Mkataba wa Lights (RITES

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Du!!!!!!!!! Uandishi gani huu yaani hizi L na R zinaleta shida mpaka Tasnia ya habari inapoteza umakini kiasi hiki????- ina maana huko Mwananchi hata proof readers hamna?

Mkataba wa Lights lazima uvunjwe-Trwawu

source: Hapa

Send to a friend Saturday, 29 January 2011 09:35 0diggsdigg

Lilian Lucas,Morogoro

KAMATI Kuu ya Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu), imeiomba serikali kutekeleza ahadi yake kuhusu kuvunja mkataba wa Kampuni ya Lights.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa Trawu,Sylivester Rwegasira, alisema serikali kupitia kikao cha Bunge la mwisho, ilitangaza azma ya kuvunja mkataba wa Kampuni ya Lights, lakini hadi sasa haijatekeleza ahadi hiyo.

Alisema Trawu imesikitishwa mno na itendo hicho ambacho alikiita kuwa ni cha kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi wa Shirika la Reli.

Rwegasira alisema ahadi hiyo ya serikali haikuwa ya kweli hasa ikizingatiwa kuwa menejimenti ya Lights, bado inaendelea kufanya kazi ikiwa ni pamopja na kukusanya mapato ya Kampuni ya TRL.

Alielezea kushangazwa kwake juu ya serikali kutochukua hatua dhidi ya kampuni hiyo, ambayo imekuwa ikiitia hasara Tanzania.

Hata hivyo kamati kuu hiyo imetoa muda wa wiki moja kwa serikali kuhakikisha kuwa menejimenti ya Kampuni ya Lights, inaondolewa katika kusimamia shughuli za uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania na kutoa nafasi kwa kamati ya wazawa kusimamia shughuli hizo katika kipindi cha mpito.


Katibu huyo alisema kama serikali haitafanya hivyo, suala hilo litafikishwa katika ngazi ya wanachama ili ikibidi wagome kufanyakazi.

"Tunadhamiria kuchukua sheria kama serikali haitasikiliza madai yetu," alisema Rwegasira .
 
Duh, hiv kumbe huu mzima bado unaendelea kula kwetu. Bongo tuna kazi kubwa mpaka tupate uhuru.
 
My GOD, ni kweli hawa wahindi bado wapu? Nakumbuka na DG alishateuliwa kama sikosei bwana Kisamfu!!! How comes kwamba Rites is still managing?
 
Back
Top Bottom