Mke anashinda Kanisani !!

HIVI NI KUSEMA ANAMPENDA YESU ASIYEOMWONA N KULIKO WEWE MUMEWE??. NA UKIJARIBU KUMWELEKEZA ANAKUIMBIA VIPAMBIO Eti "HAKUNA MWANAUME KAMA YESU ......HALELUYA (Mipasho ya dini)

..

sijacheka siku nzima..
kwakwakwakwa!!!
Ngoshwe u've made my day Thanks!
 
Acheni ujinga nyie, hivi mkiambiwa Mungu na mume bora nini? mume si udongo tu, Yesu alishasema na watu kama nyinyi kuwa, mtu kama hataacha familia yake ni kunifuata, hataurithi uzima wa milele, hakumaanisha uwachukie au uondoke home, bali alimaanisha kuwa, unatakiwa umuweke Yeye wa kwanza ktk kila kitu, Yesu ni mwa muhimu kuliko mume wako au mke wako. Mungu ndiye mwumbaji wetu unajua?....Mungu anatakiwa aheshimiwe kuliko hata mume wako, Mungu anatakiwa atafutwe kuliko hata mume wako, hata kama utapita kwenye moto alimradi unamtafuta Mungu ni bora.

Huyo jamaa ashukuru sana Mungu kwamba mke wake anashinda kanisani. kwasababu anamuombea na yeye, na pengine anaishi leo kwa maombi ya mke wake tu. kuna watu hivi ninavyoongea wanalia mchozi, wanatamani wake zao wangegusa hata uwanja wa kanisa tu, wanatamani wanawake wao wamche Mungu, lakini wapi, wanashinda kunywa mipombe, wanashinda wakitoka nje ya ndoa, hawana hata hofu ya Mungu katika mioyo yao.

Kukimbilia kwa Mungu kuna faida sana. huwezi jua kwanini huyo dada kakimbilia kanisani, inawezekana kuwa ameamua kwenda kanisani kwasababu tu Mungu amemgusa, akaamua kuokoka. pili ni pengine ameenda kanisani kutokana na matatizo ya kindoa ambayo huyo mwanaume anayo, angeongea yeye ndo tungepata picha halisi.

ila kwahabari ya kwenda kanisani, nawatangazie enyi nyote msioenda kanisani, msiookoka na kumpa Bwana Yesu maisha yenu kama Bwana na mwokozi wa maisha yenu, bora mfanye hivyo mapema kabla usiku haujaingia, mtakapotafuta hata mtu wa kuwahubiria tu msimpate, mtakapotafuta walau hata pambio au nyimbo za dini lakini hamtazipata....wale wote waliompokea Bwana Yesu watakuwa wameshanyakuliwa na mpinga kristo atakuwa ameshaanza kuwatandika fimbo hapa duniani. MTAANI NINAPOKAA KUNA MAMA ANAFANYA KAZI NZURI SANA, anaendesha magari mazuri sana ya garama, ana nyumba nyingi zingine masaki, lakini anakunywa pombe, anakuja amekunywa kila siku. pamoja na usomi wote, kuendeshwa na mashangingi mazuri, ANAPIGANA NA MME WAKE KARIBIA KILA SIKU. mmewake hanywi, yeye akirudi amelewa anamfanyia fujo mmewe.

Heri enyi mnaowaruhusu wake zenu kwenda kusali kumtafuta Mungu, kwasababu kwa mafundisho ya Mungu wanayoyapata watawafundisha na watoto wenu wakakulia katika njia ya Bwana, kuliko watoto wakakulia kwenye kufuga malasta, kuvuta mibange, kusuka nywele kama wanawake na mwishowe kuvaa heleni kama wanawake. kuna faida kubwa sana kumruhusu mkeo aende kanisani kumtafuta Mungu. kila mtu ataubebe msalaba/furushi lake peke yake mbele za Mungu, wewe kama unakatanzwa na mme wako usiende kanisani na unakubali, utaenda naye motoni. Mungu ni wa muhimu kuliko mume. mumeo akifa leo si utabaki na Mungu? au na wewe utakufa? kama hauombi na kumtafuta Mungu, tumaini lako ninini, ni mume wako? Mungu na awasaidie sana. natamani ningekuwa pauloniwaite wagalatia msiokuwa na akili....

