Mirathi inanitoa Roho

Strawberry

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
274
108
Habari wana Jukwaa.Mimi ni mwanamke wa umri wa miaka 32.nilifiwa na mme wangu sasa ni miezi sita toka afariki.
Alifia hapa DSM na kuzikwa kijijini kwao huko mkoa flani sitaki kuutaja jina kwa kuhofia usalama wangu.
Aliumwa nikauguza na akanifia mie mwenyewe.Tumejenga Nyumba moja na tuna shamba.Tulifunga ndoa ya kanisani.

Tatizo linakuja kwenye kufungua mirathi ya mme wangu.Maana alikuwa mtumishi wa serikalini.
Shemeji zangu wanataka mirathi tufungulie kijijini kwao.na mie nataka tufungulie hapa DSM maana ndipo tunapoishi na kujenga tumejenga hapa na kufia kafia hapa pia cheti cha kifo kinaonesha kafia hapa DSM.

Hawa shemeji zangu hawana nia njema na mie maana tayari wameshaanza chokochoko za kutaka kunitoa kwenye nyumba niliyojenga na marehemu mme wangu.Kwa kisingizio ipangishwe ili watoto wapate ada ya shule.
Tulifanikiwa kukaa kikao cha kuteua misimamizi wa mirathi mwaka jana Dec na wakaniteua mie nikisaidiwa na shemeji yangu.ila kwa ugomvi mkubwa sana walitaka wao wawe wasimamizi.
Mwisho wasiku tukaafikiana na wao kazikatalia zile karatasi za kuteua msimamizi wa mirathi wakazipeleka weyewe mahakamani bila mimi kunishirikisha.Hakimu akawarudisha akaaambia waje adi mie niwepo.

Basi wapendwa naomba msaada kwa yeyote anae jua wapi nianzie ili niweze kufanikisha kufungua mirathi huku hata kama ni shirika au taasisi yeyote inayoweza kunisimamia kwa hilo.
 
Pole sana mpendwa.

Hao mashemeji ni walafi na wana tamaa za mali. Zinawahusu? Wewe simama katika sheria utashinda.

Pili usisahau kumuomba Mungu akutangulie.

Katika hiyo ishu ya miradhi, pia washirikishe ndugu zako kama kaka mkubwa akuwakilishe. Usisimame mwenyewe. Tunakuombea ushinde mpendwa.
 
Ukisikia mashemeji njaa ndo hao. Kwanin usikauke? Yan wew ishi na maisha yako kana kwamba hakuna kinachoendelea? Kama mumeo amefariki inamana undugu nao umeshakufa automatically, hakuna kinachowaunganisha tena.

Kausha mama ishi kivyakovyako tu

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
logo3jpg.jpg
 
Nenda tamwa utapata msaada na namna ya kuwaelewesha hao shemeji zako bila misuguano.maana ukumbuku wao ndio baba wa watoto kwa hio usiweke misuguano, tamwa will help you vizuuurii tuu




habari wana jukwaa.mimi ni mwanamke wa umri wa miaka 32.nilifiwa na mme wangu sasa ni miezi sita toka afariki.
Alifia hapa dsm na kuzikwa kijijini kwao huko mkoa flani sitaki kuutaja jina kwa kuhofia usalama wangu.
Aliumwa nikauguza na akanifia mie mwenyewe.tumejenga nyumba moja na tuna shamba.tulifunga ndoa ya kanisani.

Tatizo linakuja kwenye kufungua mirathi ya mme wangu.maana alikuwa mtumishi wa serikalini.
Shemeji zangu wanataka mirathi tufungulie kijijini kwao.na mie nataka tufungulie hapa dsm maana ndipo tunapoishi na kujenga tumejenga hapa na kufia kafia hapa pia cheti cha kifo kinaonesha kafia hapa dsm.

Hawa shemeji zangu hawana nia njema na mie maana tayari wameshaanza chokochoko za kutaka kunitoa kwenye nyumba niliyojenga na marehemu mme wangu.kwa kisingizio ipangishwe ili watoto wapate ada ya shule.
Tulifanikiwa kukaa kikao cha kuteua misimamizi wa mirathi mwaka jana dec na wakaniteua mie nikisaidiwa na shemeji yangu.ila kwa ugomvi mkubwa sana walitaka wao wawe wasimamizi.
Mwisho wasiku tukaafikiana na wao kazikatalia zile karatasi za kuteua msimamizi wa mirathi wakazipeleka weyewe mahakamani bila mimi kunishirikisha.hakimu akawarudisha akaaambia waje adi mie niwepo.

Basi wapendwa naomba msaada kwa yeyote anae jua wapi nianzie ili niweze kufanikisha kufungua mirathi huku hata kama ni shirika au taasisi yeyote inayoweza kunisimamia kwa hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom