Mkapa Adai heshima kwa Viongozi wastaafu.

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,244
Rais mstaafu BW Mkapa ametoa kilio chake cha kutaka heshima katika ibada aliyoalikwa mkoani DODOMA.

Akiyasema hayo aligusia ni jinsi gani viongozi wastaafu wasivyopewa heshima stahiki mbele ya jamii.

Wanajamvi hivi ni kweli tumewatupa viongozi wetu wa kitaifa?

Je kwa sasa wanapotumia mafao kutoka kwenye kodi zetu wanafanya au wanashauri taifa vizuri?
Na ni kweli wanatumika kwa chama kimoja yaani ccm kubomoa vyama vingine?

Au kwa kuwa baadhi yao wamechafuka kwa tuhuma za UFISADI ndiyo kunakopelekea wananchi kutowapa heshima?

Je wewe unaonaje hili jambo?
 
daifu na serikali yake imezidi kuwadharau, Mkapa kasema kweli.
 
Anataka aheshimiwe kiaje? Kama hadi leo analindwa na anatembea na msafara? Haiingii akilini au anataka tumlambe miguu huku tumepiga uzi wa kijani na njano? Huyu anazeeka vibaya.
 
Nianavyo mimi Rais mstaafu aukandia msimamo wa CCM baada ya kuwaengua marais wastaaf kwenye maamuzi mazito ya kichama kwa kisingizio cha kuwaundia baraza lao (marais wastaafu) ambalo halina nguvu zaidi ya kutoa uhauri tu. Ushauri huo unaweza kuchukuliwa au kupuuzwa. Hawana chao tena pa kusemea mawazo na misimamo yao. CCM kalale pema peponi kamanda kwa kujiua mwenyewe.
 
Rais mstaafu BW Mkapa ametoa kilio chake cha kutaka heshima katika ibada aliyoalikwa mkoani DODOMA.
Akiyasema hayo aligusia ni jinsi gani viongozi wastaafu wasivyopewa heshima stahiki mbele ya jamii.
Wanajamvi hivi ni kweli tumewatupa viongozi wetu wa kitaifa?
Je kwa sasa wanapotumia mafao kutoka kwenye kodi zetu wanafanya au wanashauri taifa vizuri?
Na ni kweli wanatumika kwa chama kimoja yaani ccm kubomoa vyama vingine?
Au kwa kuwa baadhi yao wamechafuka kwa tuhuma za UFISADI ndiyo kunakopelekea wananchi kutowapa heshima?
Je wewe unaonaje hili jambo?

Nashindwa kuelewa ikiwa kama wewe mwenyewe hukujiheshimu, vipi watu wakuheshimu leo? Angalia vidokezo vichache kama hivi,

1. Kashfa ya EPA
2. Radar
3. Kiwila - (Tanpower)
4. Kesi ya Mahalu - Italy
5. etc

Sasa heshima itatoka wapi?? Hembu watanzania tuache umbumbumbu, let call spade a spade.
 
Rais mstaafu BW Mkapa ametoa kilio chake cha kutaka heshima katika ibada aliyoalikwa mkoani DODOMA.
Akiyasema hayo aligusia ni jinsi gani viongozi wastaafu wasivyopewa heshima stahiki mbele ya jamii.
Wanajamvi hivi ni kweli tumewatupa viongozi wetu wa kitaifa?
Je kwa sasa wanapotumia mafao kutoka kwenye kodi zetu wanafanya au wanashauri taifa vizuri?
Na ni kweli wanatumika kwa chama kimoja yaani ccm kubomoa vyama vingine?
Au kwa kuwa baadhi yao wamechafuka kwa tuhuma za UFISADI ndiyo kunakopelekea wananchi kutowapa heshima?
Je wewe unaonaje hili jambo?

Mkapa aliliibia taifa. hatuwezi kusahau KIWILA etc. Tuna kumbukumbu. Akitaka heshima ya kweli, aachane kwenda majukwaani wakati wa kampeni kuwatukana watanzania walio kwenye vyama vya upinzani. AACHANE NE MWIGULU , LUSINDE, WANATUKANA NAYE ANATUKANA HALAFU ADAI HESHIMA.
 
Heshima huwa haitafutwi bali inakuja yenyewe.Ye mwenyewe kachafuka tangu akiwa rais na anaendelea kujichafua kwa kuenda kupigia magamba kampeni.Naamini hatarudia tena baada ya kujikuta yuko kwenye tope zito ambalo hatatoka mpaka kifo
 
nashindwa kuelewa ikiwa kama wewe mwenyewe hukujiheshimu, vipi watu wakuheshimu leo? Angalia vidokezo vichache kama hivi,

1. Kashfa ya epa
2. Radar
3. Kiwila - (tanpower)
4. Kesi ya mahalu - italy
5. Etc

sasa heshima itatoka wapi?? Hembu watanzania tuache umbumbumbu, let call spade a spade.

