Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,735
Hatimaye Serikali ya CCM imeamua kutumia wanasheria wa Serikali kushughulikia vijana wa CHADEMA wanaofanya mafunzo ya uzalendo na ukakamavu Kwa kutumia Sheria ya kikoloni iitwayo The Public Order Act ya Mwaka 1951 kuanzia leo.
Hatua ya kwanza ya kuhakikisha Red Brigade ya CHADEMA inashughulikiwa kisha kuwapatia mwanya vijana wa CCM kupitia Green Guard wafanye wanavyotaka, inaanzia rasmi leo mkoani Simiyu ambako vijana takriban 13 wa CHADEMA wanafikishwa mahakamani leo eti kushtakiwa kwa kosa la kufanya kazi au majukumu yanayofanana na polisi baada ya kukutwa uwanjani wakifanya mazoezi ya ukakamavu.
Hatua hiyo inafuatia maelekezo ya kikao kilichofanyika mkoani Morogoro ambapo maofisa wa serikali walipewa maagizo maalum ya kuhakikisha Red Brigade haiendelei na ifikapo wakati wa uchaguzi iwe 'imekufa' ili kutoa mwanya kwa CCM kupitia Green Guard kufanya wanavyotaka kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kama ilivyo ada, wakishirikiana na baadhi ya watumishi kwenye Vyombo vya dola.
Katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokutana Zanzibar hivi karibuni suala la mafunzo ya uzalendo na ukakamavu Kwa vijana wa CHADEMA liliibua mjadala ambapo walikubaliana kuwa wakiiacha Red Brigade ikaendelea kuimarika CCM itakuwa kwenye wakati mgumu wa kufanya hujuma wakati wa uchaguzi. Kwa hiyo ikakubaliwa lazima kuwepo mikakati ya kuizuia.
Mkakati wa kwanza ulikuwa ni kutumia ziara za akina Nape na Kinana mikoani kusema maneno majukwaani kuwa Red Brigade eti ni ugaidi na uhaini. Ndiyo maneno aliyoyasema Nape akiwa mkoani Dodoma, Kongwa.
Maneno hayo yalikuwa ni code words kwa ajili ya Vyombo vya dola kuchukia hatua lakini bahati mbaya baadhi ya watu serikalini na katika Vyombo hivyo ambao ni wapenda haki walihoji na kusema iwapo CCM inataka Red Brigade isiwe
wakaenda mbali na kuwaambia CCM kuwa Green Guard ndiyo imekuwa kikundi kinachotishia amani na kusababisha vurugu, utekaji nyara, mateso na mauaji wakati wa uchaguzi na kufanya hujuma zingine mbalimbali hata kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kuiba kura.
Baada ya mkakati huo wa kutumia code words za ugaidi na uhaini kwenye mikutano ya hadhara ili eti vyombo vya dola vichukue hatua za makosa ya ugaidi na uhaini kushindikana, ndiyo sasa imetafutwa njia nyingine...
Maofisa kadhaa wa Serikali wakaitwa Morogoro kwa ajili ya jambo moja tu; Red Brigade ambako ndiyo ikakubaliwa kuwa Sheria ya The Public Order Act itumike 'kuwashughulikia' vijana wa CHADEMA ili kuwatisha wasiendelee na Red Brigade.
Baada ya hapo ndiyo vijana wa CHADEMA wakakamatwa huko Bariadi wakiwa katika mafunzo ya uzalendo ambapo walipofikishwa kituoni walipewa kesi ya tuhuma za Unlawful Assembly...kisha wakapewa dhamana na kuondoka kituoni hapo.
Lakini punde tu baada ya vijana hao kutoka kituoni hapo, wakakamatwa tena na kuwekwa ndani kwa kosa lingine.
Leo ndiyo wanafikishwa Mahakamani wakishtakiwa kufanya kazi zinazofanana na majukumu ya polisi.
Huu sasa ndiyo umeamriwa uwe mkakati wa kuzuia Red Brigade utakaotumika kuhakikisha haiendelei nchi nzima baada ya CCM kuona wazi kuwa haitapata mwanya wa kufanya hujuma dhidi ya CHADEMA, viongozi wake na mali za chama hicho kama ambavyo imekuwa ikifanyika Kwenye kila uchaguzi.
Wakati kesi hiyo ikianza leo, hakuna kesi hata moja ambayo inaendelea mahakama yoyote ya Tanzania kuhusu vitendo vya kihalifu vya kikosi cha ulinzi cha CCM, Green Guard, ambapo ushahidi upo wazi namna ambavyo wamekuwa wakipewa mafunzo Kwenye makambi ya siri, huku pia wakifanya shows za kijeshi mchana hadharani na Mkuu wa Nchi akipita akikagua magwaride yao.
Imetolewa na mkuu wa habari Chadema
Tumaini Makene