Mathayo/ Chapter 15 13. (Bwan Yesu ) Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.
14. Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

Bwana Yesu Kristo hakuja kufundisha Wanawake Waache Waume zao wakeshe Makanisani hiyo katika Dini hakuna kuna wakati Maalumu wa kufanya ibada ikiwa kila asubuhi na jioni au kila siku ya Jumamosi na Jumapili,sio kila wakati mke aache kufanya shughuli zake za nyumbani akeshe Makanisani akiomba Mungu hayo Bwana Yesuı Kristo hakufundisha hivyo. Kama kuna mtu anao ushahidi atowe kwenye Biblia . itabidi mume wa huyo Mke aende kumshitaki kwa Mchungaji pale anapofanya ibada aone Mchungaji atamuambia nini kuhusu Mke wake kuacha tabia ya kushinda Makanisani. Kama anaona Kukesha Kanisani bora kuliko kuangalia Familia yake mbona anafanya kazi? Sio bora aache kufanya kazi akeshe Kanisani? Anafanya kazi na wakati wa kazi ukimalizika anakwenda Kanisani Ehh kasheshe hiyo itabidi mume wake huyo Mwanamke aende kumshitaki kwa Mchungaji ili mke wake aweze kujirekebisha hiyo tabia yake asante.
 
Actually, kukesha kanisani bila makubaliano fulani na mmewe, si busara, pamoja na kwamba wakati mwingine inaweza uwa si dhambi. ninachosema ni kwamba, inategemeana na mazingira, ndio maana tunashauri upande wa pili yaani uyo mama angekuja na yeye aeleze hapa, hapo ndo tungepata picha kamili. kung'ang'ania kumchambua huyu mama wakati hatujui mazingira halisi hasa upande wa pili wa mama, ni kujilisha upepo, kutwanga maji. mistari uliyoikoti hapo juu, haiendani kabisa na kinachojadiliwa hapa, unahitaji kusoma Bible kwa upyaaaa, nashindwa nikusaidieje.
 
Sio mkeo tena huyu huko makanisani wanawake wamekuwa wake za viongozi au wauumini wenzako,muache ili upate mapozo ya moyo kwa mwingine usije ukafa bure mtoto watu mamako akazimia bure
 
Rafiki yangu analalamika....,

.................. amebobea kuliko hata "mama mchungaji",

Hivi hali inapofikia hivi, tunajenga au tunabomoa??...

Pengine tayari ameshapandishwa cheo na kuwa mama mchungaji. siku hizi hayo yapo. fanya uchunguzi ktk makanisa mengi ya ki upakao utakuta kuna mwanamke mmoja au wawili wako karibu sana na mch kuliko hata mama mchungaji na wanajiremba kuliko mama mchungaji. Na ukiwachunguza mama wachungaji wengi usoni wanakuwa na simanzi fulani. It is as if they are being bullied.
 
Actually, kukesha kanisani bila makubaliano fulani na mmewe, si busara, pamoja na kwamba wakati mwingine inaweza uwa si dhambi. ninachosema ni kwamba, inategemeana na mazingira, ndio maana tunashauri upande wa pili yaani uyo mama angekuja na yeye aeleze hapa, hapo ndo tungepata picha kamili. kung'ang'ania kumchambua huyu mama wakati hatujui mazingira halisi hasa upande wa pili wa mama, ni kujilisha upepo, kutwanga maji. mistari uliyoikoti hapo juu, haiendani kabisa na kinachojadiliwa hapa, unahitaji kusoma Bible kwa upyaaaa, nashindwa nikusaidieje.

