Mkapa arusha kombora; Awashutumu viongozi wa dini, Serikali

Siku hizi watu hawaambiliki na chimbuko kubwa la matatizo ni ujuaji mwingi, kila mtu anaamini kuwa anajua, na hili jambo ni la hatari.

“Wengine hawakuwapo wakati nchi hii inapata uhuru na hata wakati uhuru unapiganiwa, wao waliikuta nchi ikiwa huru.

“Lakini utakuta wanasimulia mambo mengi ambayo hata hawayajui na hayana msingi wowote,” alisema Mkapa.

Pamoja na wengi kuona kuwa Mzee Makapa ameanza kuchoka kifikra, kauli hii hapa juu ni ya kweli na ndiyo sababu kubwa ya kukwamisha maendeleo ya nchi ambayo pia inatoa fursa kwa wachache kutumia mwanya huo kujinufaisha, tukubali tusikubali bila kubadiliaka maendeleo ni safari ambayo bado ni ndefu sana kwa Tanzania.

Ujuaji wa kila mtu ni muhimu sana ktk kuleta maendeleo. Ujuaji unasaidia kuidhibiti serikali na kuifanya iwajibike. Mataifa yaliyoendelea yameendelea kutokana na ujuaji wa watu wao. Watawala ovyo hukerwa na ujuaji wa wananchi, hufurahia umbumbu wa watawaliwa. Hekima ya watawala wetu huonekana tu wakiwa watawala. Leo hii unafundisha shule ya msingi na hakuna anayekusikiliza, lakini kesho mumeo akiwa rais ghafla unakuwa mwenye hekima na uchaguzi ukija, wapita bila kupingwa! Mumeo aking'atuka utazirudia akili zako asilia, na usilalamike jamii haikujali. Kujua kuwa juu ya mlima Kilimanjaro kuna barafu sio lazima mpaka ufike juu ya mlima, watwambia hatukuwepo uhuru ulipokuwa unapatikana!
 
hivi hawa kama wameshindwa si wajitoe tu wajipange kwa uchaguzi wa 202
 
Back
Top Bottom