Mitandao ya Simu KERO..KEROOO, WIZI MTUPU!!!

Eng Kimox Kimokole

JF-Expert Member
Jun 9, 2010
1,032
759
HEBU TUZITAZAME HIZI KERO ZA MITANDAO YETU YA SIMU >>>

Binafsi ninazo 'line' za mitandao yote minne inayofanyakazi hapa Nchini. Sikupenda tu kuzimiliki bali nililazimishwa na ukali wa gharama za kuunganishiwa simu pale unapompigia simu mtu mwenye mtandao tofauti! Nikajikuta nimemiliki line hizo zote! Sasa hivi nasikiasikia eti gharama hizo zimehuishwa hata hivyo sina hakika ni kwa kiasi gani.

Nimeamka asubuhi ya leo kwa kuamshwa na simu ya kutoka nyumbani kwetu kijijini. Ndugu yangu huyu amenipigia katika line ya TIGO, lakini akaniomba tafadhali nimpigie!

Hapo kichwa kikaanza kuniuma! Ni kutokana na huu mpango ulioanzishwa na mitandao yote ya simu, kwamba 'nafuu ya gharama za simu ni kujiunga na PROMOSHENI mbalimbali zenye gharama tofauti kwa muda tofauti wa maongezi, sms, na Mb za kufacebooker!

Sasa sikiliza huu wazimu: Juzi nilichagua kutumia line ya VODA. Nikajiunga hivi: *147*600# ili nitumie sh 600 kwa siku hiyo. Wakanijibu kuwa wamenipatia sekunde 1200 za kupiga mitandao yote, sms 150 na 60mb! Baada ya ujumbe huo, mtandao ukakatika na haukuimarika kutwa nzima hadi masaa 24 baadaye, nikapata ujumbe wa kwamba Kifurushi chako cha CHEKA kimekwisha, kujiunga tena piga namba . . . ! Jeeeeesus!

Kwa hasira sikujiunga tena na VODA kwa jana, nikaamua kuchagua AIRTEL 'Line nyingi za nini? Moja yatosha!' Nikabofya *149*99*01# Nikapokea maelekezo nikachagua kifurushi cha siku cha sh 999 ambacho wakanijulisha wamenipatia Dk 40 za kuwasiliana mitandao yote! Kweli nilibahatika kupiga simu kadhaa lakini cha ajabu nao wakati kifurushi kinakaribia kwisha hawakujulishi! Wakaniacha nikaongea hadi wakanikatia simu huku wakileta sms inayonitaarifu kuwa kifurushi kilikwisha na nimeendelea kuongea hadi kufyeka salio langu lote! Kifurushi chote cha 999, na kwa kuwa simu ya mwisho nilikuwa naongea na mtu wa TIGO, mara tu sekunde kifurushi kilipokomea, wakafyeka salio langu lote sh 1,001 zilizokuwa zimesalia baada ya kununua kifurushi cha 999! Kutwa nzima ikabakia biashara ya sms! Hahaaa!

Leo sasa! Leoo! Nimeamua kujiunga na TIGO! Hawa TIGO nao nilisahau tu kuwa majuzi walinikera! Nilisahau leo nimejiunganisha tena. Hebu sikia maudhi au kero zao: Unapopiga - *148*01# Wanakupeleka kwenye ulimwengu wao wa KABANG! Kuna machaguo mbalimbali pia! Nimeamua kuchagua MINI KABANG: Ninajulishwa kuwa chaguo langu litanipatia Dk 25 kwenda mitandao yote. Nimeipenda hii! Lakini mara tu ninapojiunga, ninapokea maelezo mapya! Mara hii ninapokea mchanganuo mpya; ninaambiwa: "Umepata Dk 15 TIGO - TIGO, Dk 10 kwenda mitandao yote Tz, sms 300 & MB 60 kwa shs 600 tu. Tumia ofa yako ndani ya masaa 24! Hawa hawa TIGO waliponichanganya majuzi, nilijiunga na KABAANG ambayo wakanijulisha mwanzo kuwa wangenipatia Dk 40 kwenda mitandao yote! Lakini baada ya kukubali tu, kama leo, wakaniletea maelezo mapya, wakichanganua kwamba, katika hizo Dk 40 walizonipa, Dk 30 nizitumie TIGO - TIGO, na 10 tu ndiyo walizoniachia nitumie kwa mitandao mingine! Huu sio UTAPELI? Sio KERO kweli? Nafuu iko wapi waliyotuahidi wabunifu wa SERA? Na je, Hata haya mapatano ya 'mawasiliano kwa Vifurushi, Wazazi wetu wanaomiliki simu huko vijijini wanao upeo wa kutosha kweli wa kufuatilia huu utaratibu wa Mawasiliano kwa Vifurushi? UTAPELI MTUPU!
 
