Miwasho baada ya kuoga inatibika vipi?

frenderPH

JF-Expert Member
Oct 30, 2019
619
806
Habari zenu wana Jamii Forum. Poleni kwa changamoto na mchaka mchaka wa utafutaji pesa na kadhalika.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi mwenzenu katika hili jukwaa la Urembo, mitindo na Utanashati nahisi nnashida ambayo inanitesa sana saivi ni takriban miaka minne.

Yani iko hivi, shida ninayoipitia ni kwamba kila nikitoka kuoga nahisi kuwashwa washwa kwenye ngozi kila mahali ya mwili wangu hata sometimes nikitaka kuoga naanza kua na mawazo.

Yani kila nikimaliza kuoga nawashwa karbia dakika 15 au 20, kila sehemu ya mwili inawasha lakini hauvimbi wala nini. Na baada ya hizo dakika 15 au 20 za kuwashwa kuisha naendelea na maisha freshi tu kama hakukua na tatizo lolote.

Nimesha badilisha kila aina ya sabuni na madodoki nikihisi pengine labda chanzo ndo hiko lakini hii hali bado inanisumbua vibaya mno.

Sasa wadau wangu wa Jamii Forum hasa katika hili jukwaa kwa wale ambao wameshapitia hii hali na ambao hawajapitia lwa ujumla. Naombeni ushauri nifanyeje ili niondokane na hii hali maana inanitesa sana.
 
Pole sana nahisi nilishakutana na changamoto ya aina hiyo , badae nikaja gundua sabuni hizi zinakemikali zinazosababisha shida hiyo, nikawa naoga then natumia maji mengi kujisuuza bila sabuni, shida hiyo now siioni
Nb. Mf. Jaribu kuoga bila sabuni uone kama itatokea the same
 
Habari zenu wana Jamii Forum. Poleni kwa changamoto na mchaka mchaka wa utafutaji pesa na kadhalika.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi mwenzenu katika hili jukwaa la Urembo, mitindo na Utanashati nahisi nnashida ambayo inanitesa sana saivi ni takriban miaka minne. Yani iko hivi, shida ninayoipitia ni kwamba kila nikitoka kuoga nahisi kuwashwa washwa kwenye ngozi kila mahali ya mwili wangu hata sometimes nikitaka kuoga naanza kua na mawazo. Yani kila nikimaliza kuoga nawashwa karbia dakika 15 au 20, kila sehemu ya mwili inawasha lakini hauvimbi wala nini. Na baada ya hizo dakika 15 au 20 za kuwashwa kuisha naendelea na maisha freshi tu kama hakukua na tatizo lolote.

Nimesha badilisha kila aina ya sabuni na madodoki nikihisi pengine labda chanzo ndo hiko lakini hii hali bado inanisumbua vibaya mno.

Sasa wadau wangu wa Jamii Forum hasa katika hili jukwaa kwa wale ambao wameshapitia hii hali na ambao hawajapitia lwa ujumla. Naombeni ushauri nifanyeje ili niondokane na hii hali maana inanitesa sana.

Ni minyoo wa kwenye ngozi mi nilisumbuliwa sana nikanywa dawa ya kienyeji ya wamasai nikapona mwanzoni nilihisi sabuni hola nikahisi maji hola nikahisi dodoki hola baadae jikamweleza dokta mmoja wa ngozi akaniambia kuna dawa ya sindano kuchoma au vidonge,au nikiamua nitafute ya kienyeji ndio nikapata kwa mmasai huyo alienda nichimbia nikainywea kwenye kahawa ila ilikuwa chungu balaa nimepona mpaka leo tatizo limeisha
 
1.badilisha taulo au kifuta maji kama ni cha muda mrefu nunua kipya pengine yaweza kuwa ni bacteria wa ngozi
2.usitumie maji chumvi kuogea
3.usitumie sabuni za magadi kuogea
4.kunywa maji kwa wingi kuweka ngozi yako sawa
5.tumia mafuta universal kama vile vaseline nk baada tu ya kuoga

NB:kama tatizo litaendelea ni vema ukamuona daktari alie karibu nawe

jaribu hizi 5 kwa muda wa week 1 tu naamini tapata matokeo mazuri kwa idhini ya (Mwenyezi Mungu) na pia pole sana kwa changamoto hio
 
Weka chumvi ya mabonge kwenye maji kabla hujaanza kuoga itakusaidia sana
 
1.badilisha taulo au kifuta maji kama ni cha muda mrefu nunua kipya pengine yaweza kuwa ni bacteria wa ngozi
2.usitumie maji chumvi kuogea
3.usitumie sabuni za magadi kuogea
4.kunywa maji kwa wingi kuweka ngozi yako sawa
5.tumia mafuta universal kama vile vaseline nk baada tu ya kuoga

NB:kama tatizo litaendelea ni vema ukamuona daktari alie karibu nawe

jaribu hizi 5 kwa muda wa week 1 tu naamini tapata matokeo mazuri kwa idhini ya (Mwenyezi Mungu) na pia pole sana kwa changamoto hio
Good ushauri. Pia anaweza kutumia sabuni isiyo na manukato. Fragrance-free soap inaweza saidia.
 
Hilo tatizo haliishi ila unaweza kulicontrol na kuishi nalo, Mimi toka nijifahamu nimekua nalo, now nimekua mkubwa najua cha kufanya.

Kwanza lazima ufahamu kuwa unaasili ya ngozi kavu ndio maana unawashwa ikikutana na vitu kama 1.Maji ya baridi sana, 2. Maji ya moto sana. 3. Baridi au upepo mkali baada ya kuoga, 4. Sabuni yenye manukato na kemikali kali, 5.kujifuta mwili na nguo au taulo lenye unyevu, au chafu 6.kujisugua mwili na dodoki gumu au kujisugua sana 7.Kusugua mwili kwa scrub.

Sasa kazi kwako kuavoid hizo situations, Usioge maji ya moto sana au ya baridi sana pendelea ya uvuguvugu, Epuka sabuni za manukato kama alivyosema mdau hapo juu, sugua mwili kwa mikono tu au kitambaa laini, ukimaliza kuoga usikae na maji, jikaushe kwa taulo/nguo safi then paka mafuta mazito yenye moisture then stay hydrated. Halafu tuletee mrejesho.

Mimi hizo measures zimenisaidia siku hizi siwashwi kabisa siku zingine nawashwa kwa mbaali nikikosea step. Waliokwambia juu ya kwenda hospitali, unaweza kujaribu lakini kwangu mimi dawa nilizopewa hazikufanya kazi, Ohh its bad, nilikua sipendi wala sifurahii kuoga.
 
Ni minyoo wa kwenye ngozi mi nilisumbuliwa sana nikanywa dawa ya kienyeji ya wamasai nikapona mwanzoni nilihisi sabuni hola nikahisi maji hola nikahisi dodoki hola baadae jikamweleza dokta mmoja wa ngozi akaniambia kuna dawa ya sindano kuchoma au vidonge,au nikiamua nitafute ya kienyeji ndio nikapata kwa mmasai huyo alienda nichimbia nikainywea kwenye kahawa ila ilikuwa chungu balaa nimepona mpaka leo tatizo limeisha
Fuata huu ushauri pia. Minyoo ni sababu kubwa ya ngozi kuwasha baada ya kuoga au ukisimama Juani
 
Back
Top Bottom