Chief Rumanyika
Senior Member
- Dec 29, 2010
- 138
- 0
WATANZANIA MCHAKATO MZIMA WA KATIBA MPYA NI HAKI YETU NA WALA SI MILIKI YA RAIS
Heri ya Mwaka Mpya 2011 kila mmoja wetu!!
Ndugu zangu Wana-JF na Watanzania kwa ujumla wetu, tusisahau mambo ya msingi yaliotufikisha hapa hasa sisi VIJANA kutaka kujiandikia wenyewe KATIBA MPYA.
Sote tunaelewa ya kwamba KATIBA ni MKATABA rasmi kati ya WATAWALA (Serikali) na WATAWALIWA (Sisi Wananchi) kusimamia maendeleo yetu, usimamizi mzuri wa rasilmali zetu, na kuzingatia haki katika taifa letu.
Kimsingi mara baada ya wengi wetu kugundua ya kwamba WATALA WETU hawako tena darakani kwa MASLAHI YETU KAMA UMMA WA TANZANIA bali lao ni kushiriki uchafu mwingi ukiwemo UFISADI WA KUPINDUKIA hapo ndipo wazo la zaidi ya miaka 20 sasa likatujia upya KUANZISHA MARAMOJA MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA.
Lengo letu hapa ni kwamba tunataka kuwadhibiti WATAWALA na tamaa zao wasiathiri tena maendeleo ya taifa letu. Kitendo cha Rais Kikwete naye kupendezewa na wazo hili la wananchi KUJISHIRIKISHA KATIKA KILA HATUA YA MCHAKATO MPANA KUPATIKANA KATIBA MPYA ni jambo la kupongezwa kwake kama raia mojawapo nchini mwetu ambaye naye ana haki kulizungumzia katiba kama mzaliwa wa taifa hili.
Hoja Yangu:
Sote tunatambua ukweli kwamba TUNAPOZUNGUMZI UTEKELEZAJI WA KATIBA ILIOTAYARI hapo wanahitajika watendaji ambao ni WATAWALA kwa misingi ya vyeo vyao kufanya hiyo kazi.
Ila kwa upande wa pili, TUNAPOZUNGUMZIA UUNDWAJI UPYA WA KATIBA YA NCHI hapo WATAWALA huitajika kuchagua kujumuika pamoja na wananchi watawaliwa (kwa msingi wa haki yao ya uraia wao na wala si VYEO VYAO) kuja KUANZISHA MCHAKATO PAMOJA NA KUIENDELEZA KILA HATUA PAMOJA huku washiriki wote wakiwa na cheo cha URAIA TU kwenye kuunda KATIBA MPYA.
Kwa msingi huu, Mhe Kikwete, hawezi akajitwisha jukumu la RAIA WOTE WA TANZANIA kujiendeshea hatua zozote za mchakato mzima wa kupatikana kwa KATIBA MPYA. Endapo atakua na maoni yenye kusaidia basi awe huru kuja nayo kwenye MKUTANO MKUU WA TAIFAKUANDIKA KATIBA utakaoundwa na bunge.