Mzee Ubungo2,

Naweza kufahamu toka kwa maelezao yako kuwa wewe ni muumni wa kweli, umeoa, unafamilia na unafahamu vyema matatizo ya ndoa. Utakuwa unajua siri ya kutatua matatizo ya ndoa inayodumu kuwa kamwe huwa hakuna dhana ya kimahakama ya kusikiliza hoja za pande zote mbili mpaka mwisho ikiwemo kuita mashahidi. Pia katika ndoa hakuna kitu kinaitwa hukumu ya huyu ameshinda na yule kashindwa kama mahakamani. Ukijaribu kufanya hivyo, sikuzote familia itakuwa na mafarakano makubwa kwani kwa mfano katika ugomvi kati ya Mkeo na Mama yako mzazi, ukiwakarisha chini wote wakueleze chanzo, wewe utaishia labda kumwona mama yako hafai milele au kuachana kabisa na mkeo. Ukiacha Mahakama za Kidunia, mara nyingi inashauriwa kuwa kesi za ndoa zinazohitaji suluhu ya kuendeleza ndoa zinapofikishwa mbele ya msuluhishi, ni kweli kujaribu kuitengeza kesi ya dhanio (hypothetical case) na sio kuuliza kina mmoja aelezeee mpaka mwisho nini kilitokea na nani shahidi wake. Utasikia mengi na utaishia katika kuongeza mafarakano zaidi ya kutatua mgogoro.

Ndoa ina mambo mengi sana, na makuu ni haya:
  1. yapo ya chumbani yaani yale wanayoyajua wahusika tu (hayo huwezi kuthibitisha kwa ushahidi wa mtu wa tatu (kubali tu yale unayoweza kuelezwa au kujua kwa busara zako za kimaisha kuwa uenda yapo au yasiwepo).
  2. Kuna mambo ambayo wewe kama mume au mke huwezi kuyajua kabisa pengine mpaka utakufa au kuachana na mwezio (yawezekana haya mwenzio anayajua fika na ni siri kuu sana kwake hata ikiwa kufa yupo tayari na hawezi kukuambia kamwe labda akijisikia (kwa mfano kujua kiuhakika kama mwenzio amewahi kujihusisha au mahusinao ya kimapenzi na mtu mwingine, huwa aridhika kabisa anapokuatana na wewe au analazimika tu kuwa na wewe nk).
  3. Kuna yale ya Sebule na kwingineko (wanayojua wanajamii) pengine hata wewe mwenyewe au mwenzio hajui (kwa mfano ndugu na marafili zako wanaweza kujua fika tabia za mkeo/ mume na wanasita kukueleza kutokana na ulivyo au kupogopa kuvunja mahusiano yenu)
  4. Yapo yale ambayo unaweza pia kuyasikia au kuyajua katika maisha ya kila siku na pengine hata kama ni ya muhimu ukayaona ya kawaida au hata ukiambiwa huwezi kuayaamini ukasema unaongopewa na pengine usitafiti ukweli juu yake.
Wakati mwingine, wataalamu wanasema kujua ukweli wa jambo, waweza kupima kwa kusikiliza maelezo ya visa vingi vinavyofafana na kukubali kuwa kesi kama hii inawezekana kuwa ipo na ukimtaka mhusika ajieleze, unaweza kuishia kuambiwa kuwa anasingiziwa au hakuna jambo kama hilo (kwani siku zote hakuna aliye tayari kuiteketeza nafsi yake kwa kusema ukweli hata ikiwa mbele ya madhabahu ya MUNGU.

Yawezekana kwa kiasi kikubwa sana matatizo mengi katika ndoa chanzo chake huwa ni jitihada za kila mwanandoa kutafuta amani na furaha katika ndoa yake. Kwa mfano kwa kusikiliza visa vingi, yawezekana kuwa inapofikia mke anaenda mpaka kwa waganga wa kienyeji, anakunywa mipombe hovyo au kutoa "tunda" nje ya ndoa, huwa ni hatua ya kujaaribu kupigania ndoa yake hususan pale mumewe anapoonekana kwenda kinyuma. Kwa kudhani kuwa mumewe akiona nae anafanya vile basi atarejea pasipo kujua kuwa ile staili anayoitumia ndo inazidi kuchochea moto kwa maana ya kulipiza kisasi.

