benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Mitungi ya gesi 71,000 yenye thamani ya Sh3 bilioni inatarajiwa kusambazwa na kugawiwa bure katika mikoa 26 ya Tanzania Bara, lengo likiwa ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Mitungi hiyo itagawiwa baada ya Serikali kutoa ruzuku ya asilimia 100 kwa awamu ya kwanza na tayari kampuni nne, ikiwemo Oilcom, Lake Oil, Oryx na Taifa zimeshatangazwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwamba zitakuwa zinasambaza mitungi hiyo.
Akizungumza kwenye shughuli ya utiaji saini mkataba na kampuni tatu kati ya nne zitakazokuwa zinasambaza
mitungi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Hassan Saidy alisema mpango huo unahusisha usambazaji mitungi ya gesi, vipikio pamoja na kichomeo kidogo (bana).
Alisema katika ugawaji wa mitungi hiyo kwa awamu ya kwanza wataanza na taasisi zinazohudumia kuanzia
watu 100, huku akieleza kuwa wanategemea mkakati huo utaongezeka kulingana na gharama halisi ya mradi huo.
"Gharama za mradi ni Sh3 bilioni ambazo zitawezesha usambazaji wa mitungi 71,000 na mtungi mmoia kulingana na bei tuliyoingia mkataba utakuwa kwa Sh 38,000 hadi Sh 45,000 kutegemea kampuni na mkoa. Mfano Dar es Salaam ni Sh38,000," alisema.Mitungi hiyo itagawiwa baada ya Serikali kutoa ruzuku ya asilimia 100 kwa awamu ya kwanza na tayari kampuni nne, ikiwemo Oilcom, Lake Oil, Oryx na Taifa zimeshatangazwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwamba zitakuwa zinasambaza mitungi hiyo.
Akizungumza kwenye shughuli ya utiaji saini mkataba na kampuni tatu kati ya nne zitakazokuwa zinasambaza
mitungi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Hassan Saidy alisema mpango huo unahusisha usambazaji mitungi ya gesi, vipikio pamoja na kichomeo kidogo (bana).
Alisema katika ugawaji wa mitungi hiyo kwa awamu ya kwanza wataanza na taasisi zinazohudumia kuanzia
watu 100, huku akieleza kuwa wanategemea mkakati huo utaongezeka kulingana na gharama halisi ya mradi huo.
Alisema mikoani bei itapanda kutoka Sh41000 hadi 45,000, huku akieleza Serikali inatoa ruzuku hiyo ili iwe chachu kwa kuwa kuna sababu nyingi zinazochangia watu wasitumie nishati safi, ikiwemo uelewa na hali yao ya uchumi.