Mkakati Mzito waandaliwa na CCM kumchonganisha LIPUMBA

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Mkakati mzito umesukwa na CCM wa kumchonganisha Prof Lipumba na waislam. Kwa mujibu habari zilizonifikia mpango huo una lengo la kusambaratisha UKAWA wasisimamishe mgombea mmoja nafasi ya urais. Mtoa habari anasema kuwa CCM wameiona hatari ya muungano wa CUF na CHADEMA. Wanasema ni hatari hasa watakapofanikisha lengo la kumtosa Lowasa rasmi. Mtoa habari anasema kunakanda zimekusanywa za kuonyesha unafiki wa Lipumba kwa Waislam.Naambiwa mkakati huo unaandaliwa na wanaojiita Mashekh kutoka Morogoro wakiongozwa na mhariri gazeti moja linalondika habari za waislam likijifanya ni la waislamu
 
Watanzania wana miliki viwanda vya kutengeneza uongo-JK
 
UKAWA fanyieni kazi taarifa hii...inaweza kuwa na ukweli

cc Tumaini Makene
Sasa hivi wakuu hakuna taarifa ya kudharu, ila kujua mbinu za adui yako ni nusu ya kumumaliza. Mwaka huu CCM imeshikwa pabaya kwa vyovyote lazima yatimie kwa kuondoka madarakani.
 
Last edited by a moderator:
UKAWA fanyieni kazi taarifa hii...inaweza kuwa na ukweli

cc Tumaini Makene

Freeland ni ile video ya msikiti wa .....akihutubia mwaka juzi shekh basalehe alikua ndani ni ile aliyokua anasema Jk kawaangusha waislamu ingawa cuf ilimsaidia kushinda uchaguzi.Akasema wenzao wamejiandaa wao ( waislamu? je ? ingawa hakusema kuwa ni watu wa mlengo upi?
 
Kama ni hiyo haina impact........
 
Ukawa muwe makini na watu kama mleta mada. Anasema CCM wanasema ukawa no hatari hasa kama wakifanikiwa lengo lao la kumtosa Lowassa, anataka kuwaaminisha CCM kuwa Lowassa ndiyo kiboko ya Ukawa hivyo asitoswe. Hapa lengo siyo kuitahadharisha Ukawa bali kumpigia debe Lowassa ili CCM wasimtose.
 
Ccm imeishiwa sera zile kampeni za maji na Barabara zimepitwa na wakati. Sasa wameingia hadi makanisani wanatutaka nini hawa!
 
Maintarahamwe sasa yameingia kiwewe cha UKAWA, yanahangaika huku na kule bila ya kujua wafanye nini. Mwaka huu lazima muisome namba na ujinga wenu dhidi ya UKAWA kamwe hautafanikiwa.
 
Tatizo la CCM wana mikakati mingi sana, mara kumtosa Lowassa, mara kumzuia Mwighulu Nchemba aache kutangaza nia, mara kumtetea waziri Muhongo muongo asivue uwaziri, sasa hivi wamekuja na wa Lipumba tena!!??, sasa sijui ni mkakati upi watakaofanikiwa, kimsingi ni kwamba wameshapoteza dira wakubali tu matokeo...
 
Mkakati mzito umesukwa na CCM wa kumchonganisha Prof Lipumba na waislam. Kwa mujibu habari zilizonifikia mpango huo una lengo la kusambaratisha UKAWA wasisimamishe mgombea mmoja nafasi ya urais. Mtoa habari anasema kuwa CCM wameiona hatari ya muungano wa CUF na CHADEMA. Wanasema ni hatari hasa watakapofanikisha lengo la kumtosa Lowasa rasmi. Mtoa habari anasema kunakanda zimekusanywa za kuonyesha unafiki wa Lipumba kwa Waislam.Naambiwa mkakati huo unaandaliwa na wanaojiita Mashekh kutoka Morogoro wakiongozwa na mhariri gazeti moja linalondika habari za waislam likijifanya ni la waislamu

tutayAsikia mengi sana kuelekea octoba.
 
Back
Top Bottom