Miezi sita watu wanapambana na kivuli cha Diamond, sasa kakirudia kiti chake inabidi wawe wapole

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,518
34,913
Diamond amejijenga Sana kimziki Hilo halina ubishi, inawezekana kuna mapungufu pia , hata hvyo katengeneza team work yenye nguvu Sana ,....

Kwa sku za hvi karibuni kapigiwa kelele Sana negatively, kelele hzo hazijaathir chochote career ya mshikaj , Sana Sana zimempa hipe kubwa Zaid, .... , kila msanii akitoa kazi anajipima Kwa Diamond , hyo kitu inampa mileage kubwa Sana mshikaji , kibaya zaidi anajua kutumia fursa , hvyo malengo ya haters kutimia itachukua mda kidog......

Jamaa miez sita bila wimbo lakni alikuwa na backup yenye nguvu Kias kwamba platform yake haikutetereka , Yani Kwa mda wa miez sita watu walikuwa wanapambana na kivuli cha mshikaji , huku Zuchu , huku Rayvanny, huku Mbosso, pembeni Lava lava , huku kukiwa na drama za hapa na pale yote hayo yalihitimishwa Kwa kumhusisha Diamond , hvyo wakat yupo kimya bado kaz zake zilitambaa ...

Machawa wenye chuki walitafta, wametafta na wanaendelea kutafta kuongea kwenye vyombo vya habar lengo kumuongelea mshikaji na kumtukana , dharau na kila aina ya fitina , lakini imeonekana kama wanatwanga maji kwenye kinu..!!

Mwisho wameanza kushauriana Tu sasa kwamba wapeane Tyme ya kuachia nyimbo mana msuli wao mdogo kumkabili Simba wa Tandale ... Majadiliano hayo yameishia kwenye kutupwa nje ya kinyang'nyiro mmakonde huku wimbo wake ukifutwa YouTube...

Tukumbuke tunapomtukana jamaa na kumuita mshamba tujue mwamba kaishia form two sjui form four , akiwa na ukwasi wa kuridhisha, Sisi wengine tupo na degree zetu maeneo ya Ikunguilipu tukiwakaririsha watoto Archimedes principle ... , Achilia mbali kulipwa posho ya laki tatu Kwa mwezi Kwa wale waliojishikiza mjini na vikazi vya hapa na pale...Huku tukimlilia mama Samia atuletee Tanzania mpya ambayo haipo na haitakuja kuwepo kamwe
 
Slowly baada ya kutoka ofiaini kwake instagram..
FB_IMG_16247412102700368.jpg
 
Ila tuache uongo hii Kamata ni takataka huwezi kulinganisha na Salute💂👮‍♂️
Sasa mkuu ulitaka nyimbo zote ziwe htsong Mzee , subir albam utaokoteleza size yako boss
 
Back
Top Bottom