Mkapa denounces culture of aid dependency

Ben kakumbuka shuka kumeshakucha!!!

Si huyu huyu mteule wa Mwalimu?

Aliyoyafanya wakati wa utawala wake sote tunayajua.Yeye aliuza almost kila kitu kwa kuwakaribisha "wawekezaji" , wengi wao wakiwa feki.

Suala la kuwakaribisha wachimbaji wanaotuibia kutwa kucha tunalifahamu fika. Net Group Solutions je? Na ufisadi wao nani alilazimishia?

Ni jambo la kisikitisha Ben anakumbuka Ujamaa na Kujitegemea sasa hivi anapoona mambo akiwa nje ya uongozi.

Anachokiona sasa ndo alichokuwa akiaambiwa mara zote, na yeye akijibu kuwa Watanazania "wavivu wa kufikiri".

Hivi na viongozi wavivu wa kuwasikiliza wananchi wao tuwafanyeje?

Yanayotokea sasa hata nchini kwetu Tanzania , muasisi wake ni Ben William Mkapa. Hatushangai sana kwa yanayotokea ingawaje yanatusikitisha.

Tatizo kubwa tulilonalo ni kwamba wengi wetu huangalia nani kasema nini na hapo kumjibu yule aliyesema bila kuangalia ukweli ya yale aliyoyasema!! Mimi binafsi nakubaliana kabisa na hoja kuwa nchi za Africa haziwezi kuendelea kwa kutegemea misaada toka kwa wajomba wa ughaibuni!! Hiyo ndio hoja ya msingi aliyoiongelea Ben; kama Ben hakuliona hilo alipokuwa Rais, inawezekana kuwa sasa ambapo yuko nje ndio amepata mwanga wa kutafakali kwa kina mambo ambayo yalimpita alipokuwa kiongozi!! Mpirani pia , watazamaji wanafulsa nzuri zaidi kugundua makosa ya team kuliko wale wanaocheza na hasa captain wao!!
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni. Kauli ya Mkapa ni kweli tupu ambayo kila mwafrika mwenye mawazo mgando ya kutegemea ufadhili hata kwa ujenzi wa choo chake mwenyewe anatakiwa aelewe. Mbona kinachofanyika ktk nchi zetu ni kubadilishana uzoefu wa kibiashara na kuingia kwenye ubia wa kibiashara wenye kumfaidisha kila mbia lakini tunalazimishwa kuiita hiyo mikataba ya makubaliano misaada? Msaada gani una riba? Hii ni biashara bana. Halafu hebu mtu mwenye data za kupanda kwa ukusanyaji kodi wa mkapa aumwage hapa jamvini. Alipokea kwa Mwinyi kutoka Sh. Ngapi na alimkabizi kikwete zikiwa sh. Ngapi na Mkwere amepandisha kufikia wapi. Pia tusisahau kuainisha hili la ukusanyaji wa kodi na mfumuko wa bei.
 
kuna tofauti kubwa kati ya uwekezaji na misaada

Nakubaliana na wewe mkuu juu ya hilo, lakini tofauti kubwa zaidi ni msimamo wa wenzetu wanosimamia hizo areas mbili.
Katika kuwekeza kunahitajika akili zaidi hasa kwa wewe "unyewekezwa"-nchi inayo attract wawekezaji.
Wanao attract hao investors lazima wafahamu nchi inafaidika nini,Mifano ya 3% royality katika madini ilifanyika wakati wa Mkapa.

Leo Australia ukiwekeza kwenye madini rolaty ni 40%, Australia wanajua wanataka nini katika uwekezaji wa madini.
Hatuna haja ya kueleza mifano mingi mibovu katika hili, ambapo uwekezaji unachukuliwa kama fashion na ni suala ambalo limetushinda miserably.

Kwa walio "dhaifu wa kusumbua vichwa vyao" huendea misaada.
Hii ni omba omba
Kati ya hivyo viwili Mkuu De Novo hebu tupatie data za mahali tulipofanya vizuri na nchi ikafaidika.
Iwe uwekezaji au misaada tumeshindwa kwa sababu kimsingi hatujui tufidike vipi.
Heads or tails we lose
To the layman it is all rot.
 
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uwekezaji na misaada. Hiyo misaada ndiyo gia ya kupata dili la uwekezaji. Rejea hotuba ya JK Sweden!
 
