Ukitaka kuliwa sharti na wewe uliwe
No pain no gain
Nioshe
Ni mtazamo tu.
Raha jipe mwenyewe..
Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge..
Mwanzo mgumu..
Kufa kufaana..
Ukitaka upakatwe...
Hapa stori tu,kula kwenu...
Alfa na omega...
1. Mwisho wa ubaya aibu
2. Hata mbuyu ulianza kama uyoga
3. Nibora kuishi na nyoka pangoni kuliko kuishi na mwanamke mkorofi
4. Kuwa mkweli leo ili usiadhirike kesho
5. Iga ufe
6. Kunya kanya kuku bata akinya kaharisha
7. Kesi ya nyani kapelekewa ngedere
8. Mwanamke kiuno makalio hata kwa mchina yapo
9. Baba kanikataza
10. Mali ni mateso
Maanta utuh(sina hakika na herufi zake) ikimaanisha Ubinaadamu kazi!
Uza nyuba jenga heshima baa
Kuna jamaa alilowea mjini na akawa anapata lawama nyingi kutoka 'home' kuwa haendi kusalimia, alipozichonga akanunua gali na kuliandika hivi 'Baleke bajobheke, Pambwani panyafu'. Guess alikuwa mutu ya wapi?
Ni kweli muungwana misemo ya kwenye vyombo vya barabarani ni mingi na baadhi inachekesha. Yote uliyoiandika imo ila nitaongeza baadhi. Umekuwa mtindo kwa wenye mabasi na malori kuandika pia majina ya vitu au kitu kinachojulikana na wengi.Nakumbuka kwa mfano mwaka 1997-2000 wakati kituo cha ITV kinaonyesha tanthiliya ya EGOLI, mabasi kadhaa ya abiria Yalichora neno EGOLI kwenye bodi za mabasi hayo, hasa kwenye kioo kikubwa cha nyuma. Baadhi ya misemo mingine ni:
Kama kuoga ni usafi kwanini taulo huchafuka?
Kama waijua kaizibe
Wakati mwingine hata majina ya watu maarufu duniani hutumiwa sana.Nilishapata kuona mabasi yameandikwa:
Hans Blix
George Bush
Osama bin Laden
Sylvester Stallone
Arnold Shwaznagger nk
Baada ya miezi miwili usishangae kuona basi limeandikwa "Mafuriko ya Dar"
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.