Mkanganyiko Wa Siku Ya Pasaka!

Umeelezea tu maisha kwa Ujumla lakini naona Chadema wameona una mpiga vijembe Mbunge wao! Lakini Ndugu zangu wa Chadema hamtaki hata mtu aongee mambo yanayo endelea Iringa na maeneo mengine! Mbona nyie mnaisema Serikali kila siku,lakini mkiguswa na wakati mwingine mnajihisi tu mmgushwa basi inakuaa balaa mna anza matusi! Hivi mkija shika serikali tutaongea kweli! Nadhani hata JF mtaifunga na wanaharakati wengi watafanyiwa assasination! Maggid haja mlaumu mtu wala Kumtaja huyo Mbunge wa Chadema! Wafuasi wa Chadema acheni upimbi,acheni ushabiki mahaba!
Ndugu, pamoja na kuwa mi si mfuasi wa chama chochote, naomba nikuulize. Unapoandika kuwa "Chadema wame....." unamaanisha kuwa hawa wafuasi wa vyama kila wanachosema/tenda ndiyo misimamo ya vyama vyao? Au kwa mtazamo huo tuseme huyu ndugu aliyeleta hii mada nzuri hapa siyo yeye ila ni Chama chake (kama anacho)? Kwa nini hata kosa la mtu mmoja (na unaweza kuta hata siyo kiongozi wa ngazi yoyote ktk chama chake) linafanywa ngazi ya kushambulia vyama?? Halafu kama tunakuwa wakweli sijaona tusi lolote kwa waliompinga, labda kama matusi yatakuja baadaye! That aside, big up mleta mada. Hiyo picha umeiona mjini kuna balaa zaidi vijijini.
 
Nimejukuta mwenye huzuni baada ya kusoma hii habari, kwani inaelezea ni kwa jinsi gani maisha ya mtanzania wa kawaida yalivyokuwa magumu kwa sasa.

Mmmh tutafika kweli tuendapo?
 
Back
Top Bottom