Kwa matazamo huo huo, hata pale Mke anapoamua kwenda kushinda ndani ya kanisa, muda wote, haimaanishi ni usafi wa moyo ndio uliomvuta aende kanisani na kwamba huko hawezi kufanya kama ambavyo angeenda baa, kwa mganga wa kienyeji nk. Aidha, kwa kuwa Kanisani, pengine inaweza isiwe suluhisho kwani bado huko nako sio wale wote anaokutana nao na kuwaeleza shida zake za ndoa na kuomba wamuombee au waombe pamoja nae hata ikiwemo Baba Mchungaji ni watu wema, kwani kila mtu yupo kanisani kwa makusudi maalumu na wengi ni shida ndo zinawafanya wamjue Mungu hata kukesha makanisani kwa staili ya kinafiki.

Na ikumbukwe kuwa si kila aitae jina la Mungu moyoni mwake anamaanisha MUNGU wa KWELI au ana huyo "MUNGU"...na sio kila anayedai kuwa anashughulika na matatizo ya ndoa za watu huwa anafanya hivyo kwa wema. Wapo wanandoa wengi ambao wamepoteza amani kutokana na kujaribu kuitafuta hiyo amani huko makanisani ikiwemo kwenda kueleza shida zao kwa hawa wanaoitwa "WACHUNGAJI" au kusimama mbele ya madhabahu na kutangaza shida zake ili kanisa limuombee...(hapo yupo peke yake au na watoto tu huko kanisani).

Baadhi ya hao wachungaji wakijua nini kilichokuleta hapo kanisani, basi inakuwa ndio siri ya yeye kukufikia "kibinadamu"..utatumika kiroho na kimwili, utatoa kila ulichokuwa nacho, na kwa akina mama huwa kama ilivyo kwa wanaume wengi tukisikia yupo kanisani au kwa Baba Mchungaji, hisia hazitutumi kuwa huko hawezi kutenda jambo baya...hawezi kutoa mapato yoote ya ndani kwa ajili ya kuilisha familia ya Mchungaji, hawezi kuanika siri zote za ndoa weye na hata akifanya hivyo, Mchungaji atazibariki kama kwamba mchungaji yeye hana matatizo ya ndoa na yupo karibu sana na MUNGU!.

Kwa nini inasemwa kuwa ufumbuzi wa matatizo ya ndoa ni ninyi wawili? ...ikiwa utamweleza mtu shida zako hata akiwa baba au mama yako mzazi, ufumbuzi atakao kushauri unaweza kuupokea kama mwezio hayupo tayari kwa ufumbuzi huo??...na kama unaweza kusali kanisani na mchungaji au waumini wengine kila siku kuombea shida za familia yako, Mungu hawezi kukusikia na kukusaidia ukikaa na familia yako nyumbani kusali kwa ajili ya jambo hilo na mengine??. Je, ni lazima uhamie na Kanisa au dhehebu pale unapatwa na shida za kimaisha??.

Iwapo mumeo au Mkeo amepotoka na anakwenda kinyume na maadili ya ndoa, je njia iliyo njema machoni pa MUNGU ni kutumia muda mwingi sana kuwa mbali nae ikiwemo kushinda makanisani au ni kujitahidi kuwa karibu nae na kumshawishi ili abadilike ili ikibidi mwende wote huko kanisani na sio kwenda peke yako huko kwa waumini na mchungaji kuomba maombi ya kumkemea mwenzio kama pepo na badae kutangaza wokovu juu yake??.
 
