Stories of Change - 2023 Competition

Dr Erasmi

New Member
May 31, 2023
4
3
Siku hizi ulimwengu wa leo umekuwa ukitumia njia za mkato katika tiba za dalili ya ugonjwa wanaoupitia. Bila kujali kumwona Daktari kwa vipimo ili kugundua Magonjwa yanayo wakabili, Mfano Mtu anaweza akaumwa kichwa kisha kwenda duka la dawa na kuchukua dawa za kupunguza Maumivu bila kujali matokeo hatarishi yanayoweza kujitokeza kwake pasina kufika kituo cha Afya.

Hii imekuwa mazoea vivyo hivyo mtu akiumwa tumbo na kupata Maumivu anapo jisaidia haja ndogo hukimbilia kutumia dawa za kupambana na maambukizi katika njia ya Mkojo. Utumizi huu wa dawa umekuwa ukitumika pasina kupewa ushauri na daktari pasina kufahamu ni hatari kwa afya ya binadamu.

Athari mojawapo ya haya ni kuchosha Ini, na figo katika uchakataji wa dawa na kuchuja sumu mwilini na hatimaye kuweza kufikia kufeli kwa Ini au Figo. Pili kutokana na kutotibu ugonjwa husika kwa wakati sababu ya kutumia dawa bila kufahamu nini kinawasumbua.

Hali hii inaweza pelekea ugonjwa kukua zaidi na kuenea, hii huweza sababisha kushindwa kudhibiti ugonjwa huo na kisha kuleta athari, Mfano anayeumwa kichwa na kutumia dawa za Maumivu na kuacha kwenda kuchukua vipimo kwa daktari, kwa hali hii kama itakuwa ni ugonjwa wa Malaria unaeza panda kichwani na kusababisha hali kuwa mbaya zaidi na hata kuhatarisha maisha. Tatu inaweza ikapelekea athari za usugu wa Madawa katika kupambana na vimelea vya maradhi.

Wataalamu wa Afya wengine wamekuwa wakifika mbali zaidi, inatokea mtaalamu wa afya wa kada flani anafika mahala kutekeleza majukumu yasiyo ya kada yake husika. Mojawapo Mfano kada ya famasi utaalamu wao ni dawa tu na si kuchoma sindano, shida inakuja pale Mtaalamu wa kada ya famasi anapo jaribu kuchoma sindano na si kazi yake. Mfano mwingine baadhi ya madaktari wa ngazi flani ya utabibu kufanya majukumu ya ngazi ya Daktari wa Shahada.

Kitendo hiki kinaweza kutokea pale watumishi wa Afya ni haba yaani wachache kulinganisha na majukumu. Ila baadhi ya wataalamu mitaani hufanya hivyo kinyume na utaratibu pasipo kuwa na sababu yoyote ya msingi.

Hali hii ikiendelea ni moja ya uhatarishi wa afya za watu katika jamii. Kuna umuhimu wa wataalamu wetu wa afya kuziheshimu kada zao na kuwa waaminifu na kutetea afya za Watanzania na wana jamii wote.

Aidha pia kuna umuhimu wa kujali na kuwaheshimu wataalamu wetu wa Afya. Hii huwa inawapa nguvu katika kutekeleza majukumu yao kwa usahihi. Jamii ya leo asilimia kubwa ya watu inashindwa kutoa heshima kwa wataalamu wetu wa afya, bila kujali ni kwa kiasi gani watumishi wetu wa afya wanajitoa kuacha familia zao na kwenda kutetea afya za watu wengine.

Hali hii husababisha wataalamu wetu wa afya kukosa hari ya kazi na kupelekea kukosa uaminifu katika utendaji wa majukumu yao.

Tunaweza kuboresha huduma za Afya, kwa kupitia kuboresha stahiki na maslahi kwa wataalamu wetu wa afya kupitia Serikali yetu na hata Sekta binafsi. Njia hii itasaidia kuongeza chachu kubwa katika utendaji, mojawapo kuboresha vima vya mishahara, posho na vitendea kazi katika Vitua vya afya. Njia hii itasaidia wataalamu wetu wa afya kuongeza chachu na uimara katika kutimiza majukumu yao.

