Mkataba wa Bandari wanaoona ni mbaya na wanaona ni mzuri kaeni meza moja

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,651
1,895
kwa nini wa africa tunapenda ugomvi ?kama mkataba bandari kati ya Tanzania na DP World kuna wanaona ni mkataba ni mzuri na wengine ni mbaya kwa nini wasiitane wakakaa pamoja wakaelewashana mambo yakaisha kuliko kutukanana na kupelekana police na mahakamani? wanaolumbana wote ni wantanzania ambao wanataka kila kitu kiende sawa.

unasikia huyu anasema kapewa hela ili aitetee DP world ,mwingine utasikia huyu kanunuliwa ili aipinge DP world.sasa mnazua taharuki kwa taifa.embu itaneni mkae pamoja mwelekezane kwa amani yaishe tujenge nchi kwa pamoja.acheni siasa sana ,acheni wivu .mnawachanganya wananchi.

mimi siamini kuwa wanaopinga ni waongo 100% maana tumeona wanasheria nguli kam Prof SHIVJI,TLS,NK kweli hawa wote wamenunuliwa kwa pamoja wamewekewa hela kwenye accout kila mmoja kwa nyakati tofauti?na kama ni hivyo TAKUKURU kazi yake ni ipi? BOT ilishindwa kujua kuwa hizi hela zinazoingia kwenye makaunti kwa fujo ni za nini?wakati wananunuliwa inteligensia yetu haikufanya kazi kiasi hicho? nchi haiko salama kiasi hicho?common guys !!!!nchi yetu ni ya ummoja lakini kwa nini hatuna umoja tunapoendesha nchi yetu?shulenitunasoma paomoja ,tunaka madawati pamoja,tuna discuss pamoja ,tukifiwa tuko pamoja .lakini siasa hatuko pamoja ,kuendesha nchi hatuko pamoja!!!this is more satanic style .

lakini pia wanaotetea DP world nao siamini kuwa wako wrong 100%.kilichotakiwa kwa kundi hili kwa sababu ndilo lenye dhamana la kuisimamia serikali na kuhakikisha linaleta maendeleo ni kuwaita wanaopinga mkae meza moja. CCM ndiyo inashikilia msimamo huu kwamba mkataba wa DP World ni mzuri.sawa.kwani hii ilikuwa ndiyo teke ya mwisho ya kupata kura 2024 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa? ndiyo teke ya mwisho ya kupata kura kwenye uchaguzi mkuu 2025? au tunapenda ugomvi tu usiyokuwa wa maana? ina maana CCM haijaona kabisa kwamba swala hili laweza kusambaratisha muungano? kweli?

TUSIPENDE KUENDEKEZA UGOMVI USIYOKUWA NA SABABU ZA MSINGI .KIBRI HAKISAIDI

Leo vita kati ya URUSSI NA UKRAINE ni matokeo ya kiburi cha USA iwaongoza NATO,ni matokeo ya kiburi cha viongozi wa ukraine na rassia.na bado hatujifunzi

Duniani hakuna amani kwa sababu ya kiburi cha viongozi na watu fulani fulani wanaojiona kuwa wanajua kuliko wengine.
 
Wacha upumbavu, DPw hakuingia mkataba Na waafrika wote bali na Wanzibari wakiidalali Tanganyika. Ndo ujiulize kwanini Wanzibari wanapoenda ugomvi not all Africans.

Sema Mzanzibar Mpenda ugomvi No. 1. Jecha Salum Jecha ameaga mashindano wiki hii.
 
Back
Top Bottom