Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Akitaka kuondoa shilingi, Mhe.Msnyika anashauli kufumua bajeti ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa kile anachodai kuwa bajeti hiyo imetenga fedha nyingi kwenye mafunzo na posho badala ya kwenda kwa wakulima.
Mhe. Halima Mdee na Machali wanasema ni aibu kwa kilimo kukua kwa asilimi 4 wakati kuna fedha nyingi zinatengwa kwenye utafunaji.
Sina hakika kama wabunge wa Upinzani wanajua wanachochangia. Mhe. Waziri wa Kilimo anaummuliza Mhe. Machali kama anajua "Systems of Rice Intensification" (teknolojia ya kilimo shadidi cha mpunga).
Ni wazi kuwa hakuna mtu yeyote anayezaliwa anajua chochote. Pia kila anayejua jambo flani huwa si kweli kuwa anajua mabo yote. Hata huyo anayefikiri yeye ndiye anyejua vizuri kilimo sidhani kama anajua kama nguruwe anazaa mara ngapi kwa mwaka!
So kuuliza swali kama hilo, kwa mtu mwelewa ni kutangaza ujinga wako hadharani kwamba wewe unaua kila kitu, wakati hata mjinga anajua kuwa hata mwenye akili hajui kila kitu!
Kwa upande mwingine, ni kweli kuwa bajeti inakuwa ya kipumbavu, kama fedha zinazoelekezwa kwenye semina na posho ni nyingi kuliko zinazoenda kwenye mambo mengine kama pembejeo na huduma za wakulima. Kwa kifupi nakusudia kusema kuwa ni bajeti za aina hii ndiyo zilizofikisha kilimo hapa kilipo. Binafsi nimefanya uchunguzi na naweza kusema tena bila hata kupepesa, kuwa mabwana shamba wanaowasaidia wakulima ni wachache sana. Katika mia labda mmoja au usipate kabisa. na pia utashangaa kuwa hata hapa mjini kuna mabwana shamba na mabibi shamba wakati kila mtu anajua mjini hakuna mashamba!
Kwa hali ilivyo sasa, kama nchi ingekuwa na viongozi wenye akili na makini ( namaanisha walioko sasa ni dhaifu, mafisadi, wapumbavu na wezi), Wizara ya kilimo ingeshafutwa kabisa kwani hakuna inachosaidia zaidi ya kutia hasara nchi. Hali kadhalika fedha zote zinazoenda kwenye wizara hiyo zingetafutiwa sehemu nyingine ya kwenda kama afya au elimu hii ikiwa ni baada ya kuondoa mawaziri hawa wa sasa ambao hata mbuzi wangu amewazidi akili, hekima na busara.(Mtanisamehe...inaniuma sana)
Kwa mtindo huo, kama bajeti hii siyo ya kijinga ni bajeti ya aina gani?