Uboreshaji wa Afya kwa jamii inaweza kufanikiwa kwa kutoa rai na elimu kwa jamii kuhusu namna ya kulinda na kuboresha afya zao. Kutoa elimu kwa jamii kuwafahamisha umuhimu na madhara ya kutojali afya zao. Kuieleza jamii wanaweza kuwaona wataalamu wa afya husika kwa wakati husika ili kulinda na kuboresha afya zao.

Pia kusihi jamii kutumia lugha njema kwa wataalamu wetu wa afya kabla na baada ya huduma pia. Vivyo hivyo wataalamu wetu wa afya wanapaswa kutumia lugha njema kwa wagonjwa.

Aidha Watumishi wa afya wanapaswa kuzingatia haiba, sheria na kanuni za baraza la taaluma husika kwa uaminifu mzuri. Hii itasaidia kutoa huduma kwa wagonjwa vizuri bila kuharibu utu wao. Pia itawafanya wana jamii pale wapatapo maradhi kuweza kufika vituo vya afya kwa matibabu bila hofu yoyote ile.

Kuna umuhimu wakati wa utolewaji wa taaluma za afya Chuoni. Ipo haja ya kuboresha usimamizi na utoaji elimu za kanuni za taaluma husika kupitia vyama hivyo vya kitaaluma vya wanafunzi vyuoni.

Hii itasaidia kutengeneza wataalamu wenye tija na taaluma yao na uaminifu. Kwa usahihi vyama vya kitaaluma vyuoni vizidi kutoa elimu ya taratibu na kanuni za taaluma husika kwa wanafunzi wa kada za afya.

Vyama hivyo vya kitaaluma vyuoni katika kada za afya ni pamoja na TAMSA kwa wanafunzi wa Udaktari, TAPSA kwa wanafunzi wa famasi, TEMELASA kwa wanafunzi wa Maabara. Vivyo hivyo na taaluma ya wanafunzi wa Uuguzi na taaluma zingine za afya vyuoni.

Hivi sasa tunaona jitihada za Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya Sita, inayo ongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Inasaidia kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa kuboresha Miundombinu ya hospitali za Kanda na za rufaa pamoja na kuboresha huduma za afya.

Hivyo Wananchi wakipata elimu kupitia Semina za tambua umuhimu wa kujali afya zao. Hii itasaidia wana jamii kutumia vyema fursa kufika katika Vituo vya afya na kuonana na watumishi wa afya kwa suluhishi ya maradhi yanayo wakabili na pindi wanapo jihisi hawapo sawa kiafya. Aidha pia itawasaidia kulinda na kuboresha afya zao, pamoja na kujikinga na maradhi nyemelezi.

Kuna umuhimu Mkubwa sana wa semina za afya kwa jamii hizi zinahitajika kwa kiasi kikubwa. Hii itasaidia jamii kuweza kutambua namna gani wanaweza kujali afya zao na kujikinga na maradhi.

Jamii inaweza kutambua namna gani wanaweza kukabiliana na milipuko ya maradhi pindi inapotokea, kupitia semina za itambue afya yako kwa jamii. Kutasaisia wananchi kufahamu umuhimu wa kufika vituo vya afya na kuwaona wataalamu wa afya.

Sekta ya afya inaweza kuboreshwa kwa ushirikiano kupitia sekta binafsi kwa kuungana na Serikali katika kuboresha huduma za afya. Aidha vitengo vya afya, umoja wa baraza za taaluma husika, kuungana na Serikali kupitia wizara ya afya zinaweza kuungana katika kusimamia misingi na kanuni za taaluma husika.

FB_IMG_16902005809831745.jpg
 
View attachment 2697915
Hongera Sana, nimependa sana hii, ni moja ya misingi bora inayo weza kusaidia katika kuboresha sekta ya afya Nchini mwetu
 
Back
Top Bottom