Mikingamo ya Misemo ya Mapenzi...........

Hahahah Eti swali linaulizaje! we Soulmate wewe!
Kwa tafsiri hii ninaamini napendwa teh teh teh:becky:

Haya bana mkishakutana na Babu DC siwawezi, ninaombea asiuone mjadala huu maana atanipin kwenye angle hadi nikome mwenyewe.

Hapo kwenye upendo vs mapenzi ndipo ninapojaribu sana kupaelewa ingawa mwe! Nahisi nahitaji external energy kuielewa

.....lol, ati "unahitaji external energy
" kuielewa....ngojea siku (ombea mungu isikutokee) utapopoteza Upendo uliotunukiwa na kubakiwa na penzi pekee...-'hutajua thamani ya kitu mpaka ukipoteze'-

By the way, napatwa na hisia kwa haya maswali yako ewe Soulmate maishani mwako hujawahi kuishi kwenye Upendo,..bali. umekuwa unaishi kwenye Mapenzi pekee, ndio maana wataabishwa na hali iliyopo...:D
 
Mbu,unachosema ni kweli kabisa,wengi wanaishi kwenye mapenzi sio upendo,lakini balaa kubwa watu wanazungumzia mapenzi na kutafuta mapenzi badala ya upendo.Ukiupata upendo unakua uko kwenye kiwango cha juu kabisa cha maisha na furaha!
 
Wanadamu ni wanafiki,sio wakweli.Mwanadamu anataka mazuri lakini hataki kuwajibika kuyatenda.Ni rahisi kusikia nataka mke/mume mwenye upendo wa kweli nitaridhika.Mwisho wa siku anaanza kuangalia mwili hela na ujinga mwingine mwingi,mwisho wa siku hakuna kinachoendelea.Umezungumzia upendo,let me tell u,hakuna anaejua maana ya upendo,ukiujua yote mengine hayana maana!

....Eiyer bana, take a deep breath....duniani hapa kuna Optimists na pessimists. Ili uweze kuishi kwa furaha na amani, jifanye 'kinyonga'....be flexible and adaptable...

....penye Mapenzi kuna kutaka na kutamani. Penye upendo kuna kuridhika na kukinai.... Unaposema hakuna ajuaye maana ya upendo,.... dahh? ...ndio yale ya kusema 'a glass is neither empty or full!'...

.....mwanajamiiOne hapa amechanganyikiwa, hajitambui anapenda/anapendwa kimapenzi (au ki Upendo?)...- kwenye mabano anamtafsiri Soulmate wake na sentensi "... love is a game!" (Enjoy it!)....live the fun of it....
 
Mbu,ninaposema hatujui upendo namaana ya KUTOKUJUA.Nayachukia maisha ya kuwa kama kinyonga.Siyapendi kwa sababu unalazimika uwe na mambo fake na pengine usiyoyapenda.Mbu,kwenye upendo hakuna kukinai kuna kujua na kuridhika.Unajua unatoa upendo na unaridhika kwa sababu unajua kupenda.Penye upendo kuna raha hakuna majuto na kujilaumu!
 
.....lol, ati "unahitaji external energy
" kuielewa....ngojea siku (ombea mungu isikutokee) utapopoteza Upendo uliotunukiwa na kubakiwa na penzi pekee...-'hutajua thamani ya kitu mpaka ukipoteze'-

By the way, napatwa na hisia kwa haya maswali yako ewe Soulmate maishani mwako hujawahi kuishi kwenye Upendo,..bali. umekuwa unaishi kwenye Mapenzi pekee, ndio maana wataabishwa na hali iliyopo...:D

Soulmate bana, huwenda ikawa kweli ingawa ninawiwa kuamini kuwa ni kweli. Unajua mie ninaposhindwa kuelewa kwa nini isiwe rahisi kumsamehe mtu unayeona amekukosea (pale unapokuwa bado hujakinaiwa na matendo yake na kuamua kubwaga manyanga) katika ile ya Love is blind yaani kila kosa we waona linasamaheka as long as you are still in love?

Pengine nimmewahikuwa kiupendo zaidi but nikawa mapendwa kimapenzi ati!

Hebu nitafsirie qualities/characteristics za upendo na mapenzi Mbu.
 
Mbu,ninaposema hatujui upendo namaana ya KUTOKUJUA.Nayachukia maisha ya kuwa kama kinyonga.Siyapendi kwa sababu unalazimika uwe na mambo fake na pengine usiyoyapenda.Mbu,kwenye upendo hakuna kukinai kuna kujua na kuridhika.Unajua unatoa upendo na unaridhika kwa sababu unajua kupenda.Penye upendo kuna raha hakuna majuto na kujilaumu!
Eiyer mpaka hapa ndugu yangu tupo ukurasa mmoja, how can someone live maisha ya ukinyonga kwa ampendaye? unless hampendi bali anaplay the game kama anavyosema Mbu
 
Mbu,ninaposema hatujui upendo namaana ya KUTOKUJUA.Nayachukia maisha ya kuwa kama kinyonga.Siyapendi kwa sababu unalazimika uwe na mambo fake na pengine usiyoyapenda.Mbu,kwenye upendo hakuna kukinai kuna kujua na kuridhika.Unajua unatoa upendo na unaridhika kwa sababu unajua kupenda.Penye upendo kuna raha hakuna majuto na kujilaumu!

