Mke hasidi, Tena hasidi kwelikweli !

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,780
Wadau ni imani yangu mmeamka salama.
Katika hali isiyo ya kawaida, ndoa ya mfanyabiashara maarufu wa Nazi hapa mjini kwetu, iliingia utata yapata miaka miwili iliyopita.
Mke wa mfanyabiashara huyu ( jina ndani ya hifadhi) aliamua kurudi kwao yapata miaka miwili sasa, huku akiwa amefungua kesi ya kudai talaka.
Hata hivyo ziko habari zenye uthibitisho kua mke huyu sababu zilizomfikisha kudai talaka ni baada ya kua amepata bwana wa nje anaempagawisha.
Hivyo katika kuhakiki malengo yake yanakua ikamlazimu kubumba jambo ambalo lingezaa yeye kutalikiwa.
Ndipo alipotoka na tuhuma ya kwamba mumewe anamwendea kinyume na maumbile.
Kesi ikapelekwa kote kwenye mabaraza ya awali ya usuluhishi, ambapo kote huko Mme alionekana na hatia na akaombwa aridhie kutoa talaka.
Hatimae kesi ikafika mahakamani, na siku ya hukumu habari zikawa hivi :-
- Hakimu : Mama unaweza kuithibitishia mahakama kua mumeo alikua akikuendea kinyume na maumbile ? Naomba jibu moja ndiyo au hapana.
- Mama :
Ndiyo
- Hakimu :
Unaweza kuiambia mahakama ni mara ngapi mumeo amekuingilia huko nyuma ?
- Mama :
Mara 5 au 6 hivi !
- Hakimu :
Kwa nini hukumfungulia kesi pale tu mara ya kwanza alipokutenda hivyo ?
- Mama :
K i i m y a a a !
- Hakimu :
Kwa hiyo Mama umefanywa mara ya kwanza , ya pili, ya 3 !, ya 4 ! , ya 5!, ya 6 !
Unasubiri tu, (mpaka dot inakua 0 ! ) kipi kilikufanya unogewe ?
na usichukue hatua haraka ?
- Mama :
K i i m y a a a !
- Hakimu :
Mahakama inamuacha huru mumeo kuanzia muda huu, baada ya kujiridhisha hii ni kesi ya majungu na ya kupangwa, na kudhalilisha.
Aidha mahakama imejiridhisha kumshauri mume kwamba mke huyu ni hatari kwa maisha yako ikiwa utapenda uishi nae, ama umuache yote yanabaki ktk maamuzi yako.
> Haikupita dkk 15 mume akawa ameandika talaka hapohapo kotini.
 
Mbona sijaelewa hapo hakimu anasema Mahakama imekuachia huru wakati mume hana kesi! ni mama tu alikuwa anadai talaka.
 
Mbona sijaelewa hapo hakimu anasema Mahakama imekuachia huru wakati mume hana kesi! ni mama tu alikuwa anadai talaka.

kumuingilia mtu kinyume na maumbile hata kama ni mkeo wa ndoa ni kosa la jinai. Ndio maana hakimu akasema mume hana hatia kwa kuwa ushahidi hautoshelezi kumtia mtuhumiwa hatiani.
 
hii mambo imeshamiri sana huko pwani, sisi huku kwetu hata kunyonyana ulimi ni uchafu
 
Mbona sijaelewa hapo hakimu anasema Mahakama imekuachia huru wakati mume hana kesi! ni mama tu alikuwa anadai talaka.

Nadhani hukunisoma vizuri, ni kwamba mashtaka ya mke ni yalikua ni Kuingiliwa kinyume na maumbile ! Kosa ambalo lingethibitika lingetolewa adhabu, na yote kwa yote mke akawa anadai talaka.
 
Mkuu judgement napita tu hapa.
MAPROSOO.

Maprosoo as kwon as BawaPopo, nakukubali kweli currently umemrudia Mola ! Sikuoni majukwaani mida ile ya nite kali na msuli wa chukuchuku tangu umebadili ID au X 1 , 1 unavinjari ?
 
kumuingilia mtu kinyume na maumbile hata kama ni mkeo wa ndoa ni kosa la jinai. Ndio maana hakimu akasema mume hana hatia kwa kuwa ushahidi hautoshelezi kumtia mtuhumiwa hatiani.

Mdau wewe! Yaonekana tumesomea fani moja nini ? Kule Lushoto .
 
Back
Top Bottom