Mji wa Rajasthan nchini India wavunja rekodi ya juu ya kiwango cha joto

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
160520111823_india_hot_640x360_epa_nocredit.jpg

Mji mmoja katika jimbo la Rajasthan nchini India umevunja rekodi baada ya kusajili vipimo vya juu vya joto vya hadi 51 C,ikiwa ni vya juu tangu kuanzishwa kwa rekodi za viwango hivyo ,kulingana na ofisi ya hali ya hewa.

Rekodi hiyo mpya katika eneo la Phalodi katika jimbo hilo la jangwa inajiri wakati ambapo kuna wimbi la mvuke joto kali nchini India.

Rekodi ya awali ya vipimo vya juu vya joto ilikuwa 50.6C mnamo mwaka 1956.

Wimbi hilo la Joto hilo limekumba eneo kubwa la India Kaskazini ambapo joto limepita vipimo vya 40C kwa wiki kadhaa sasa.

Wakati wa msimu wa upepo nchini India huwa na jua kali na kupanda kwa vipimo vya joto ,lakini viwango vya joto vinavyopanda hadi 50C sio vya kawaida.

Murari Lal Thanvi,shahidi mmoja huko Phalodi amiambia BBC ,kwamba alijaribu kukaa nje siku ya Ijumaa.

140607124553_india_heat_wave_640x360_ap.jpg

''Hata simu yangu ilisalimu amri na kuwacha kufanya kazi nilipokuwa nikipiga picha'',alisema.

Nilifanikiwa kuiwasha simu yangu baada ya kuiweka kitambaa chenye maji kwa takriban dakika 20-25

Chanzo: BBC Swahili

Wakuu kwa joto hili sijui niseme tumemkosea nini mungu, au ndo tunahitaji kutubu?
 
Inamaana ukimchukia mrajasthan mmoja ukamleta hapa dar atalalamika baridi!!
aisee wanaipata, maana hii dar yenyewe tu balaa.afu ni nusu ya hii.
 
Hasa kipindi hiki cha kibaridi maana mimi mwenyewe usiku wakati mwingine pangaboi linanishnda
 
Matokeo ya kuharibu mazingira. India ni mzalishaji mkuu wa air pollutants na madhara yake yanafika hadi Afrika. Maendeleo yana gharama zake.
 
India kipindi hiki huwa na joto kali na mvua hatari.Nakumbuka niliwahi kuteseka sana na hali ya hewa
 
Unaweza kuthibitisha uhusika wa Mungu kwenye hilo ongezeko la joto?
 
160520111823_india_hot_640x360_epa_nocredit.jpg

Mji mmoja katika jimbo la Rajasthan nchini India umevunja rekodi baada ya kusajili vipimo vya juu vya joto vya hadi 51 C,ikiwa ni vya juu tangu kuanzishwa kwa rekodi za viwango hivyo ,kulingana na ofisi ya hali ya hewa.

Rekodi hiyo mpya katika eneo la Phalodi katika jimbo hilo la jangwa inajiri wakati ambapo kuna wimbi la mvuke joto kali nchini India.

Rekodi ya awali ya vipimo vya juu vya joto ilikuwa 50.6C mnamo mwaka 1956.

Wimbi hilo la Joto hilo limekumba eneo kubwa la India Kaskazini ambapo joto limepita vipimo vya 40C kwa wiki kadhaa sasa.

Wakati wa msimu wa upepo nchini India huwa na jua kali na kupanda kwa vipimo vya joto ,lakini viwango vya joto vinavyopanda hadi 50C sio vya kawaida.

Murari Lal Thanvi,shahidi mmoja huko Phalodi amiambia BBC ,kwamba alijaribu kukaa nje siku ya Ijumaa.

140607124553_india_heat_wave_640x360_ap.jpg

''Hata simu yangu ilisalimu amri na kuwacha kufanya kazi nilipokuwa nikipiga picha'',alisema.

Nilifanikiwa kuiwasha simu yangu baada ya kuiweka kitambaa chenye maji kwa takriban dakika 20-25

Chanzo: BBC Swahili

Wakuu kwa joto hili sijui niseme tumemkosea nini mungu, au ndo tunahitaji kutubu?
Ni mabadiliko ya hali ya hewa broo.siku zijaazo dunia itakumbwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.
 
India wategemee majanga makubwa zaidi ya hayo ila nasisi huku kwetu afrika kama hatuta chukua tahadhari za kutunza mazingira mapema basi nasisi lazima tutegemee mengi yatatukuta kama yaliyo wakuta wenzetu wa india.
 
Back
Top Bottom