Mheshimiwa huyu ni mfano wa kuigwa na wengi

MORIA

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
706
277
Mimi ni mkazi wa dom,kuna mheshiwa mmoja kwa kweli sisi jirani zake wa hapa area( ) tunampongeza kwani kila ajapo kwa vikao vya bunge huja na mke wake, jioni atokapo huwa anamshika mkono mkewe afu haoo! - ktk hili ametuambukiza, unaweza sema ni kitu kidogo tu sisi wakaazi wa dom tunajua vurugu za hawa ndugu (sio wote) hawaji na wake zao,kukesha chakos n' clabus, kifupi the v8 zinakuwa ktk patrol ya hiyari haijalishi ni week'nd au la....HIVI NI MTIHANI KWA SISI KINA BABA WA TZ KUTOKA AU KUMSHIKA MKONO WIFE MBELE ZA WATU? huo ni mkono je kiuno itakuwaje? je ni dini au mila? michango p/se
 
Watu wanaogopa kuonekana na wake zao...wengine wanaogopa kuonekana mazoba...wengine basi tu sijui hata wanaona tatizo gani!
 
sio uwoga ni culture

ndo maana kwenye culture yetu
kuna akina baba na akina mama

wakati wenzetu kuna mr and mrs....
 
Watu wanaogopa kuonekana na wake zao...wengine wanaogopa kuonekana mazoba...wengine basi tu sijui hata wanaona tatizo gani!
kwanini waogope? au ndo mambo ya kuchafua mtaa..hakuna uzoba tena ndiyo kileo obama style
 
Tabia za kuwa na vidumu kila kona vinasababisha wanaume wengi kukosa ujasiri wa kuonekana barabarani na wake zao. Kwa wengine ni ushamba tu ila kwangu mi nafikiri kutembea na ubavu wako uliyemchagua mwenyewe ni jambo zuri sana na mara nyingi wake zetu wanaongezeka confidence unapokuwa naye na ukutanapo na friends kumtambulisha. Kuna wale akina mama wanaofanya kazi inakuwa ngumu sana kuwa na waume zao mara kwa mara na hivyo ukiwaona waume zao wako peke yao usiwaelewe vibaya. ILA MWANAUME YEYOTE ANAYE JIAMINI HAONI TATIZO KUTOKA NA MKEWE, KUCHEKA NAYE WAKIWA PUBLIC N.K.
 
kwenye culture yetu
hata misibani ni akina baba peke yao,na akia mama peke yao
 
hata harusi ni hivyo hivyo
kina baba peke yao,kina mama wako nyuma ya nyumba peke yao

mr and mrs ni kwenye party tu,reception
 
Unajua kujizoeza kitu kipya ni vigumu sana.Sisi mambo haya ni mageni kwetu.Lakini tabia hizi zimeota mizizi sana katika desturi za watu wa nchi za maghariba,lakini hata wao hawakuwa na tabia hizo some generations back.Hata hivyo sidhani kama tunahitaji kuiga kila kitu kutoka kwa wazungu.Kwanza mambo yao mengi ni ya kishenzi tu.Sio lazima umshike mkono mkeo ndio ajue kwamba unampenda,upendo ni zaidi ya kushikana mikono.
Watu wanaogopa kuonekana na wake zao...wengine wanaogopa kuonekana mazoba...wengine basi tu sijui hata wanaona tatizo gani!
 
Hongera zake huyo anyeonesha uaminifu wake kwa mkewe kwani ni jambo jema,
azidi kuonesha zaidi gizani isiwe nuruni tu peke yake.
 
Ni kweli huyo mbunge ni wa kuigwa! Unajua tatizo la hao wabunge wasiokuja na wake zao(wenye nao)ni kuwa watakosa uhuru wa kujinafasi na izo nyumba ndogo! Ila wakaaji wa DOM mna kazi kubwa ya kuwalinda wake zenu na mabinti zenu thidi ya hao wabunge walafi. Poleni sana!
 
asante, kazi kidogo tunayo kaka..!
 
hata harusi ni hivyo hivyo
kina baba peke yao,kina mama wako nyuma ya nyumba peke yao

mr and mrs ni kwenye party tu,reception

Kwahiyo huko kwenye party culture hakuna?
Hivi kumshika mkeo/mmeo mkono tu.......kunavunja heshima jamani?
 
si jambo jema kwani inaonekana kabisa huyo mama hana kazi so kitu muhim ni pale mume anamtafutia mke kazi ili mkono uende kinywani na sio kusindikiza tu mme kapata tumepata kakosa tumekosa..
 
Back
Top Bottom