.....zote hizo ni tafsiri ya Upendo, na zinakubalika. 'Ukinyonga' ni sehemu ya maturity....compromising....uking'ang'ana na 'umimi' (being Rigid and selfish) kwenye mahusiano -utayapelekea maisha ya mwenza wako aishi kama "msukule" mtumwa wa mapenzi. Yaani usemalo wewe ndio Amri!

Wk'end nilikuwa na Soulmate twatazama movie ya 14 Days....JB & Wema Sepetu. Script nzuri, japo ni copy & paste, lakini ni funzo tosha ukiamua kuiangalia movie hiyo kimtazamo wa kisaikolojia (impacts) zaidi...

Be adaptable, it costs you nothing to be humble kwa yule umpendaye.
 
...................Eh 14 Days, I love that movie ingawa mara ya kwanza nilikuwa ninaiangalia kwa jicho la kawaida la kuangalizia movie, but baada ya ku'funuliwa' a lot of lessons can be drawn from that movie aisee Soulmate, Mbu. Aksante kwa kutukumbusha.
Nakumbuka (kama sijachanganya) kuna kipande yule rafiki wa JB (Adam Kuambiana) Wile (Willy) alifananisha ndoa na chumvi na pilipili (Chill) za mezani, kuwa kwa mtazamo wa mapenzi, chumvi na pilipili havikai pamoja but kwa mtazamo wa Upendo, chumvi haiendi bila pilipili (kwa mlaji) pamoja na kuwa vina ladha na rangi tofauti.
 
Mbu,kuwa wewe kwenye mahusiano sio umimi,umimi ni mama wa dikteta.Kuwa wewe kuna maana kuishi maisha halisi na sio fake!Unajiamini na unakua wewe,huwezi kwenda kuazima nguo fulani uvae ili fulani avutike nawe.Huu na wendawazimu,atakua amevutika na mtu fake!
 
Mapenzi hayafundishiki wala hayafunzwi. Mapenzi ni mchezo asilia wa moyo kutoa na kuingiza hisia...
 
''mapenzi ni kama upepo...huuoni bali una u feel" kama hivyo kwanini unasema flani ananipenda wakati love haiyonekani.ni maneno mbofu bofu tu hii
 
"Love is a matter of Chemistry. Sex is a matter of Physics"
Erotica! Nimeipenda hiyo. Kuna Bidada kule majuu ilichagua PHYSICS (kwa miaka 9 ilitembea na nyamaume 5000) watu humu Jamvini wameilaani ile mbaya.

Ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
MwanajamiiOne! Unazungumzia upendo upi? hebu angalia hapa halafu unijuze.

Tunaweza kupata ufahamu wa ndani wa neno UPENDO kutokana na maneno ya awali (ya Kiyunani) yaliyotafsiriwa "Upendo" katika Biblia (ya Kiswahili). Neno UPENDO linatokana na kutafsiri maneno manne (ndio aina nne za upendo) ya Kigiriki cha mwanzo/awali.

Maneno hayo ni;
·PHI·LE´O
·STOR·GE´
·
E´ROS
·
A·GA´PE

PHILEO: Kitenzi kinachomaanisha kuwa na shauku, kuthamini au kupenda (kama mtu anavyompenda rafiki wa karibu au ndugu). Hutumika mara nyingi katika Agano Jipya baada ya neno Agape.

STORGE: Upendo ulio kati ya watu wa familia moja. Huu ndio upendo ambao Paulo mtume alisema una/utakuwa haba katika siku za mwisho (2Tim 3:3).

EROS: Upendo wa kimahaba kati ya watu wa jinsi tofauti. Upendo huu hautajwi katika Agano Jipya bali katika Agano la Kale (Mith 5:15-20).

AGAPE: Upendo unaoongozwa na kanuni na unatia ndani mambo mengi; unahusisha fikira na una kusudi fulani na hauna ubinafsi. Upendo huu sio hisia tunayokuwa nayo bila kufikiri. Mara nyingi huhusisha uhusiano wa karibu wenye upendo. Agape ndilo neno linaloelezea Upendo kwa njia nzuri zaidi. Aidha kati ya maneno hayo yote kuhusu Upendo; Agape limetumika mara nyingi zaidi katika Agano Jipya.
 
Back
Top Bottom