama ni ndugu kwanini ndugu wafanye mapenzi?
Na kama ni marafiki basi na watoto wawe marafiki tu!
Post what you think about this
 
kwan wewe unafikir wao watakuwa upande gan? Na wewe umeoa au kuolewa? Je mkeo au mumeo ni nan kwako?
 
Mke na mume ni zaidi ya ndugu ni zaidi ya marafiki,wale ni mwili mmoja,kuwa mwili mmoja kuna maana ya kuwa kitu kimoja kama unajua maana ya kuwa mwili mmoja utamheshim sana na kumjali mwanandoa wako maana wewe ni yeye na yeye ni wewe,hamtofautishwi,ndio maana kuna mambo yanayokuhusu hawezi kuambiwa baba yako au mama yako au ndugu yako yoyote anaambiwa mwanandoa wako tu na hayo ni yale mambo nyeti,akiwa hayupo ndo wanaweza kuambiwa wazazi au ndugu zako!Ndoa ni kitu cha thamani sana!Usiichulie kawaida!Kama uko kwenye ndoa itunze!
 
Mume/Mke ni ndugu sababu undugu si wa damu tu...
ndugu ni mtu ambae mnajaliana, pendana, saidiana, wasiliana,
na muhimu zaidi ni kua uko kwa ajili yako no matter what!

Mume/Mke ni rafiki sababu rafiki aweza kua ni ndugu au mtu baki...
Rafiki ni mtu ambae anakuelewa kwa upana jinsi ulivyo, wapi akuguse
kukuumiza, wapi aguse kukufurahisha, kitu gani unapenda/chukia,
jinsi gani aku handle ili msikwazane, ni mtu uta confide siri zako bila
kuogopa atatangaza, ni mtu ambae pamoja ya kwamba mnaweza mkawa
siio blood relatives but ni mtu wa muhimu mno katika maisha yako ya kila siku...

Huo undugu na urafiki kati yenu ndo hufanya muwe best couple au vice versa
tokana na jinsi mnavyo handle undugu au urafiki wenu....
 
Ebwn hilo sual ni issue, ingawa kila mmoja anaweza kulijibu kwa uelewa wake lakini jiulize
kama ni ndugu yako mbona likitokea tatizo hasa la mahusiano mnapeana talaka?
Kama ni rafiki mbona huwa unamjali kuliko hata mama/baba au ndugu yako?
Kama ni mwili mmoja mbona moja anaweza kufa na kumwacha mwingine alitoa machozi?

Philosophical question.!!!
 
Mke na mume kwanza ni marafiki kwabla hawajafunga ndoa.. sababu wanajuana kwanza.. urafiki wao unaongezeka pale wafungapo ndoa na kama marafiki kuna ishu za hapa na pale na saa nyingine urafiki haudumu..(what goes up must come down)

mke na mume ni ndugu na undugu
unakuja pale kwenye shida na raha wako pamoja..

lakini papo hapo tukumbuke hawa
ni binadamu wenye mapungufu
yao saa nyingine wote wana different opinion kuhusu kitu fulani
wameshindwa ku compromise vitu
fulani maishani hapo ndipo urafiki na undugu unaingia matatani..
 
Mke na mume ni zaidi ya ndugu ni zaidi ya marafiki,wale ni mwili mmoja,kuwa mwili mmoja kuna maana ya kuwa kitu kimoja kama unajua maana ya kuwa mwili mmoja utamheshim sana na kumjali mwanandoa wako maana wewe ni yeye na yeye ni wewe,hamtofautishwi,ndio maana kuna mambo yanayokuhusu hawezi kuambiwa baba yako au mama yako au ndugu yako yoyote anaambiwa mwanandoa wako tu na hayo ni yale mambo nyeti,akiwa hayupo ndo wanaweza kuambiwa wazazi au ndugu zako!Ndoa ni kitu cha thamani sana!Usiichulie kawaida!Kama uko kwenye ndoa itunze!
Mie naamini yapo unayoweza kumwambia mke/mume na usimwambie mzazi na yapo unayoweza kumwambia mzazi na usimwambie mwezi wako tena basi hata awepo huyo mwenza. Umuhimu wa wazazi ni wa kudumu zaidi hata kama mnakuwa mwili mmoja au nusu mwili au miili elfu.
 
They are more than friends and ndugu! They are partners! They share more than what you could think of.......

What did you have in mind when you posed this thread...
 
Hii kama tuliijadili kwa mapana na marefu kwenye thread ingine
 
there a neither ndugu nor marafiki bt their both............and watoto ni zao la udugu na urafiki wa wazazi.....so watoto ni ndugu
 
Mke na mume ni Ndugu,na wanafanya mapenzi kwa kuwa udugu wao umeunganishwa na mapenzi.ni marafiki,tena mke ni mama yako kwa upande mwingine,na mume ni baba yako kwa upande mwingine.yaani unapaswa kumuheshim mumeo au mkeo km mzazi wako.na unapaswa kufurahi nae km rafiki yako,na ku du nae kama mpenzi wako.
 
Japo ilishajadiliwa si vibaya nikirudia hapa tena kuwa. MKE NA MUME NI MAADUI WANAOLALA PAMOJA. Kama huamini ngoja mmoja akimchoka mwenzi wake.
 
Undugu.....tafsiri yake ni kuwa unatokana na damu au ndoa. Hivyo basi mume na mke ni ndugu
 
hayo yote naona mnapoteza muda mimi mke wangu sijui ni rafiki au ndugu kwa sababu nayokutana nayo siamini kama anweza kuwa ndug au rafiki huo ni ujusiano upo kwa muda mambo yakienda vibaya basi kila mtu anachukua zake
 
Back
Top Bottom