Mkandarasi achota 3bn advance akimbia! Alipewa kujenga km 26 za lami wakati hana ujuzi wowote...

Nilijua tu ni Mhindi kafanya hivyo. Kashfa hizi: EPA, RICHMOND, RADAR, IPTL, ESCROW na zingine zilizozimwa zinahusu wahindi. Na bado tutaendelea kuwaamini na kuwapa tenda. Sijui viongozi wetu wanaweka vichwa vyao kwenye ma-deep frieezer halafu ndio wafanye maamuzi?

...mkuu' ni kwa sababu viongozi wetu karibia wote ni feki..., ukianza na mkubwa wao!
 
Uko sahihi, hivyo vitu vyote kama security bond na bank guarantee zote zipo kweny makaratasi na ndo maana walipokuwa wanataka kusitisha mkataba ikabidi waanze kufuatilia kujua na kutoa taarifa sehem husika ikiwepo hiyo insuarance. Lakin mwisho wa siku hivyo viti vyote vilikuwa vimefojiwa na watu walikaa kimyaa.

Tatizo ni kuwa hawakuomba authenticity ya submitted Advance Bank Guarantee kabla ya kulipa invoice ya advance payment. Kwa mradi wa 26Bilion ilikuwa ni lazima ku-request for authenticity kwa banker wake or Insurance Company kama waliruhusu insurance.
 
Nadhani mleta mada hajafanya utafiti wa kina kujua kama hizo hela zimeliwa au la,kuna mambo ambayo contactor before apewe tenda anatakiwa afanye na pia kabla hajapewa advance kuna insurance anatakiwa awe nazo,sasa inakuwaje vitu kama hivyo visilipe hilo deni?i think haujadunguka vya kutosha get some more meats urudi hapa

Mambo anayotakiwa kufanya contractor kabla ya advance payment ni pamoja na Bank Guarantee. Kama nimesoma vizuri mtoa mada amesema Guarantee iliyokuwa submitted ni feki.
Watu walijipanga kiwizi wizi tangu awali. Ni movie ambayo walijua mwisho wake.
 
Ujinga wa watanzania utatuponza sana. Sitashangaa mabilioni haya ya walipa kodi yakinyamaziwa na maccm

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums


Tunaelekea uchaguzi mkuu, miongoni mwa mbinu za kupata fedha ya kampeni ni hizo
 
hao wafanyakazi waliokwenda huko nchumbiji kuona hizo kazi na kuhakiki hizo document tutajiwe majina yao au waanze kuchunguzwa
 
magufuli ni mwizi wa nyumba za serikali,tangu lini jizi likawa jembe!mwakyembe ndio njaa tupu.
 
Hivi kwanini serikali isitumie Balozi za nchi husika ku certify kampuni inayotaka kufanya kazi na sisi kuepuka haya......hatukujifunza kwenye Richmond na mengine kibao? Au ndio kutengeneza loop holes za kupiga? Kama ubalozi wa UK hapa ungetumika vizuri walau kuna taarifa za msingi zingejulikana......

.......Kweli Tanzania ni nchi yenye kila kitu isipokuwa Watanzania....:A S 13:
 
Kwanza hata hiyo strada original unayodhani ipo haipo. Moja,Google strada international then utaipata hiyo kampuni jaribu kuhusianisha na kampuni kama kuna strada nyingine. Pili na hata kama ipo inakuaje unaenda kufanya uchunguzi wa kama aliesoma hiki chuo kweli ni huyu john juma makiti, unacomfirm ni yeye wakati aliesoma pale ni john juma mapunda. Kama lilifanyika kosa na namna hilo kwanin wasiadhibiwe kwa kuipa serikali hasara kwa uzembe.

Mkuu usitegemee hii serikali inayoongozwa na Chamacha Mapinduzi kumuadhibu mzembe hata siku moja!

Wangekuwa wanafanya hivyo matatizo ya aina hiiyangekuwa yamepungua. Chukulia madudu yaliyofanyika katika kubinafsishamashirika ya Reli na Ndege kwa mfano. Baada ya wawekezaji waliowekwa kuzidikuyadhoofisha haya mashirika na mikataba yao kuvunjwa na serikali hiyo hiyoiliyowapigia debe, nani kachukuliwa hatua zozote?!

Kwa hii nchi, kulindana hata katika maswala yanayosabibishia nchi hasara imekuwa ni jambo la kawaida kabisa!
 