Ktk sekta ambayo tunaibiwa kwa kiwango cha juu ni mawasiliano. Yaani hakuna sehemu inayogharimu fedha nyingi bila kujijua kama mawasiliano.

Kwa kifupi hakuna mtandao rahisi kwa mawasiliano hapa Tanzania, ni maumivu kila uchao na hatuna mtetezi.
 
Hii mitandao wizi tu,wala hakuna cha promosheni,ukiwa hata na salio ndani ya simu ndo ugonjwa wa moyo,yaani wanakwangua kabisa.TIGO ndo balaa kweli
 
Ktk sekta ambayo tunaibiwa kwa kiwango cha juu ni mawasiliano. Yaani hakuna sehemu inayogharimu fedha nyingi bila kujijua kama mawasiliano.

Kwa kifupi hakuna mtandao rahisi kwa mawasiliano hapa Tanzania, ni maumivu kila uchao na hatuna mtetezi.

Mkuu umesahau na kwenye mabenk.
Washajua matanzania ni mazezeta.
 
Mkuu umesahau na kwenye mabenk.
Washajua matanzania ni mazezeta.

Inaanza mitandao ambayo tunaibiwa kila sekunde ipitayo bila kupumzika kwa siku 7 zote za wiki ikifuatiwa kwa karibu kabisa na taasisi za kifedha kama mabenki ambayo yanaiba kwa kustukiza ndani ya siku 6 za wiki.

"Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu" - Mwinyi.
 
"mtandao ukakatika na haukuimarika kutwa nzima hadi masaa 24 baadaye"
kwahiyo mkuu hukutumia hata kidogo kifurushi chako!!!
Aise pole.
 
tunaibiwa sana.. mimi huwa najiulza kwa wazee wa vijijini wasiojua mambo ya kabaang kwao sijui inakuwaje
 
HEBU TUZITAZAME HIZI KERO ZA MITANDAO YETU YA SIMU >>>

Binafsi ninazo 'line' za mitandao yote minne inayofanyakazi hapa Nchini. Sikupenda tu kuzimiliki bali nililazimishwa na ukali wa gharama za kuunganishiwa simu pale unapompigia simu mtu mwenye mtandao tofauti! Nikajikuta nimemiliki line hizo zote! Sasa hivi nasikiasikia eti gharama hizo zimehuishwa hata hivyo sina hakika ni kwa kiasi gani.

Nimeamka asubuhi ya leo kwa kuamshwa na simu ya kutoka nyumbani kwetu kijijini. Ndugu yangu huyu amenipigia katika line ya TIGO, lakini akaniomba tafadhali nimpigie!

Hapo kichwa kikaanza kuniuma! Ni kutokana na huu mpango ulioanzishwa na mitandao yote ya simu, kwamba 'nafuu ya gharama za simu ni kujiunga na PROMOSHENI mbalimbali zenye gharama tofauti kwa muda tofauti wa maongezi, sms, na Mb za kufacebooker!

