LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 457
- 1,746
Nahodha akanipigia kelele kwa sauti kwamba nizame chini kwamba mwenzangu amechoka niende kumsaidia na kweli nilivo mtazama alikuwa akiniita kwamba niende,
Naam natumaini humu wote hamjambo humu pia niwashukuru hawa jamiifurm kwa kuendelea kupeperusha nyuzi zetu hewani
Tukianza moja kwa moja kuhusu mambo yaliyonikuta nikiwa nafanya kazi za baharini
Nakumbuka nilipofika kwa mara ya kwabza msasani beach nilikuwa sijui hata kuogelea ila nilianza kujifunza kwa kujifunga chupa za maji ya lita moja na nusu miguuni na mikononi mpaka nikawa nimejua kuogelea kabisa, sasa tukianza na mkasa wa kwanza,
Siku hiyo tulienda kuvua uvuvi wa kuzamia chini au wanaita kokoro yaani hiyo nyavu huwa ikisha zungushwa kweny maji chini huwa haiachi kitu, sasa tukisha tupa nyavu chini ile nyavu inakuwa na kamba kwa bande mbili wakati tunaanza kuidondosha tubapoanzia kuidondoshea tunaacha alama ya boya tunaweza izungusha raundi kama kilometa moja hivi mpaka tunakutana tena na lile boya tunakuwa wastani wa watu kuanzia 12,
Sasa tunachukua lile boya tunalivuta mpaka tunaishika ile kamba tunaanza kuvuta kila upande halafu kuna watu wanajitosa majini wanaenda mpaka kule katikati kwenye nyavu wanakuwa wanatuelekeza ili kuivuta kwa usawa,
Pia kwaajili ya kuitoa inapotokea imenasa kwenye mawe maana ile kamba huwa ina zama chini kabisa ardhini ili kuwastua wale samaki hasa pono kukimbilia katikati,
Na inapo karibia karibu na boti tunashuka kwenye maji watu watatu au wanne ili kuwazuia wale samaki warudi kwenye nyavu, na pale katikati ya nyavu huwa tumeitoboa na kushonea likitu kama mfuki hivi, ambapo tundu lake limerudi kwa nyuma kama shimo,
Sasa siku hiyo nahodha akaniambia nishuke kwenye maji ili tukawazuie samaki tulivoshuka mtu 3 tuaenda wakwanza akaenda chini akawazuia wakati sisi huku juu tumevaa vioo vya kutazama na tunamtazama akikaribia kuishiwa pumzi anatuita kwa ishara sasa alivoita yule mwenzangu akaenda,
Pia na yeye alivochoka akaniita muda huo huko juu ya boti wanakazana kuvuta nyavu kwa kasi sana,
Nikazama chini yeye akapanda juu nikawa nawazuia samaki walikuwa wengi tu wakawa wanakimbilia kwenye hilo shimo nilivoona nimechoka nikamuita jamaa aje nikapanda juu kutema mate hivi nikashangaa natema damu, kwakweli hiyo ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuzamia kina kirefu hivo nahodha akanimbia nirudi tena kule chini ili tukawafungie hao samaki nikawa tu nimeshikilia kulikuwa na boya ambalo huwa linafanya nyavu isimame,
Kutazama chini jamaa ananiita niende aaa wapi ikawa ngumu muda wote huo bado natema damu tu nilipatwa na hofu sana japo tulifanikiwa mzigo ukawa umepanda juu, mimi ndo nilikuwa mdogo kuliko wote humo japo nahodha alikuwa ananielewa sana,
Lakini sikumwambia mtu yoyote kilicho tokea nashukuru mungu alinisaidia ila ndo ikawa mwanzo na mwisho kuzama kina kirefu hivo,
Ipo mikasa mingi ila nimmeanza na huoo ipo mingine ikiwemo
Kuvua samaki wengi mpaka tukawamwaga wengine maana tungezama
Kutumia siku mbili kutoka msasani mpaka bandarini tukiwa tumevuta chuma la kujengea madaraja lipo kama box mpaka kupata ajali ya kugongana na boti la kubeba mzigo
Kupinduka bongoyo na msanii mwigizaji lucy komba
Tuishie hapo kwanza