Hivi kwanini serikali isitumie Balozi za nchi husika ku certify kampuni inayotaka kufanya kazi na sisi kuepuka haya......hatukujifunza kwenye Richmond na mengine kibao? Au ndio kutengeneza loop holes za kupiga? Kama ubalozi wa UK hapa ungetumika vizuri walau kuna taarifa za msingi zingejulikana......

.......Kweli Tanzania ni nchi yenye kila kitu isipokuwa Watanzania....:A S 13:
Mkuu kama hii issue ni kweli, kinachofanyika ni makusudi kwa kuwa taratibu za tender iwe ndani ya nchi au za kimataifa zinamlolongo mrefu ikiwa pamoja na kuwasilisha company profile na at least kazi mbili tatu ilizofanya plus vitu vingine kama bank statement na usajiri wake then serikali inafanya certification based na hizo information kabla ya kutoa tender, we si umeona UDA ipo hapa hapa nchini lakini kauli zinabaki sintofahamu wakati hata kwa simu tu unamaliza utata.
 
Bora hata angepewa Nyanza road hata akichakachua na kujenga chini ya kiwango lakini ni wa hapa hapa
 
Bora hata angepewa Nyanza road hata akichakachua na kujenga chini ya kiwango lakini ni wa hapa hapa

Kaka nyanza road wanajitahid sana, nenda kaangalie barabara alizojenga dodoma mjini, huwezi fananisha na za arusha mjini ambayo alifanya mchina. Project zote zilikuwa financed na world bank kupitia Tanzania strategic cities project.
 
Dah inasikitisha saana. Hao maofisa wa tan roads waloenda huko Msumbiji na Ghana wanastahili kunyofolewa korodani bila ganzi kisha wanyongwe pum.ba.vu kabisa.

Mkuu ndo nchi yetu hii watanzania na hapa ndipo tulipofikishwa. Punguza tu hasira ndugu yangu maana yake unaweza kukuta hao maofisa wa Tanroads ni wa ile jinsia nyingine kwa hiyo hawana hiyo makitu ya kunyofolewa!!!!
 
Ndugu wanaJF,

Waziri John Magufuli alipokuwa akisoma bajeti ya Wizara yake alisema contractor wa barabara ya kutoka KIA kwenda Mererani amefukuzwa kutokana na utendaji mbovu. Hakuendelea na detail yeyote ile kuhusu huo mradi, huenda hakutaka watu wajue zaidi au yeye mwenyewe hajui kilichotoekea.

Ukweli ni huu:
Kampuni iliyopewa kazi ya kujenga hiyo barabara inaitwa Strada International iliyoonyesha ina Makao Makuu yake UK. Ukubwa wa mradi ulikuwa ni km 26 za kiwango cha lami na gharama za mradi jumla ni 26bn.

Contractor alipewa advance payment ya takribani 3bn (am not sure ila ni kati ya 2.5 mpaka 3.2). Baada ya kupewa hiyo pesa contractor huyu ambae asili yake ni singa singa hakufanya chochote toka mwezi wa 5 mwaka jana mpaka mwezi wa kwanza mwaka huu. Zaidi alisafisha barabara mita 600 tu ambayo ni hatua ya mwanzo kabisa. Hata kujenga camp yake alishindwa, na mbaya zaidi hakuwa na vifaa vya kufanyia kazi. Alinunua grade 2 za kichina na hela hakumalizia kulipa. Mradi ulitakiwa kuwa na zaidi ya tipper 25 lakini alikuwa na tipa 2 za kukodi. Pamoja na kampuni ya usimamizi ya LEA kutoa vielelezo toka mwezi wa 10 kwamba Contractor hana uwezo wa kufanya kazi, aliendelea kulelewa mpaka mwezi January alipokimbia.

UFAKE WA KAMPUNI HII
Inashangaza kuona kampuni ya kigeni ambayo ni ya kisanii imepewa tenda ya kujenga km 26 za rami ambazo ni sh 26bn wakati kampuni hii haijawahi kujenga hata mita 5 za changarawe. Hii kampuni haijawah kufanya mradi wowote wa barabara, lakini walisubmit Company Profile iliyoomyesha wamejenga barabara Sudan, Ghana, Msumbiji, Ethiopia, Qatar, UK na Namibia. Kabla ya kupewa huu mradi kwa kuwa ni kampuni mpya tanroads huwa na utaratibu wa kujiridhisha kwa kupeleka wajumbe baadhi ya nchi kwwnda kuona miradi iliyofanywa na hiyo kampuni. TANROADS ilituma wajumbe ghana na msumbiji, na wajumbu hao walirud na report ya kuonyesha kwamba ni kweli walifanya na mbaya zaidi walirudi mpaka na ripoti za idara na mamlaka za barabara ktk nchi husika kwamba hiyo kampuni ilifanya kazi huko (Kitu ambacho si kweli, wajumbe walihongwa na kuchakachua report zote za Msumbiji na Ghana kwamba kampuni ilifanya kazi huko na kukamilika).

