Elections 2010 Mkakati wa kuilinda kura yako isichakachuliwe huu hapa

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
MKAKATI WA KUILINDA KURA YAKO ISICHAKACHULIWE HUU HAPA


Hivi kuna faida gani kuacha shughuli zako na kwenda kupiga kura na siku inayofuata unasimuliwa ya kuwa mambo yamekwenda visivyo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Kumbe huku nyuma yale masaa ya jioni ambayo uko kwenye mapumziko ukitegemea mfumo huu wa kidhalimu ufanye kazi ya kutenda haki wenzio uliowaamini wanaoitwa mawakala wa vyama mbalimbali wanapanga matokeo na kuyasaini tu bila hata ya kuzihesabu kura zetu!!!!!!!!! Aiseee huu kweli ni uungwana?

Jasho letu safari hii tusikubali likageuzwa kipato cha wajanja wachache.

Safari hii, dhuluma hii tupambane nayo kwa kuhakikisha siku ya tarehe 31st Oktoba hatuna shughuli nyingine ila kurudi masaa ya jioni kuhakikisha haki inatendeka na inaonekana ikitendeka.

Saikolojia imeonyesha huko Kenya ya kuwa wadhulumaji hubeba mikoba iliyorindima fedha usiku usiku ili kuyachakachua matokeo. Tukiwepo kwenye vituo vya kupiga kura hadi “kieleweke” hapo matokeo yatakapotangazwa mikoba hiyo iliyofurika balaa kwa mpigakura wataipitishia wapi na mgawo watajadiliana saa ngapi maana wewe mpiga kura utakuwa pale ukimulika nyendo zote.



TULINDE KURA ZETU KAMA KUPIGA KURA KUNA TIJA ENDAPO HUWEZI KUIILINDA BASI USIPIGE HIYO KURAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
naomba usiishie kwenye hii forum, panua uwigo ujumbe wako utoke kwenye magazeti kila siku, mda ni mchache lakini bado nafasi ipo ya kufikisha ujumbe kwa watanzania wengi
This time for Tanzania,
Tsamina mina zangalewa
Cause this is time for change

Tsamina mina eh eh
Waka waka eh eh
Tsamina mina zangalewa
This time for change
 
Ninajipanga tatizo ni vyombo vyetu vinaminya "anti-establishment news"

Hata hivyo ninakushukuru
 
Back
Top Bottom