Mimi baba wa watoto watatu ratiba yangu ya asubuhi na jioni

RATIBA YA ASUBUHI
  • Naamka saa 11 au 12 kutegemeana na shughuli za siku.
  • Nikiamka saa 11 ujue na shughuli na mama yoyo.
  • Nikiamka saa 12 cha kwanza nachukua nguo za watoto( wawili wanafunzi) na zangu na kuzinyoosha.
  • Muda huo wife anakuwa anapambana na kuwaogesha. Akimaliza kuwaogesha nampokea kuwapaka mafuta na kuwavalisha ( muda huo wife anakuwa anawapikia breakfast).
  • Baada ya hapo naenza kujiandaa mwenyewe kwa ajili ya kwenda kwenye miangaiko. Asubuhi huwa natoka nao hadi kwenye kituo ambacho huwa wanachukuliwa na school bus.
  • Wakishachukuliwa mm ndo huwa naenda kutafuta usafiri wa kwenda kwenye mihangaiko yangu.

RATIBA YA JIONI
  • Huwa najitahidi by saa 11 niwe home.
  • Nakuta watoto wamerudi muda si mrefu, so naoga then naanza fanya nao home work.
  • Wakamimaliza homework natafuta kinywaji changu pendwa na kuanza kusip nikisubr msosi wa usiku..
  • Wadau kwa ratiba yangu hii nyie mnaionaje, ratiba yako wewe ipoje?
Kwanini kila siku urudi sa 11 usipitie hata Bar mara mojamoja uongeze akili hadi angalau saa tatu hivi
 
Mimi:
Naamka saa 9 au 10 alfajiri. Nasali hadi saa 11 au 11:30. Naanza fanya kazi zangu kwenye Laptop kuanzia saa 11:30 alfajiri hadi saa 1:30 Alfajiri.

Saa 1:30 hadi 1:45 ni kuoga na kujiandaa kwenda Kazini. Saa 9:30 alasiri narudi toka Kazini. Naenda Shambani au kuangalia mifugo hadi saa 12:45 au saa 1:00 Usiku.

Hiyo saa 1:00 nitaoga na kufanya kazi kidogo kwenye laptop huku naingia mtandaoni na saa 2:00-3:00 usiku nakula Msosi huku naangalia taarifa ya habari. Saa 3:00 naingia kusali then saa 3:30 au 4:00 Nalala.

Ni Baba wa watoto 4, siwaogeshi wala wafulia wala shughulika nao. Mama yao na dada yao wanafanya hayo.
 
5.6 year almost Six years, four years na 2years
Kwanza hongera kwa kuwa karibu na familia,na kuweza kujenga upendo na ushirikiano na mkeo katika kuhudumia watoto.

Kama itakupendeza,waanze pia kufundisha kujifanyia vitu wao wenyewe,kama kuvaa,kuchana nywele,kupaka mafuta,hata kuoga,itawajenga zaidi.Kuliko kuwafanyia kila kitu.

Japo ni kama ina ugumu zaidi kuliko kuwafanyia.
 
Kwanini kila siku urudi sa 11 usipitie hata Bar mara mojamoja uongeze akili hadi angalau saa tatu hivi
ana kazi yenye heshima ktk jamii hivyo basi haitaji kwenda bar wala vijiweni kuboost self esteem pia jamaa ni introvert kinywaji ananywea nyumbani alafu ni mtu anayependa kufanya jambo moja kwa moyo wote hapend kujaribu kitu kingine ndo maana hujaona biashara wala mchepuko kwenye daily routine yake
 
Huyu asije kusumbua huko baadae kwa kuanza kufanya vitu alotakiwa kuvifanya ujanani
 
RATIBA YA ASUBUHI
  • Naamka saa 11 au 12 kutegemeana na shughuli za siku.
  • Nikiamka saa 11 ujue na shughuli na mama yoyo.
  • Nikiamka saa 12 cha kwanza nachukua nguo za watoto( wawili wanafunzi) na zangu na kuzinyoosha.
  • Muda huo wife anakuwa anapambana na kuwaogesha. Akimaliza kuwaogesha nampokea kuwapaka mafuta na kuwavalisha ( muda huo wife anakuwa anawapikia breakfast).
  • Baada ya hapo naenza kujiandaa mwenyewe kwa ajili ya kwenda kwenye miangaiko. Asubuhi huwa natoka nao hadi kwenye kituo ambacho huwa wanachukuliwa na school bus.
  • Wakishachukuliwa mm ndo huwa naenda kutafuta usafiri wa kwenda kwenye mihangaiko yangu.

RATIBA YA JIONI
  • Huwa najitahidi by saa 11 niwe home.
  • Nakuta watoto wamerudi muda si mrefu, so naoga then naanza fanya nao home work.
  • Wakamimaliza homework natafuta kinywaji changu pendwa na kuanza kusip nikisubr msosi wa usiku..
  • Wadau kwa ratiba yangu hii nyie mnaionaje, ratiba yako wewe ipoje?
Mimi ni kijana mdogo wa miaka 38 na mwanachama wa CCM, ninaahidi nikioa nitakuwa na ratiba inayoshahibiana na hii yako. Nitatumia muda mwingi na familia kadiri iwezekanavyo. Ee Mwenyezi Mungu nisaidie.
 
Back
Top Bottom