kama mchawi kweli si awatie uchizi magamba wote!!!!
Mimi nimezishuhudia....habari za huyu bibi nazisikia sana!
Katika hatua nyingine Kikongwe Somoe Issa (90) ambaye ni mkuu wa kaya ya Msimbati, kijiji ambachogesi asilia inavunwa ameionya Serikali kutoendelea na mpango wake wakusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.
Kikongwe huyo ambaye haoni wala kusikia alisema hayupo tayari kuona gesi hiyo ambayo imepatikana katika kijiji hicho ikiondoka mkoani Mtwara.
"Atakayejaribu kuondoa gesi hii kitakacho mkuta atakijua yeye mweyewe…ninasema gesi isiende kokote…iwapo atabisha inawezekana akasafirisha maji tu na isiwe gesi yenyewe"alisema bibi huyo kupitia kwa mkalimani wake Asha Hamis
Aliongeza kuwa,"mwaka walioanza kuchimba(2005) walifika hapa bila kubisha hodi, wanajua kilichowakuta…bomba lilikuwahaliendi chini wala kurudi juu…walinifuata hapa nikaenda kufanya tambiko"
SOURCE: MWANANCHI
Yale yale, uchawi, ushirikina, matambiko, uganga, ujinga......
haoni wala hasiki....sasa kajuaje hayo mambo.........jf siku hizi imekuwa kama sehemu ya udaka na umbeya tu...... Imepoteza sifa kabisa.... Mods topic kama hizi ni kuzitoa tu mana hazina ukweli bali ni umbeya tukatika hatua nyingine kikongwe somoe issa (90) ambaye ni mkuu wa kaya ya msimbati, kijiji ambachogesi asilia inavunwa ameionya serikali kutoendelea na mpango wake wakusafirisha gesi kwenda dar es salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.
kikongwe huyo ambaye haoni wala kusikia alisema hayupo tayari kuona gesi hiyo ambayo imepatikana katika kijiji hicho ikiondoka mkoani mtwara.
atakayejaribu kuondoa gesi hii kitakacho mkuta atakijua yeye mweyewe ninasema gesi isiende kokote iwapo atabisha inawezekana akasafirisha maji tu na isiwe gesi yenyewealisema bibi huyo kupitia kwa mkalimani wake asha hamis
aliongeza kuwa,mwaka walioanza kuchimba(2005) walifika hapa bila kubisha hodi, wanajua kilichowakuta bomba lilikuwahaliendi chini wala kurudi juu walinifuata hapa nikaenda kufanya tambiko
source: Mwananchi