Viongozi wenu zeroHakuna zero brain anayeweza kuongoza mwenye akili. Ukiona Zero brain anakuongoza ujue yeye ana akili kukuzidi. Ushaona wapi ng'ombe akichunga kundi la masai?
Wasomi wa vyetiKi ukweli, ni shida sana tena sana.
Misri wanatumia maji ya mto Nile ambao chanzo chake ni Ziwa Victoria, wakati huo sisi tumekaa kama wajinga fulani hivi.
Hata mimi huwa najiuliza, ni kwa nini Tanzania ina wasomi wengi mpaka sasa lakini sioni kama wanatusaidia kutatua changamoto zinazotukabili katika jamii. Inauma sana.
Kabisa liondoe lote kizaz cha bongo flevaKuna mda huwa nawaza ingewezekana basi sijui kingekuja kitu gani kikatuondoa wote within a second! Labda wangekuja wenye akili wakafanya mambo makubwa.
Wacha mambo yawe magumu labda akili zitakuja. Kutwa kulalamika bila kuchukua hatua. Tena tukiishia kulalamika ndiowanafurahi ili waendelee kututawala vizuriDu, umenikumbusha juzi tu hapo natembea kwa mguu kijiji Fulani ambacho kipo main road tu kwa mbaali naona kama kunakundi la watu na vitu vya rangi ya njano. Wakati huo kulikuwa na mtu ambaye alikuwa anatembea sambamba na Mimi lkn Kila mtu alikuwa bize na safari yake. Sasa kadri nilivyokuwa na karibia lile kundi la watu ndio nagundua walikuwa kwenye foleni ya kuchota maji na vile vitu vya njano nilivyokuwa naviona ilkuwa madumu ya maji. Kwa wastani palikuwa na watu wasiopungua 200 hv na madumu labda 1500. Nilijikuta nimesema mwenyewe hii nchi tunaonewa sana mpk yule mwenzangu niliyekuwa natembea nae sambamba akasikia na kujikuta tunaendelea mazungumzo. Yule mwenzangu akasema bro usione hvyo watu wapo hapo tokea saa 11 asubh na huenda wengine wakakosa maji kwa sababu ni ya mgao na huwezi amini ni zaidi ya mwezi mmoja ndio maji yametoka leo. Tulizidi kuongea mengi lkn nikagundua maji yalitekwa kutoka kwenye chanzo ambacho sio cha uhakika lakini nachojua umbali km kilometer 40 kunachanzo cha uhakika kabisa cha maji nikamuuliza mshikaji kwann wasingetua chanzo hicho cha uhakika cha maji, nilichojibiwa ilisemekana Kule n mbali so gharama ingekuwa kubwa kulinganisha na fedha waliyobajetiwa. Ghafla na pigwa na kitu kizito kichwa I( nasikia king'ora) ni msafara wa walamba asali 🤔🤔☹️☹️ aiseeeee ule msafara ulikuwa na gari kama 15 hv, nikajiuliza hapo ni mtu mmoja mlamba asali anasindikizwa alafu mamia ya watu wapo foleni ya maji tokea alfajiri. Tusichoke tutafika tu japo tukiwa hoi.
Kipindi cha nyuma ulimpendaNa liraisi limekaa kimyaa siku hizi simpendi mama Samia
Na liraisi limekaa kimyaa siku hizi simpendi mama Samia
Upo sahihi mkuu,ngozi nyeusi popote alipo,hapa Afrika au diaspora,kichwani Kuna matatizo.Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane.
Huwa ninajaribu kuitazama Afrika(Bara)na watu waishio humo ndani hasa ngozi nyeusi nabaki kupata sintofahamu! Mimi ni mkristo na nina amini ya kwamba Mwanadamu ameumbwa na Mungu. Sasa huwa napata taabu sana kuona kwanini sisi waafrika tupo tofauti na jamii nyingine hasa weupe!. Utofauti ninao usema hapa ni kuhusu - MAAMUZI, AKILI, UTENDAJI na UTEKELEZAJI WA MAMBO.
Leo nitajikita zaidi kwa jamii hii ya watu weusi wapatikanao Tanzania.
Kadiri miaka inavyozidi kusogea na teknolojia ikiongezeka kwa kasi,ndivyo jamii hii ya watu weusi wakaao Tanzania ni kama AKILI nazo zinazidi kupungua kwenye vichwa vya watu!.
Dubai ni nchi ndogo sana ambayo ni muunganiko wa zile nchi zinazounda jumuia ya falme za kiarabu (Emirates), kiasili Dubai ni Jangwa lakini wanamaji ya uhakika masaa 24, siku 7, miezi 12 na miaka yote!
Naomba hapa niongeze sauti ili walioko baki bencha wasikie vizuri!.
"Dubai kiasili ni jangwa lakini wao kuhusu tatizo la maji wamebaki kulisoma kwenye vitabu na kuliona kwenye taarifa za habari ambazo nyingi huwa zinahusu Afrika"
Tanzania ambayo inakila kitu cha asili na iliyozungukwa na Maziwa makubwa,mito mikubwa,bahari na mabwawa ya kila aina lakini bado wananchi wake wanaendelea kuteseka kuhusu maji.
Hii ngozi sijajua aliyetuachia laana ambayo haifutiki milele zote ni nani! Je ni kwamba hatuna akili? Hili mbona kama nalikataa! Hivi ndugu zangu ni kweli hatuna akili? Ni kitu gani kinachotusumbua sisi ngozi nyeusi?.
Sasa kila mmoja wetu hapa anafahamu kwasasa jiji la Dar es salaam na viunga vyake kuna mgao mkubwa wa maji na umeme, nadhani kwasasa siyo Dar es salaam pekee bila shaka ni nchi nzima!.
Dunia ya leo ya Sayansi na Teknolojia eti tunategemea maji ya mto Ruvu ndiyo yanyweshe mamilioni ya wakaazi wa Dar es salaam, hivi kweli tuko serious? Hivi ni nani aliyeturoga? Hivi tumemkosea nini Mungu mpaka kutuadhibu kiasi hiki? yaani Dubai ambayo iko jangwani wanapata maji kwa uhakika lakini siye tuliozungukwa na kila aina ya maji tunakosa maji?
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam bil hata kuona haya na aibu anakaa kabisa mbele ya watu anasema ndugu zangu "Tumuombe Mungu ili mvua zinyeshe!"
Aisee hadi nashindwa kuandika!.
Kwani wale waarabu waliweza vipi kubadili yale maji chumvi kuwa maji ya matumizi ya kawaida? gharama yake ni kubwa kiasi gani hadi sisi kama taifa tushindwe kuafodi? ina maana akili za viongozi wetu ndiyo zimefika mwisho!
Leo Karne ya 21 maji tu ni shida kwenye jiji kubwa kama Dar es salaam, je huko vijijini hali ikoje?
Wenzetu kadiri miaka inavyosonga wanapanuka kiakili lakini sisi ngozi nyeusi pamoja na kwenda shule ndiyo kama akili zinarudi nyuma!.
Tanzania ni mfano tu lakini nchi karibia zote za kiafrika matatizo hufanana!
Aisee kiukweli nina mengi moyoni lakini ngoja niishie hapa, hata kuandika sasa imeniwia vigumu!