Mizengo Pinda: Ni sawa kwa wakuu wa wilaya kuinadi CCM mikutanoni!

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Ni siku chache tokea wakuu wa wilaya walipokula kiapo cha uaminifu wa kuwatumia wananchi wote pasipokujali itikadi za wananchi husika. Cha kushangaza, leo hii Waziri mkuu, mhe.Mizengo Pinda a.k.a mtoto wa mkulima (asiye na shamba) amesema ni sahihi kwa wakuu wa wilaya kuinadi ccm (kama makatibu wenezi) wanapokuwa wilayani haswa katika mikutano ya hadhara.

Alipokuwa anajibu swali la Mb.Ezekiel Wenje kuhusu uhalali wa wakuu wa wilaya kukinadi chama wakati wanatumia kodi za watanzania wote kupitia mishahara,usafiri na posho wanazopewa Wakuu hao. Kwa mtazamo wa mtendaji mkuu wa serikali Mhe.Pinda aliyedai ni sawa kunadi chama na kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachokimbiwa na wanachama kila kukicha.

Baadhi ya wananchi niliowahoji mjini Mbeya...wamesema hawana imani na wakuu wa wilaya wakiwa kama Wakuu wa ulinzi na usalama wilayani kwani hawawezi kusimamia haki panapo matatizo kwa kuwa wanafungamana na chama cha (zamani).Katiba mpya itutatulie utata huu.
 
Kwa mwendo huu wataendelea kufanya utawala wao kuwa mgumu, kwani wananchi waliowengi watakasa imani nao na kutoshiriki katika miito pamoja na majukumu yatakayokuwa chini ya usimamizi wao.

Ni bora wakaliangali pia kwa jicho la pili, sio kudhani kuwa itawaokoa katika kipindi hiki wanaposhika kwa mwendo kasi mtoroko!
 
Tatizo lipo ktk katiba ya nchi hakuna inapoeleza majukumu ya mkuu wa wilaya au mkoa wapo wapo tuu . Mara mjumbe wa kamati ya siasa mara mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama . Tutoe maoni yetu ktk tume ya katiba.
 
Ni siku chache tokea wakuu wa wilaya walipokula kiapo cha uaminifu wa kuwatumia wananchi wote pasipokujali itikadi za wananchi husika. Cha kushangaza, leo hii Waziri mkuu, mhe.Mizengo Pinda a.k.a mtoto wa mkulima (asiye na shamba) amesema ni sahihi kwa wakuu wa wilaya kuinadi ccm (kama makatibu wenezi) wanapokuwa wilayani haswa katika mikutano ya hadhara.Alipokuwa anajibu swali la Mb.Ezekiel Wenje kuhusu uhalali wa wakuu wa wilaya kukinadi chama wakati wanatumia kodi za watanzania wote kupitia mishahara,usafiri na posho wanazopewa Wakuu hao. Kwa mtazamo wa mtendaji mkuu wa serikali Mhe.Pinda aliyedai ni sawa kunadi chama na kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachokimbiwa na wanachama kila kukicha.Baadhi ya wananchi niliowahoji mjini Mbeya...wamesema hawana imani na wakuu wa wilaya wakiwa kama Wakuu wa ulinzi na usalama wilayani kwani hawawezi kusimamia haki panapo matatizo kwa kuwa wanafungamana na chama cha (zamani).Katiba mpya itutatulie utata huu.

Huu ni ushenzi kabisa. Yaani Mkuu wa Wilaya na Mkoa wanawakilisha SSM wakati wanawakilisha wananchi wote na vyama vyao? They are supposed to be neutral katika siasa. Katiba mpya ifikirie suala hili kwa makini sana. Just a little brain to issues about this sensibly!!!
 
Hivi ni kwanini nchi imetumia rasilimali nyingi kuwalipa wakuu wa mikoa na wilaya pasipo kuandikwa kwa kueleweka majukumu yao tangu 1992 baada ya vyama vingi? Ama kweli Raila Odinga aliona mbali aliposema UTULIVU unatokana na satisfaction au kutojitambua.
 
Huu ni ushenzi kabisa. Yaani Mkuu wa Wilaya na Mkoa wanawakilisha SSM wakati wanawakilisha wananchi wote na vyama vyao? They are supposed to be neutral katika siasa. Katiba mpya ifikirie suala hili kwa makini sana. Just a little brain to issues about this sensibly!!!

Rafiki, mchakato wa sasa wa Katiba Mpya umeshachakachuliwa na hao hao ma-RCs na ma-DCs. Lazima baada ya 2015 tutengeneze mchakato mpya wenye kukubalika na halali ili tupate Katiba ya Ukweli. Mchakato wa sasa ni kiini macho.
 
Kwa hiyo wameshaingizwa rasmi katika kundi la mafisadi. Tutapambana nao mpaka kieleweke, kilio na kusaga meni ni 2015. Pinda keshawafukuza kazi in advance, wasimlaumu mtu.
 
:nerd:Amelewa madaraka pinda....alishawahi ulizwa hilo swali kipindi kile ndo anaanza uwazir mkuu,alijibu kwa nidhamu sana
 
Kwa mwendo huu wataendelea kufanya utawala wao kuwa mgumu, kwani wananchi waliowengi watakasa imani nao na kutoshiriki katika miito pamoja na majukumu yatakayokuwa chini ya usimamizi wao.

Ni bora wakaliangali pia kwa jicho la pili, sio kudhani kuwa itawaokoa katika kipindi hiki wanaposhika kwa mwendo kasi mtoroko!

Hilo jicho la pili wanalo? wangekua nalo mbona wangeona mauchafu yao mengi tu. Nadhani wanalo moja tu tena linaloishiaishia maana inabidi watumie lensi yenye nguvu sana. Na kwa kutumia hiyo lensi kitu chenye ukubwa kama tembo wanakionakama punjeya mtama!! Hebu fikiria ufisadi unaouona; unafikiri wao wanauona?!
 
Ni siku chache tokea wakuu wa wilaya walipokula kiapo cha uaminifu wa kuwatumia wananchi wote pasipokujali itikadi za wananchi husika. Cha kushangaza, leo hii Waziri mkuu, mhe.Mizengo Pinda a.k.a mtoto wa mkulima (asiye na shamba) amesema ni sahihi kwa wakuu wa wilaya kuinadi ccm (kama makatibu wenezi) wanapokuwa wilayani haswa katika mikutano ya hadhara.

Alipokuwa anajibu swali la Mb.Ezekiel Wenje kuhusu uhalali wa wakuu wa wilaya kukinadi chama wakati wanatumia kodi za watanzania wote kupitia mishahara,usafiri na posho wanazopewa Wakuu hao. Kwa mtazamo wa mtendaji mkuu wa serikali Mhe.Pinda aliyedai ni sawa kunadi chama na kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kinachokimbiwa na wanachama kila kukicha.

Baadhi ya wananchi niliowahoji mjini Mbeya...wamesema hawana imani na wakuu wa wilaya wakiwa kama Wakuu wa ulinzi na usalama wilayani kwani hawawezi kusimamia haki panapo matatizo kwa kuwa wanafungamana na chama cha (zamani).Katiba mpya itutatulie utata huu.
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa hawa wakuu wa wilaya walitakiwa kusimamia mchakato wa katiba mpya wakitetewa kuwa hawafungamani na CHAMA CHA MAPINDUZI!imekuwaje ghafla mtoto wa mkulima (anayelima) anatangaza hadharani kuwa wanatikiwa kufanya kazi za ukada kama NAPE na MUKAMA
 
Na hili ni udhaifu mkubwa wa kuweza kuwaelimisha wananchi ili kulifanyia mabadiliko katika katiba. Sijaona umuhimu wa wakuu wa mikoa zaidi ya kujiongezea gharama za kuendesha serikali na kutoa nafasi za zawadi kwa Rais kuwapa watu wake wengi waliokosa Ubunge. Ukuu wa wilaya kazi zake zinatakiwa ziainishwe katika katiba na zisiwe za kiitikadi.
 
wakuu wa wilaya ndio wawakilishi wa rais katika wilaya zao na ndio wasimamizi wa amani na utulivu katika maeneo yao.
 
huu ni upuuzi tu alioujibu pinda kwani kila anaelipwa na serikali kama mfanyakazi ni budi kueneza sera za chama tawala? Au lengo kuu ni kuhudumia jamii yote bila kujali tofauti za itikadi zao kama taifa!! Ifahamike kuwa itafikia kipindi watu watashindwa kujitokeza ktk shughuli za maendeleo kwa kuhofia kwenda kuhubiriwa siasa za chama ambacho kwao ni kero kubwa na chenye kuwatia kichefuchefu.kuna hatari pia ya hata baadhi ya wanafanyakazi wa umma mathalani madaktari,walimu na wengineo kuhudumia watu baadhi kwa kujali msimamo wao wa kiitikadi kwa kisa cha kukubaliana na sera za chama tawala.jamani tunalipeleka wapi taifa hili? nijuavyo mimi public servant yeyote awaye yule hapaswi kujishughulisha na mambo ya kisiasa bali kutekeleza majukumu ya serikali inayoongoza watu wa itikadi zote vinginevyo wasije laumiwa watu wakijitokeza kwa kusema hawaitambui serikali iliyoko madarakani kwa kuwaita wahaini au wanataka nchi isitawalike kama watawala wengi wanaopingwa wakiwashutumu watu wenye kuwapinga...Pinda tafakari kabla hujaropoka!!
 
Mizengo Pinda mimi huwa namfananisha na Masanja Mkandamizaji!

Bora Masanja Mkandamizaji anatufanya tunacheka. Huyu mzee ametufanya tumebaki kulia tu. Anatudanganya masuala ya mkulima wakati kundi la wachache linazidi kuneemeka na nchi hii. Siku ya siku inakuja, hata ikichelewa but yaja.
 
Tatizo lipo ktk katiba ya nchi hakuna inapoeleza majukumu ya mkuu wa wilaya au mkoa wapo wapo tuu . Mara mjumbe wa kamati ya siasa mara mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama . Tutoe maoni yetu ktk tume ya katiba.

Kwenye katika ya sasa majukumu ya mikuu wa mkoa yapo kaka soma vizuri katika no Kama tulivyo watz kukurupukia Hoja hate Kama hatujafanya utafiti
 
Ninamheshimu sana PM lakini ananikwaza maana ukweli ameonyesha udhaifu mkubwa katika kujibu maswali ya papo kwa papo bungeni, kutekeleza ilani ya chama sio siasa, siasa hukoma kwenye kuiandaa, lakini utekelezaji huhusisha taaluma, rasilimali na kodi za wananchi wote pasipo kujali itikadi zao.

Mkuu wa mkoa/wilaya huhusika kwa kiwango kikubwa kusimamia utekelezaji wa ilani na sio kupiga siasa jambo ambalo wakuu wengi hulifanya na cha kushangaza hata PM anaunga mkono, maendeleo yatajia wapi kama wasimamizi wa maendeleo badala ya kuelekeza akili zao na nguvu kwenye maendeleo huelekeza akili hizo na nguvu kwenye siasa?

Inabidi swala la wakuu hao lijadiliwe kwa kina ikibidi waondolewe la sivyo wachaguliwe na wananchi badala ya uteuzi au gharama zao zibebwe na vyama maana wapo kisiasa zaidi na si kiserikali.
 
Tatizo tunaiga kila kitu.

Bunge tumeiga Westminster, mpaka majibu ya hapo kwa papo nayo tumeiga.

Wakati Waziri Mkuu wetu hata kumung'unya boilerplate iliyopakwa koti la ukweli kama PM wa UK hawezi.

Hapo kwenye maswali ya hapo kwa papo hamna desa wala personal assistant kusaidia kupata desa, ndipo unajua nani fahali na nani ndama.
 
Back
Top Bottom