Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,346
- 33,183
Mke au Mtoto Wako Yupi wa Kumuokoa? Amuokoa Mkewe
Stacy Horton kulia akiwa ameshikilia picha ya mtoto wake aliyezama, kushoto ni mke wake Vanessa Tuesday, December 01, 2009 3:15 AM
Baba mmoja wa nchini New Zealand alikuwa na wakati mgumu wa kuchagua yupi amuokoe kati ya mkewe au mtoto wake wa kiume wakati gari lao lilipozama kwenye kina kirefu cha maji. Ulikuwa ni wakati mgumu wa kutoa uamuzi wa haraka wa kuchagua yupi wa kumuokoa kati ya mke na mtoto wakati gari la familia lilipodumbukia na kuzama kwenye mto wenye kina kirefu cha maji.
Stacy Horton aliamua kumuokoa mke wake aliyekuwa akipiga kelele akitapatapa kwenye maji akijaribu kujiokoa baada ya kufanikiwa kutoka kwenye gari lao ilililokuwa likizama huku mtoto wao wa kiume Silva akiwa amenasa ndani ya gari hilo mita 4.5 chini ya maji.
"Nilijaribu kupiga mbizi chini kumuokoa mtoto wangu lakini sikuweza kulifikia gari alilonasa ndani yake, kitu kilichonijia akilini ni kumuokoa kwanza Vanessa", alisema Horton akiongea na televisheni moja ya habari nchini New Zealand.
"Nilifanikiwa kumpata mkewe wangu na kumuokoa na tulikaa naye pembeni ya mto huku tukiziona taa za nyuma ya gari kwa mbali, tulibaki tukilia huku tukisali".
"Nilikubali kuwa ndio ameishatutoka, sikuwa na uwezo wa kufanya chochote cha kumuokoa", alisema Horton.
Vannessa alikuwa kwenye gari pamoja na mwanae mwenye umri wa miaka 14 siku ya jumamosi jioni wakati gari lao liliposerereka kwenye ukingo wa sehemu yenye mwinuko na kudondokea kwenye mto unaopita karibu na nyumba yao katika mji wa Wanganui nchini humo.
Rafiki yake Silva, Robert Palmer ambaye naye alikuwa kwenye gari hilo alifanikiwa kujiokoa toka kwenye gari hilo wakati lilipoanza kuzama na kuwahi kumpelekea taarifa Horton kuhusiana na kuzama kwa mwanae na mkewe.
Baada ya Horton kufanikiwa kumuokoa mkewe, maafisa wa polisi walijaribu kupiga mbizi kumuokoa Silva lakini walishindwa kulifikia gari alilokuwemo.
Zimamoto nao waliingilia kati kwa kujaribu kulivuta gari hilo karibu ili kumuokoa Silva, lakini mpaka walipofanikiwa kufanya hivyo, Silva alikuwa ameishaiaga dunia. http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3655490&&Cat=2