umekisia vyema ngoshwe, nimeoa na ninawatoto. mke wangu mimi hatusumbuani kabisa kwasababu tumeokoka na tunampenda Yesu. zamani nilikuwa msumbufu sana, kwa maombi yake, Mungu akanibadilisha na tupo wote kwasasa, namshukuru Mungu kwa kumtumia mke wangu kubadilisha njia mbaya nilizokuwa nazo. ninachosema hapa, ni kwamba, sio kwamba tupo mahakamani kuhukumiana, nilikuwa naona watu wanapoteza muda kujadili jambo ambalo hawajui chanzo, hawajui kiini, ni topic tu imeletwa, na watu wameanza kumshambulia huyo mama, kumbe pengine uyo baba ndo msumbufu na wa kulaumiwa...akakimbilia hapa kwetu kushitaki. si unajua zamani wakati tunakua kijijini, dogo akiiba mboga au nyama kwenye chungu anakuwa wakwanza kujitetea mbele za maza ili aonekane yeye ni mwaminifu, anawasingizia wenzie. ukija kuwaweka wote pamoja na kucharaza fimbo, utagundua yule aliyekuwa anajipendekeza kuwa mwema ndo alikuwa mdokoaji wa kwanza.

tusipende kupoteza muda kwa majadiliano ambayo hatuyajui kiini, kama huyo mama angekuwa hapa naye ajibu kwa thread, tungepata jibu. tukiendelea hivyo hapa, tunakuwa kama tunawacharaza fimbo wanawake wote, hata wale ambao wanaenda kanisani na hawakatazwi na waume zao, unaweza ukafanya wanaume humu ndani wakifika home wakabadilisha sheria. hakuna faida yoyote kujadili jambo ambalo haulijui kiini chake na upande wake wa pili. I tell you, si mahakamani tu, hata kwa mambo ya chumbani, usihukumu upande mmoja, hukumu yaupande mmoja siku zote ni dhuruma. hata watu wakigombania unyumba ndani, au kitu chochote cha chumbani, utapata solution kama utawaweka wote pamoja chini ya mshenga. so, please, hii thread iishe, kwasababu inakuja kisiasa na kichuki mno, watu wengi wanaoongea humu ndani wana chuki binafsi na kile wanachoita makanisa mapya ya siku hizi, yale ya kuokoka. wanakuwa na chuki, ukiangalia yote yaliyojadiliwa humu wengi wanakuwa biased waziwazi kwasababu huyo mama kaenda kanisa wasilolipenda, ndo maana hawana hata point ya kushikilia. jambo hawalijui, wamesikia jamaa kaandika jujuu tu, wao hadi mapovu yanawatoka. mtaumiza mioyo bure, Tanzania ni nchi inayotoa uhuru wa mtu kuabudu dini na dhehebu alipendalo, msiwachukie watu wa madhehebu mengine.
 
Hilo sio kanisa bali ni kitu kingine. Vp mchungaji wake ni yule wa viti maalum CCm asiye ishi na mume?

Huyu atakuwa ni yule Nabii aliyemvuruga yule Wakili na yule Dr wa Liberia !:laugh:
Ngoja tupate burudani za Wagalatia !:becky:
 
Sidhani kama dini ndio ya kulaumiwa ... hivi kuna dini za kisasa?dont think so... but i think she should set her priorities and time management is the key to her problem... the only problem i c there is if she will realize that whatever she is putting herself into could affect ppl around her...

I have a living example of this kind of woman and tell you what... she never ever think that this is a problem... she goes to the Fatwa (in the Islamic faith is a religious opinion concerning Islamic law ) everyday or 5 days a week. at the same time she neglects her children and husband... she has a teenager boy who started smoking and do all that bad boys stuff... while she is busy attending these Fatwa... once when she started preaching me on something, I told her oow come on at least I know what is going on in my own house.....