Sasa sikiliza huu wazimu: Juzi nilichagua kutumia line ya VODA. Nikajiunga hivi: *147*600# ili nitumie sh 600 kwa siku hiyo. Wakanijibu kuwa wamenipatia sekunde 1200 za kupiga mitandao yote, sms 150 na 60mb! Baada ya ujumbe huo, mtandao ukakatika na haukuimarika kutwa nzima hadi masaa 24 baadaye, nikapata ujumbe wa kwamba Kifurushi chako cha CHEKA kimekwisha, kujiunga tena piga namba . . . ! Jeeeeesus!

Kwa hasira sikujiunga tena na VODA kwa jana, nikaamua kuchagua AIRTEL 'Line nyingi za nini? Moja yatosha!' Nikabofya *149*99*01# Nikapokea maelekezo nikachagua kifurushi cha siku cha sh 900 ambacho wakanijulisha wamenipatia Dk 25 za kuwasiliana mitandao yote! Kweli nilibahatika kupiga simu kadhaa lakini cha ajabu nao wakati kifurushi kinakaribia kwisha hawakujulishi! Wakaniacha nikaongea hadi wakanikatia simu huku wakileta sms inayonitaarifu kuwa kifurushi kilikwisha na nimeendelea kuongea hadi kufyeka salio langu lote! Kifurushi chote cha 900, na kwa kuwa simu ya mwisho nilikuwa naongea na mtu wa TIGO, mara tu sekunde kifurushi kilipokomea, wakafyeka salio langu lote sh 1,100 zilizokuwa zimesalia baada ya kununua kifurushi cha 900! Kutwa nzima ikabakia biashara ya sms! Hahaaa!

Leo sasa! Leoo! Nimeamua kujiunga na TIGO! Hawa TIGO nao nilisahau tu kuwa majuzi walinikera! Nilisahau leo nimejiunganisha tena. Hebu sikia maudhi au kero zao: Unapopiga - *148*01# Wanakupeleka kwenye ulimwengu wao wa KABANG! Kuna machaguo mbalimbali pia! Nimeamua kuchagua MINI KABANG: Ninajulishwa kuwa chaguo langu litanipatia Dk 25 kwenda mitandao yote. Nimeipenda hii! Lakini mara tu ninapojiunga, ninapokea maelezo mapya! Mara hii ninapokea mchanganuo mpya; ninaambiwa: "Umepata Dk 15 TIGO - TIGO, Dk 10 kwenda mitandao yote Tz, sms 300 & MB 60 kwa shs 600 tu. Tumia ofa yako ndani ya masaa 24! Hawa hawa TIGO waliponichanganya majuzi, nilijiunga na KABAANG ambayo wakanijulisha mwanzo kuwa wangenipatia Dk 40 kwenda mitandao yote! Lakini baada ya kukubali tu, kama leo, wakaniletea maelezo mapya, wakichanganua kwamba, katika hizo Dk 40 walizonipa, Dk 30 nizitumie TIGO - TIGO, na 10 tu ndiyo walizoniachia nitumie kwa mitandao mingine! Huu sio UTAPELI? Sio KERO kweli? Nafuu iko wapi waliyotuahidi wabunifu wa SERA? Na je, Hata haya mapatano ya 'mawasiliano kwa Vifurushi, Wazazi wetu wanaomiliki simu huko vijijini wanao upeo wa kutosha kweli wa kufuatilia huu utaratibu wa Mawasiliano kwa Vifurushi? UTAPELI MTUPU!

Kwa Airtel *149*99# 999Tsh unapata Dk 40 na sio 25 alafu *149*99*01# kama ulikuwa unatumia cm ya double line kilikupeleka kwenye Vodacom.

Kila unapomaliza kuongea Airtel wanatoa sms inayokuonyesha umetumia dk ngapi na umebakiwa na ngapi fanya utafiti vizuri ...
 
Kuna mtandao mmoja wao wanachukua salio lao usiku,ukilala na salio basi imekula kwako,washachukua chao uck kimya kimya
 
Kutokana nanausumbufu wa voda,eartel nimeamua kujiunga na halotel angalau wao bado hawajawa wajuaji lakini pia intanet yao ikofasita sana mkuu jiunge huko
 
Back
Top Bottom