HASARA KWA SERIKALI

Serikali imepata hasara kubwa katika maeneo makuu matatu:

1. Adnvace pyament ya 3bn. Serikali imeambulia grader 2 za kichina zisizo na thamani ya zaid ya milioni 200.

2. Gharama za kumlipa mhandisi msimamizi kwa zaidi ya miezi sita aliyokaa. Ambapo ni zaidi ya million 700.

3. Kuandaa tender upya ambapo gharama za mradi lazima zipande kutokana na kupanda kwa maisha. Maana 26bn ni tender iliyotangazwa mwaka 2012.

NINI KILITOKEA MPAKA STRADA IKAKIMBIA

Katika hali ya kusuasua alikokuonyesha, serikali ilianza kuichunguza hii kampuni kwa undani zaidi maana hata wale waliokuwa wamekula hela kwa kuipa kazi hii kampuni ilionekana wanashindwa kuibeba. Serikali ikagundua kumbe hata bank guarantee iliyowekwa ni feki! Hiyo bank ilikana kuijua hiyo kampuni hii na hapo ndipo serikali ilipochanganyikiwa maana mdhamini aliyewekwa ili kama mambo yakiwa sivyo yeye ndo alipe fidia haijui hiyo kampuni. Watu hao hao wa TANROADS waliokula dili hilo wakamshtua mteja wao kwamba serikali imeshtukia mchezo na jamaa akakimbia mpaka leo.

Kuonyesha kampuni ilikua ni ya kitapeli, ilikopa mpaka furniture za ofisi. Vitendea kazi kama computers na printers walikopa duka la Compcat hapo Arusha. Ana deni kubwa la milion ka 200 hivi kutoka kwa NSK. Wafanyakaz wanadai mishahara ya mwezi wa kumi na mbili ma wa kwanza na hapo ni baada ya kugoma kwa wiki nzima na kumtumia mkuu wa Wilaya na mbunge mh Lema kumpigia simu ndipo alilipa deni la mwezi wa 10 na 11.

EXIM WANUSIRIKA

Bank ya Exim ilibakia kidogo tu nayo itapeliwe baada ya hiyo kampuni ku-process mkopo wa milion 450. Katika hali iliyoonyesha bahati kwa Exim, walichunguza kabla ya kutoa hizo hela maana walikuwa tayari wameshajiridhisha kwa asset zilizowekwa ambazo miongoni mwao ndo zile grader ambazo sasa serikali imezizuia kupitia TANROADS Arusha.

KAULI SAHIHI

Ukweli ni kwamba mkandarasi Strada alikimbia mwenyewe na si serikali kumfukuza. Na amekimbia baada ya kuona ukweli kuhusu kampuni yake kufoji vitu umejulikana. Lakini wameondoka na faida kubwa na kuitia hasara serikali. Maana ktk 3bn, alizotumia Bongo hazifiki hata 1.5bn mpaka anaondoka.

NANI WA KUWAJIBISHWA

Kitengo cha Procurement cha TANROADS lazima kiwajibike kwa hili maana walifanya Investigation kwa hii kampuni na kutoa report za uwongo. Maana huwezi kuniambia walivyoenda Ghana na Msumbiji walidanganywa na hizo mamlaka kuhusu kampuni hii. Na pia bank guarantee walishindwa ku-confirm kabla. Hili swala lilifanyika wakiwa wanajua dhahili ukweli kuhusu kampuni hii.

Na ningependa kuona Magufuli akilitolea ufafanuzi swala hili na hatua zilizochukuliwa kwa watendaji waliosaidia kuidanganya serikali. Na pia mbunge husika, Olesendeka na ningependa ajue kuhusu hili maana barabara ipo jimboni mwake.

Nawakilisha.

Yasioyowezekana nchi yoyote ile, Tanzania yanawezekana. Na bado mengi yatatokea hadi hapo Wananchi watakapoamua kama Malawi walivyoamua!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom