Mizengo Pinda amkaribia Nyerere kwa Uongozi Bora

hawa majamaa utani wao mmbaya. kwanza umeona hiyo asilimia ya popularity sijui wametumia ratio gani kupata 81, 73, 60, 45, 37, 34, 24, 20, 18 na kumi 14 au hata asilimia hawajui ni nini.

kiongozi bora ni yule ni mwenye msimamo wa maendeleo nyerere akuwa perfect kwenye kutuendeleza lakini. lakini msimamo wake wa umoja wetu ni kitu muhimu sana kwa hilo tu sidhani kama kuna viongozi wengi africa wana mkaribia. kwani nchi nyingi tu mpaka karne hii bado wanapata matatizo na mambo aliyoyaona tangu miaka ya sitini.

sokoine alikuwa na msimamo wake na ushujaa wa kutupwa katika alichokiamini, hii ni ishara ya kiongozi bora katika kipindi chake cha tanzania na socialism. ilaa ishujaa wake ungetupeleka pabaya ila ni sifaa ya kiongozi uumpe kwa msimamo wake na situation yenyewe.

Msuya alikuwa na msimamo wake Mwanga lazima kupate lami na umeme na akina nani lii washike hizi sudeko etc, etc. kwao upareni ni karibu na mtume huko lakini kwa taifa sijui wengine hila kwangu hana sifa ya kiongozi bora akua na msimamo wa taifa.

Lowassa ana msimamo wake tanzania itanikoma, nntakula kwa namna yeyote bila wa woga janja ni kumpata mtu atakae nifumbia macho watanzania wenyewe shauri zao yaani huyu kama histroria itaweza kumfuta ni vyema tu ili kuwaongepea wanetu tanzania amna watu wenye roho mbaya hizo.

huyu pinda yuko kwenye wakati tanzania ina ufisadi wa hali ya juu, ana anachosema wala ajulikani anasimamia wapi? zaidi ya kulopoka lopoka akizani ana danganya watoto wa chini ya miaka tano au anawatishia nyau watu wazima, kwa hoja zake za muungano hata sijui kama ni waziri mkuu hau ndio kwa sababu serikali yetu lazima iwe na mtu wa kuwa najina hilo ndio hapo anakuja pinda yupo kama ayupo.
 
Last edited by a moderator:
Kawawa maskini, mzee wa Muhogo Mchungu. Tuna ex PM jamani ambaye alishawahi kuwa ze komedi ya mwaka 47!
 
naamini wakifanya tena leo atakuwa wa mwisho

ha ha ha, kind of researches za kitanzania ambazo prof karim f hirji anaziita takataka
 
Kiukweli Pinda hapana. Tunamheshimu ila apo ajue anapakwa mafuta na mgongo wa chupa. Nadhani yuko safi kwenye kuvunja katiba. (Anayeua maalbino auawe).
 
Utafiti wa kijinga huu, nyerere kumfananisha na pinda? then ampite Sokoine!
Pinda huyuhuyu Mbwiga?
 
Watuhumiwa wa EPA hawakamatiki ~ MKP
Watuhumiwa wa EPA wakikamatwa nchi italipuka ~ MKP
 
Pinda!!!! mmmmmmhhh! Heri bibi yangu anaweza uongozi sio huyu Pinda. Maziri mkuu unawaogopa wezi?!! Then umfananishe na Nyerere kama sio utani ni nini
 
hivi Sokoine ameshawahi kumwaga chozi Bungeni?...
bishana kokote, Tanzania haijawahi kupata kiongozi sio tu wa nafasi ya uwaziri mkuu bali ktk nafasi zoote kama Edward wa ukweli yaani Edward Moringe Raiboni Sokoine.
Hayati Sokoine ilikuwa ni zawadi yetu watanzania toka Mbinguni.

Sokoine ndie Kiongozi pekee ambaye leo hii akifufuka basi mafisadi watarudisha mali zote walizotuchapa na kisha kila mmoja atajipeleka Gerezani.
 
Kwa kweli kumlinganisha Nyerere na Mizengo Pinda si chochote zaidi ya matusi kwa historia ya nchi yetu.
 
Hiyo research sikubaliani nayo, siamini kabisa kama Nyerere alikuwa kiongozi bora. Nnavyojuwa Nyerere alishindwa kabisa kuiongoza nchi.
 
Hao Synovate waweke hiyo "Poll" yao hapa halafu na sisi tujibu maswali yao na kupiga kura tuone kada ya wasomi inasimamia wapi kuhusu hao viongozi.


wasoomi waapii.. JF.!! Uharo mtupu.
 
Shamu na Kigogo vichwa vyenu vibovu!

Huo utafiti unalinganisha waliowahi kuwa mawaziri wakuu. Nyerere ndio kinara wao, hata Pinda anapiga mzigo vizuri. Sijui nyie mnadhani nani alikuwa bora!

Jaman Pinda huyuhuyu 2nayemjua ama pinda mwingine???
acheni unafiki, Pinda ni kiongozi muoga kuliko wote, hawezi kucmamia hoja, ni mtu wa kujiumauma daily, Nyerere hana wa kumfananisha naye, aliikuta nchi haina wasomi wala lolote.
 
Back
Top Bottom