............Wagalatia watakuelewa kwelii !???:A S wink:
 
Actually, kukesha kanisani bila makubaliano fulani na mmewe, si busara, pamoja na kwamba wakati mwingine inaweza uwa si dhambi. ninachosema ni kwamba, inategemeana na mazingira, ndio maana tunashauri upande wa pili yaani uyo mama angekuja na yeye aeleze hapa, hapo ndo tungepata picha kamili. kung'ang'ania kumchambua huyu mama wakati hatujui mazingira halisi hasa upande wa pili wa mama, ni kujilisha upepo, kutwanga maji. mistari uliyoikoti hapo juu, haiendani kabisa na kinachojadiliwa hapa, unahitaji kusoma Bible kwa upyaaaa, nashindwa nikusaidieje.

UISLAA:

Mwanamke hatoki ndani ya nyumba bila ya rukhusa ya Mumewe, hilo limehukumiwa.
Mwanamke anahimizwa ibada zake kufanyia nyumbani !
 
unajua biblia inasema 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'

pepo kashaingia hapo in the name of kushinda kanisani huyo mume ana kazi ya ziada aombe Mungu sn.
unajua watu wanashindwa kuelewa issue sio kushinda kanisani wala sio dini
 
Mathayo/ Chapter 15 13. (Bwan Yesu ) Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.
14. Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.

Bwana Yesu Kristo hakuja kufundisha Wanawake Waache Waume zao wakeshe Makanisani hiyo katika Dini hakuna kuna wakati Maalumu wa kufanya ibada ikiwa kila asubuhi na jioni au kila siku ya Jumamosi na Jumapili,sio kila wakati mke aache kufanya shughuli zake za nyumbani akeshe Makanisani akiomba Mungu hayo Bwana Yesuı Kristo hakufundisha hivyo. Kama kuna mtu anao ushahidi atowe kwenye Biblia . itabidi mume wa huyo Mke aende kumshitaki kwa Mchungaji pale anapofanya ibada aone Mchungaji atamuambia nini kuhusu Mke wake kuacha tabia ya kushinda Makanisani. Kama anaona Kukesha Kanisani bora kuliko kuangalia Familia yake mbona anafanya kazi? Sio bora aache kufanya kazi akeshe Kanisani? Anafanya kazi na wakati wa kazi ukimalizika anakwenda Kanisani Ehh kasheshe hiyo itabidi mume wake huyo Mwanamke aende kumshitaki kwa Mchungaji ili mke wake aweze kujirekebisha hiyo tabia yake asante.

u a very ryt
watu hawaelewi biblia wanakurupuka
kusali kuomba ni popote na wakati wowote sio lazma ukakeshe kanisani ili mradi uwe una abudu halisi ktk roho na kweli, coz haya mi mambo ya rohoni.na hao ndo wanaowafanya walokole waonekane wamechanganyikiwa wasio jua nn wanafanya

huyo ana pepo sio bure na asipoangalia hyo ndoa inavunjika, lucifer ana trick na yupo makini kuliko watu wanavyofikiria huwa hamisi opportunity anapoipata
 
makanisa yanayoibuka kila kukicha ni hatari,huyo mmewe atumie busara sana,ilo tatizo linaitwa ugonjwa wa dini,kumpenda Mungu wala hakuvunj ndoa bal kuimalisha,pepo uyo kwa stail yake.but wahusishe wazee waliodumu kanisan mda mwing yataisha
 
Akiwa anamuliza muliza na kumsihi ndiyo anampa kichwa. Yeye amuache hivyo hivyo huku akiendelea na mambo yake. Siku huyo mke akija kukumbuka shuka atakuwa ameshachelewa.
 
makanisa yanayoibuka kila kukicha ni hatari,huyo mmewe atumie busara sana,ilo tatizo linaitwa ugonjwa wa dini,kumpenda Mungu wala hakuvunj ndoa bal kuimalisha,pepo uyo kwa stail yake.but wahusishe wazee waliodumu kanisan mda mwing yataisha
Ni shida watu hawana ethics za kichungaji mchungaji hana ratiba. Jana mama watoto to be kaja saa moja usiku ameshinda siku nzima kanisani kisa alikua amealikwa kwenye kanisa lingine ye na wanakwaya, nilishamwambia aondoke huko ila hataki nataka nimsuprise
 
Back
Top Bottom