Mikataba kabla ya kufunga ndoa; Prenuptials TZ huwa ipo?

Futota

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
521
87
Hivi kwa bongo hii mikataba huwa ipo? kama ndio huwa inatumika katika kesi za kugawana mali wakati wa kuachana (divorce)?
Kwa sababu kama mwanamke aliolewa na urithi wake wa let say, nyumba zenye hati, sasa akiachana na mumewe, halafu mumewe akataka wagawane na hizo mali zake pia. kesi kama hii mwanamke utafanya nini, maana sijawahi kusikia haya mambo ya prenuptial bongo.
 
Ibara ya 58 ya sheria ya ndoa ya 1971 inasema ( 1 ) inaruhusu makubaliano binafsi kuhusu umiliki wa mali kwa wanandoa na pia inaainisha kuwa ndoa isikuzuie kuwa na chako binafsi.

"Isipokuwa kama kuna makubaliono binafsi ambayo wana ndoa wamefanya basi ndoa isiwe sababu ya mke au mume kupoteza umiliki wa mali yake au kumzuia asimiliki au asishikilie mali kivyake, au kuuza mali yake."
 
Ibara ya 58 ya sheria ya ndoa ya 1971 inasema ( 1 ) inaruhusu makubaliano binafsi kuhusu umiliki wa mali kwa wanandoa na pia inaainisha kuwa ndoa isikuzuie kuwa na chako binafsi.

"Isipokuwa kama kuna makubaliono binafsi ambayo wana ndoa wamefanya basi ndoa isiwe sababu ya mke au mume kupoteza umiliki wa mali yake au kumzuia asimiliki au asishikilie mali kivyake, au kuuza mali
yake."

Asante kwa kujibu mkuu, naanza kuelimika
 
Mikataba yote tangu uchumba iko covered kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Kuhusu mali kabla ya ndoa Mke/mume ataziandikisha kama mali binafsi za mwanandoa husika na ndoa ikivunjika zinabaki ni za mwanandoa husika.

Ila pia mwanandoa anaruhusiwa kuziandikisha kama mali za ndoa au hata kuzitoa kama zawadi kwa mwanandoa mwenzake.

Sheria hiyo inamtambua mume kama ndio mtafutaji, ndoa ikivunjika mali zinazogawanywa ni za mume tuu hata kama mke ana mali zake na mume huwajibika kutoa matunzo kwa mkewe na watoto hata kama mke ana kazi nzuri na anaweza kijitunza.
 
ndoa ikivunjika mali zinazogawanywa ni za mume tuu hata kama mke ana mali zake
Umetoa wapi hicho kitu wewe Pasco?!

Hebu stick kwenye journalism bana, ndo maana dhamira yako ilikwambia uachane na legal profession, huna wito huko! Umeshatamka mwenyewe mwazoni kwamba "Mke/mume ataziandikisha kama mali binafsi za mwanandoa husika na ndoa ikivunjika zinabaki ni za mwanandoa husika" halafu unakuja tena unaongeza kituko kwamba "ndoa ikivunjika mali zinazogawanywa ni za mume tuu..."

Mke/mume ataziandikisha kama mali binafsi za mwanandoa husika na ndoa ikivunjika zinabaki ni za mwanandoa husika.

Huoni hapo kwamba unajipinga pinga mwenyewe, hivi wanasheria wa kibongo mna matatizo gani jamani? Eeh?

Sheria inasema mali ya mtu, awe mwanamke awe mwanamme, kama hujachangia, cha mwenzio si chako! Mkiachana hakigawanywi!

Power of court to order division of matrimonial assets, CAP 29 of Laws, 5-1971

114.-(1) The court shall have power, when granting or subsequent to the grant of a decree of separation or divorce, to order the division between the parties of any assets acquired by them during the marriage by their joint efforts or to order the sale of any such asset and the division between the parties of the proceeds of sale.

(2) In exercising the power conferred by subsection (1), the court shall have regard: ...(b) to the extent of the contributions made by each party by money, property or work towards the acquiring of the assets...

(3) For the purposes of this section, references to assets acquired during a marriage include assets owned before the marriage by one party which have been substantially improved during the marriage by the other party or by their joint efforts
.


Watu wote tunaotoa zawadi kwenye harusi, au wafungisha ndoa, ma Sheikh, Pastor, Mkuu wa Wilaya naombeni jamani muwe mnagawa nakala ya Sheria ya Ndoa ya 1971 kwa newly weds, badala ya kuwapa vitenge na tenzi za rohoni na kanzu!
 
Wakuu, Taso na Pasco, naona sasa kabisa mmenichanganya hapa, which is which?
Labda nitoe mfano, mke aliolewa tayari anamiliki nyumba yenye hati, wakiwa kwenye ndoa wakajenga nyumba na hati ikaandikwa jina la mume pekee, pia wanalo gari na card ya gari ina jina la mume pekee. Sasa wakiachana, for sure mke ataondoka na nyumba yake. sasa ile ya pamoja yenye jina la mume na gari, hizo mali 2 kisheria si itabidi wagawane? au hapa mume atachukua vyote?
 
Ndoa hufungwa rohoni tu, lakini sheria za Tanzania ni kama wimbo wa kigeugeu

Hapa sijakuelewa Mkuu, ndoa hufungwa either kanisani, msikitini, bomani au kimila. Labda hauamini kama taratibu hizi za ndoa zinafuatwa au hizifuatwi, ila ninaamini kila kinachofanywa ktk ndoa ni utaratibu ambao sheria za nchi hutambua, kwa upande wako huwezi kufahamu kama mambo yanayotendeka ktk masuala ya ndoa ni taratibu za kisheria au ni mazoea tu. Angalia sheria ya Ndoa, Na. 5 ya 1971 (Sura ya 29 R.E 2002) itakuonyesha namna ambavyo masuala ya ndoa yanavyoendeshwa kwa mujibu wa sheria hiyo, na tatizo linakuja pale ambapo watu wengi hawafahamu taratibu za kisheria zinazoongoza ndoa yao.
 
Back
Top Bottom