Mjadala: Ni jambo gani kwenye Maisha yako lilichelewa sana? Ila sasa unaona kawaida sana

Nilitamani sana kusafiri nje ya mkoa niliokulia, Ipo siku nilimwambia B mkubwa kuwa natamani kusafiri nje ya mkoa huo, akaniambia "mwanangu ukiwa mkubwa na hela zako, usafiri popote utakapo, subiri uwe mkubwa Mungu akusaidie upate hela" kauli hii ilinipa hali na matumain makubwa mno, anyway nimeshakuwa mkubwa na sio nje ya mkoa ule tu, mpaka nje ya mipaka ya nchi nishatoa.

Sijawahi kutamani Nyumba, gari wala familia, lkn namshukuru Mungu sana hapo sina gari tu.

Mungu ni mwema.
 
Brilliant!!
 
Wakuu,

Kwenye haya maisha tuna mambo mengi sana ambayo ni matamanio, na kila mtu nafikiri wanayo. Sasa ni vitu gani ambavyo ulivitamani sana kuwa navyo, yaani ile tu unajiambia I wish, I wish...

Ila sasa unavyo au unavifanya na unaona ni kawaida kabisa yani!! Kuna watu walitamani kuwa na nyumba zao, sasa wanazo so wanaona ni kawaida tu, Wengine magari sasa wanayo so inaonekana kawaida tu...

Wengine kuwa na familia n.k Wengine hata elimu tu, kuna wale waliokuwa wanatamani kuwa na degree, masters au hata PHD sasa wanazo na ishakuwa kawaida tu!

Kila ambition mi naona kama inawezekana kwenye maisha ni kutia nia tu,

Kila unachokiona/kitamani kuwa nacho inawezekana kabisa.

Sasa kuna baadhi ya vitu vinachelewa, ila vinakuja tu!

Je, ni kitu gani mdau ulitamani kuwa nacho au kukifanya na sasa imewezekana na unaona kawaida?

Binafsi, nilichelewa sana kusafiri kwa kutumia ndege!!

Kwa sasa nasafiri na ndege maeneo mbalimbali Duniani kuliko hata ninavyosafiri na gari.

Sasa imekuwa kawaida sana .

Twende kazi.....
M naona nilichelewa sana kuwa na mama hadi saa ivi sina mama yangu but yupo hai anaishi
 
Mimi nilichelewa sana kufika Mjini kutoka kijijini katika mkoa niliozaliwa.

Watoto wengi ambao nilikuwa nawazidi umri waliweza kufika mjini kutembea, mimi nikiachwa kupigika kijijini.

Ila Shule ishukuriwe, nilipofaulu kwenda form one nikalaba Jack port ya kupangwa Boarding school iliyopo mkoa mwingine tena jiji kabisa. Hapo ndoto za kukanyaga mjini ambazo zilikuwa zinaniumiza kichwa kila mara zikaenda kutimia. Si hivyo nikaweza kuvuka mipaka ya mkoa wangu kuwashinda wale waliokuwa wananiringishia wao kufika mjini kabla yangu.

Kwa sasa imekuwa kawaida.

Ndoto zilizopo kwa sasa ni nyingi sana ikiwemo hiyo ya kukwea Mwewe hata kwa Local route tu.
Itakuwa tu mkuu.

Nakumbuka nilikuwa naenda kupokea wageni pale KIA, naishia kuiona KLM au Ethiopian na Qatar Airways! by that time najisemea tu, Nitakwea na mimi.

Sasa hivi naona kawaida sana.
 
Back
Top Bottom