Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,896
- 3,206
Labda bado anaweka fedha mifukoni mwa watu kama ambavyo aliwahi kujinasibu.Rais Samia ametimiza miaka 3 tangu achukue madaraka ya urais lakini ukilinganisha na miaka 3 ya hayati Magufuli akiwa madarakani ni kama mlima na kichuguu kwa matokeo.
Rais Samia amefanya semina nyingi kwa mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na wakuu wa mikoa lakini bado utendaji wa serikali yake uko duni sana! Matokeo baada ya semina hizo hayaonekani kabisa.
Rushwa, uzembe, mfumuko wa bei, kupandisha gharama za miradi, kuchelewesha miradi imekuwa ndiyo sifa kuu ya serikali ya Rais Samia.
Hayati Magufuli alijenga majengo ya wizara na kuhamishia serikali yote Dodoma ndani ya miaka 3 lakini Rais Samia kwa miaka 3 hakuna jengo hata moja lililokamilika kiasi cha kuanza kukaliwa na watu. Kwenye serikali ya Samia hamna mradi hata mmoja ulioanzishwa unaoweza kusema kwamba angalau hapa Kuna watu walikaa na kutumia akili.
Rais Samia amefanya vizuri sana kwenye ujenzi wa madarasa kwa kutumia mkopo wa fedha za Uviko.
Lakini kiukweli hali ya maisha ya siku hizi imekuwa changamoto sana. Ukienda dukani bei utakayoikuta asubuhi ni tofauti na utakayoikuta jioni, na kwa bahati mbaya vitu vinazidi kupanda tu bei na wala haijawahi kushuka toka aingie madarakani