Mheshimiwa Ndesamburo mbunge wa Moshi Mjini,tunaomba utusikie wana CHADEMA

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Wanajamvi Mbunge huyu anamiliki kituo cha Radio hapa Moshi mjini almaarufu kama MOSHI FM,Kituo hiki ni maarufu sana hapa Moshi mjini haswa ikifikia wakati wa shughuli za chama,kinatowa msaada mkubwa sana kwa matangazo na upashaji wa habari.

Kwa mawazo na ushauri yangu kwanini chama kisimwombe Mh,ndesamburo ili radio hii iwe ya chama na iongezewe nguvu haraka kabla ya mwaka 2013,Angalau isikike katika mikoa yote mikubwa hapa nchini ili kutangaza Demokrasia hapa nchini kabla ya mwaka 2015.

Tufanye kama tulivyofanya kwenye magari ya matangazo tuliyoyachukuwa kwa mwenyekiti wetu Mh.Mbowe na msaada wake ukaonekana wazi kwa chama japo kulikuwa na kelele nyingi toka kwa wana magamba,

Minaona kuanza mchakato wa kuanzisha Radio mpya itakigharimu chama muda mrefu na pengine tusifanikiwe kwa muda mwafaka,magamba na serikaliyao wanaweza kutuwekea kauzibe tisipewe kibali mapema na hata pengine tusipewe kabisa.

mnasemaje wenzangu?
 
Ni wazo zuri kamanda kesho itakua live mkutano wa mh.LEMA katika viwanja vya Railway kuanzia saa 8 mchana
 
Nafikiri chama bado hakijashindwa kufanya hilo, ila sijui wanasita nini, labda chama kitueleze kwa nini hakitaki kuanzisha redio na tv na kila siku kuendelea kuilalamikia tbccm, nafikiri kungekuwa na redio na chama ingekuwa vyema zaidi....kuigeuza redio ya ndesapesa iwe ya chama kuna athari kubwa sana kwa chama ndugu yangu hasa katika kipindi hiki, tuendelee kukilazimisha chadema walau ianze kujadili hili katika kamati kuu kwani kama tunaichangia m4c kwa nini tusichangie uchangiaji wa redio na tv chadema
 
ile ya St.Augustine ilifungwa kipindi cha kampeni na magamba kuwa inaingilia mitambo ya ndege?? hapo upo??
 
KASPERSKY ANT- CCM sina imani nawe. labda unampango wa kutuchafulia chedema yetu. redio ya chama itakuwa kwenye makao makuu ya chama. sidhani kama kuna makao makuu ya chadema pale keys kwa mzee wetu ndesa. wacha watu wenye uchungu na nchi hii watuchagulie pahala zitakapokuwa studio za redio yetu.
 
Ni muda muafaka sasa viongozi wa chama watueleze wana mpango gani na tv radio au gazeti kuliko hivi ,tena nawasifu sana itv kwa kutuonesha habari za m4c wengekuwa waoga tu tusingeona kitu
 
mbowe kashajenga kituo cha redio nyumbani kwake machame penye protea hotel.
Sijajua itajihusisha na nini kwani bado haijaanza kurusha matangazo ila kilakitu almost kipo tayari.
 
Wazo la CDM kuwa na Redio au Tv ni zuri, lakini kinachotakiwa ni umakini wa hali ya juu, kinatakiwa chombo ambacho hakitabase upande wowote ule kiwe kinatoa habari na sio ushabiki kama gazeti la Uhuru na TBCCM, kiwe ni kwa ajili ya Watanzania wote, na kuweza kukosolewa pale itakapohitajika. Asante nawakilisha.
 
Kuna mchangiaji humu amedai kua mkt Mbowe tayari ana kituo cha redio kilichopo kwenye hoteli yake (protea hotel)iliyopo machame ila bado hakijaanza kurusha matangazo yake hewani,hivyo basi kwa sababu tayari alishachangia magari yake yakakisaidia chama naonelea ni busara pia kuchangia na hii redio iwe ya chama kwani mzee wa chama mzee Mtei anamuamini sana shemej yake huyu na ndio maana zito kabwe alivyotaka kugombea uenyekiti mzee akamchomoa kwa madai hawez kumkabidh chama mtu ambae hamjui!!( a man from nowhere!!),mi nafkir mbowe aendele tu kujenga imani kwa mzee huyu ili badae akikaribia magogon ajirefund!,pissed off ee!!!!
 
Back
Top Bottom