Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Ni Vizuri Kama Huna Cha Kuchangia Basi Wewe Pita Tu Na Sikuhitaji UBWABWAJI Wako Huu Na Isitoshe Watu Wenye Akili Zao Wameshajibu Na Tunaliendeleza. Umekuja Na Hoja Ya Dala Dala ILA Mimi Nimekuja Na Hoja Ya Magari Aina Ya DalaDala Na Malori. Bahati Yako Sasa Ni Usiku Na Nataka Kulala ILA Ungenieleza Upuuzi Wako Huu Asubuhi au Mchana au Jioni UNGEYAKOGA KISAWASAWA na Ninge Ku Lui Suarez. Kila La Kheri JUHA Wewe.....................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Lisondo lya nyakwe.....!
 
Natumai Nyote Hamjambo Huku Tukizidi Kuliendeleza LIBENEKE Letu.
Jamani Mimi Nimejikuta Nikipenda Sana Kusoma Yale Maneno Ambayo Huandikwa ktk Eiether Mabasi Yetu Haya ( Dala Dala ) Or ktk Malori Ya Mchanga Pamoja Na Magari Ya Kubeba Taka.

Kwa Mfano Leo Nimekutana Na Magari Ya Aina Hiyo Mawili Moja Likiwa Dala Dala ( MKANGAFU ) Nikimaanisha Yale Ma DCM Likiwa Limeandikwa " KAMA SHIDA INGEKUWA SUMU WOTE TUNGEKUFA " Na Gari La Taka Nalo Likiwa Limeandikwa " MGANGA HAOMBI DAGAA " Siyo Siri Nilijikuta Nikivunja Mbavu Na Kujiuliza Ni Wapi Watu Hutoa Maneno Hayo Kwani Japo Yanachekesha Na Hata Kustaajabisha Lakini Yanachoma Sana Hadi Kumoyo na Hugusa Mno Hisia Za Mtu.

Hebu Kama Na Wewe Unayajua Mengine Hebu Tupia Hapa Nizidi Kuongeza Siku Za Kuishi Kwa Kuvunja Mbavu Lakini Pia Nipate Ujumbe................... Karibuni Wadau na Wakuu Wangu Wana JF.

Kuna bajaji moja imeandikwa "wenye huruma hawafanikiwi" Nilitafakari sana sikupata majibu.
 
2.jpg


Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).

- Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
- Ukicheka na nyani utakula mabua.
- Hata ukioga, mjini huendi.
- Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
- Akikua ataacha!
- Hata kwetu wapo.
- Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
- Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
- Jino moja mswaki wa nini?
- Swali kabla hujaswaliwa.
- Dume kwenye mfuko wa nyuma?
- Usivue viatu kuna mbigiri.
- Changanya na zako!!!
- Unga robo, usicheze mbali.
- Butua uwakomboe wenzako.
- Si ulisema tamu, unalia nini?

Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.

nafsi ya mtu ni mtu mwenyewe
 
Back
Top Bottom