"anben"
 
Nianavyo mimi Rais mstaafu aukandia msimamo wa CCM baada ya kuwaengua marais wastaaf kwenye maamuzi mazito ya kichama kwa kisingizio cha kuwaundia baraza lao (marais wastaafu) ambalo halina nguvu zaidi ya kutoa uhauri tu. Ushauri huo unaweza kuchukuliwa au kupuuzwa. Hawana chao tena pa kusemea mawazo na misimamo yao. CCM kalale pema peponi kamanda kwa kujiua mwenyewe.
Hivi hilo baraza lao litakua na nguvu kweli hii inaweza ikawa sababu ya huyu bwana kununa
 
Muda wao ushapita bana au wanataka kutembelea Presidential JET bado?
Mkuu, ujuzi na busara haupiti utabaki pale pale, ona dhaifu anavyoendesha nchi, angelikuwa anaomba ushauri kwa mzee mkapa hakika angefanikiwa, ofcoz na Ben naemapungufu lakini si yote. mfano dhaifu kuteuwa watendaji kishikaji si ma jaji tu bali watendaji wote, kulindana hata kitu cha wazi hakuna anaechukuliwa hatua.
 
daifu na serikali yake imezidi kuwadharau, Mkapa kasema kweli.
Mkapa anajidharaulisha mwenyewe pale anaposimama majukwaa kupiga kampeni za ccm. Ajue kwamba kampeni ni vita na vita haina macho. Kwa nini Ben asijifunze kwa mzee ruksa? Kama kiongozi mstaafu anakosa heshima, kamwe hataheshimiwa.
 
Rais mstaafu BW Mkapa ametoa kilio chake cha kutaka heshima katika ibada aliyoalikwa mkoani DODOMA.
Akiyasema hayo aligusia ni jinsi gani viongozi wastaafu wasivyopewa heshima stahiki mbele ya jamii.
Wanajamvi hivi ni kweli tumewatupa viongozi wetu wa kitaifa?
Je kwa sasa wanapotumia mafao kutoka kwenye kodi zetu wanafanya au wanashauri taifa vizuri?
Na ni kweli wanatumika kwa chama kimoja yaani ccm kubomoa vyama vingine?
Au kwa kuwa baadhi yao wamechafuka kwa tuhuma za UFISADI ndiyo kunakopelekea wananchi kutowapa heshima?
Je wewe unaonaje hili jambo?

Hana lolote LAANA YA MWENYEZI MUNGU IWE JUU YAKE...
 
Mkapa kule Meru wakati wa kampeni ulituita vifaranga, pumbavu, jinga, kwa kuwa tunaikosoa serikali hata kama inafanya ndivyo sivyo, wewe ndo unapaswa uwape watanzania heshima.
 
One can speak such stuff only when he/she is in Dodoma and also in a church, those are the only places that can buy it!
Akiwa Arusha au Mwanza hahitaji kuhubiri hilo maana kabla hajaanza TAYARI watakuwa wameshamdharau na kumzomea! akumbuke ya Arumeru na amuulize Pinda!
 
Rais mstaafu BW Mkapa ametoa kilio chake cha kutaka heshima katika ibada aliyoalikwa mkoani DODOMA.
Akiyasema hayo aligusia ni jinsi gani viongozi wastaafu wasivyopewa heshima stahiki mbele ya jamii.
Wanajamvi hivi ni kweli tumewatupa viongozi wetu wa kitaifa?
Je kwa sasa wanapotumia mafao kutoka kwenye kodi zetu wanafanya au wanashauri taifa vizuri?
Na ni kweli wanatumika kwa chama kimoja yaani ccm kubomoa vyama vingine?
Au kwa kuwa baadhi yao wamechafuka kwa tuhuma za UFISADI ndiyo kunakopelekea wananchi kutowapa heshima?
Je wewe unaonaje hili jambo?

Wakati mwingine uzee ni ugonjwa maana wengi wetu tukikumbuka BAE systems na Rada, pesa za akaunti ya EPA, Mchumchuma, Meremeta, kesi za Dr Mahalu na Mramba, mikataba mibovu, mashimo makubwa ya migodi ambayo haikuwanufaisha wananchi; Mkapa atuache tumsahau ili naye aendelee kula pensheni yake kwa amani, kama heshima aliyopewa na wananchi ya kuwa raisi wa Tanzania kwa miaka 10 haitoshi anaichukulia kama ilikuwa haki yake! basi bwana maana mtu asiyeweza kushukuru punje ya karanga hata umpe gunia hawezi kushukuru.
 
Back
Top Bottom