Dondoo ya JK huko Sweden hii, inaonesha kuwa hawa watu hawatoi misaada tu eti kwa sababu wanatupenda - ni kwa sababu wanataka kuwekeza:

"At the moment Tanzania exports very little to Sweden. For instance, in 2005 Tanzania's exports to Sweden were valued at 686,680 US dollars. In 2006 they were worth 515,370 US dollars. On the other hand, Sweden's exports to Tanzania in 2005 were 73.2 million US dollars. In 2006 they were valued at 52.3 million US Dollars. When you look at these figures it is clear that there is a serious trade imbalance between the two countries. But that is besides the point. What is important is for us to do more to increase bilateral trade" - http://www.tanemb.se//index.php?option=com_content&task=view&id=46&Itemid=40
 
Labda JK itamwingia akilini maana ndo huwa anahubili kutembeza bakuli bila aibu
 
Tatizo kubwa tulilonalo ni kwamba wengi wetu huangalia nani kasema nini na hapo kumjibu yule aliyesema bila kuangalia ukweli ya yale aliyoyasema!! Mimi binafsi nakubaliana kabisa na hoja kuwa nchi za Africa haziwezi kuendelea kwa kutegemea misaada toka kwa wajomba wa ughaibuni!! Hiyo ndio hoja ya msingi aliyoiongelea Ben; kama Ben hakuliona hilo alipokuwa Rais, inawezekana kuwa sasa ambapo yuko nje ndio amepata mwanga wa kutafakali kwa kina mambo ambayo yalimpita alipokuwa kiongozi!! Mpirani pia , watazamaji wanafulsa nzuri zaidi kugundua makosa ya team kuliko wale wanaocheza na hasa captain wao!!

Buesi , which Mkapa are you refering to?
Is it the 1st Term Mkapa(1TM) or the 2nd Term Mkapa(2TM).Actualy there is very little resemblance betweenthe two!!
While 1TM was austere,authentic and a product of Mwalimu , one could refer and listen to him. The 2TM is another product altogether, unyielding, aloof had ANBEN philosophy in him, he wouldnt care the least with the wa-Tz so long as he lived happily ever after.
The metamorphosis of the person, between the two will make a very good academic thesis.
All the same an average of the 1TM and 2TM does not make Mkapa an authority to talk of the Mwalimu philosophy.
The truth is pure and simple , he bungled his own legacy
 
Ben kakumbuka shuka kumeshakucha!!!

Si huyu huyu mteule wa Mwalimu?

Aliyoyafanya wakati wa utawala wake sote tunayajua.Yeye aliuza almost kila kitu kwa kuwakaribisha "wawekezaji" , wengi wao wakiwa feki.

Suala la kuwakaribisha wachimbaji wanaotuibia kutwa kucha tunalifahamu fika. Net Group Solutions je? Na ufisadi wao nani alilazimishia?

Ni jambo la kisikitisha Ben anakumbuka Ujamaa na Kujitegemea sasa hivi anapoona mambo akiwa nje ya uongozi.

Anachokiona sasa ndo alichokuwa akiaambiwa mara zote, na yeye akijibu kuwa Watanazania "wavivu wa kufikiri".

Hivi na viongozi wavivu wa kuwasikiliza wananchi wao tuwafanyeje?

Yanayotokea sasa hata nchini kwetu Tanzania , muasisi wake ni Ben William Mkapa. Hatushangai sana kwa yanayotokea ingawaje yanatusikitisha.

Kama maisha yangelitupa wasaa wa kurudisha nyuma wakati, naamini kabisa Mkapa angelifanya hivyo. Amepoteza yote!! Heshima yake na yale aliyoyaamini yamekwenda na maji.Alipokuwa madarakani alisahau haya leo hii anagundua alifanya makosa. Kwa bahati mbaya anaona aibu kusema I am sorry.I was wrong on these.
Afadhali Lole umesema maana bado majuto mjukuu. Mwinyi amelikumbuka azimio la Arusha. Mkapa anakumbuka kuwa maendeleo ya kweli hayatatoka kama msaada nchi za Ulaya na magharibi wala wawekezaji uchwara wanaowaleta. JK sijui atasema nini maana kweli naye anaweza kawa na mengi yatakayomsuta nafsi siku akikaa pembeni na kuangalia yanayoendelea.
 
Hilo la uwezekaji Mkapa alishakiri alifanya makosa na akasema if he could turn the clock back angehakikisha anawawezesha watanzania kuwekeza.
Lakini kuna kiongozi yoyote mstahafu wa afrika ambaye haimbi huo wimbo? kuanzia Jerry Rawlings, Abasanjo.....
 
Bulesi,
Mkuu wangu Mkapa sii mcheza mpira wala uchumi hauna ushindani zaidi ya wewe mwenyewe kujiweka ktk hali mbaya. Ni sawa na mchawi kumkumbuka Mungu wakati unakata roho...
 
This is the reason why am saying, despite the rumours that Mkapa had his own dirty deallings, I respect BEN MKAPA.
I urge bwana JK to invite Ben Mkapa in his close advisory ring. That way we, (Tanzanians) will survive the next 5yrs bwana JK is rumoured to rule after this year's general election

aje amu advise kitu gani? kuhusu wizi ili naye Kikwete afanye wizi? Watu wengine bwana! Huyu jamaa ni mwizi na hakuna chochote alichofanikisha kwa kuwepo madarakani miaka 10 isipokuwa kujitajirisha yeye na familia yake na jamaa zake wa karibu. Wacha kutukuza uchafu wa huyu Mkapa.
 
Back
Top Bottom