Mhadhiri Bakari Mohammed wa Mzumbe University amjibu JK kisayansi!

Ok. Kumbe ni hesabu rahisi:

1. 315 000 * (15 / 100) * 400 000 * 12 = 226 800 000 000

2. 315 000 * (3 / 100) * 400 000 * 12 = 45 360 000 000
 
Mhadhiri kwa kweli I SALUTE YOU!!
Sasa kwa kuwa imedhihirika kwa ushahidi wa zaidi ya mara moja ukianzia na ule muswada wa gharama za uchaguzi na hii ya gharama za mishahara kwamba rais analidanganya taifa kwa makusudi, na ni uvunjaji wa katiba ya nchi kwa makusudi, hivi anasuburi nini huko ikulu asiondoke.
P/se mzee mwanakijiji huwezi ukatunga kitabu kwa kichwa cha 'IKULU YA VIHIYO?' maana ikulu yetu imesheheni vihiyo. Eeh ndiyo namaanisha hivyo!!
 
Duuh!! Hii kali sana jamani!! It's simply unbelievable! Seriously. I am genuinely shocked!
 
Hahahahaaa...huyu jamaa kweli kaenda shule huyu maana huu uchambuzi huu....kiboko msheli kweli kweli

Huu uchambuzi utawauma sana na wataanza kuuliza kuwa Mhadhiri anafanya kazi kwa mkataba baada ya umri wa kustaafu kufika au bado anafanya kwa ,ujibu wa sheria, kitakachofuata ni Mkuu wa chuo kutumiwa ujumbe amuonye kijana wake. Hawa ndiyo CCM aliowachambua, wanajua kabisa kuwa Tanzania yenye watu walioelimika ni tishio kwa mustakabali wao ndiyo maana wanaua viwango vya elimu kwa sera mbovu.
 
Dokta atakuwa anatengeneza wajenga hoja wazuri chuoni...uchambuzi wako umeniguza sana!Tunahitaji kuhakikisha hii makala inamfikia kila mfanyakazi.Kama unaweza ku-print na kuhakikisha rafiki yako anaipata tafadhali fanya hivyo!
 
Na mimi sinaga historia ya kubadili badili misimamo yangu.

Watu kama ndugu Bakari na yule Bibi aliyesafiri ni vielelezo tosha kabisa kuwa si miafrika yote ndivyo ilivyo ni miongozi inakaa madarakani kwa vitishoo!Huwezi kuwaambia wafanyakazi ambao kodi yao ndiyo inayolipa mshahara wako eti mimi ni mwajiri acheni kazi kama hamtaki,kauli gani hio kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi nayesimamia mali zetu kwa niaba yetu?ama ukiwa raisi unamiliki nchi ama unatawala?Bibi amenifurahisha sana kumkumbusha kuwa uongozi ni dhamna?

Back to the point,kudanganywa kuhusu facts vs usahuri mbaya ni vitu tofauti,na kwenye maelezo yako haukuwa clear,uligenerelize,ungekuwa more specific kwa sababu umejumuisha matokeo yote aliyoboronga kwa kublame ushauri na wakati kwenye issue hii hapa ni udangayifu wa facts,sasa sijui kisichoeleweka hapo ni ni kipi?maana ni wazi kama angechanganya na zake,basi angedouble check na si kuendesha mabo way too ina partisan way in issue tat demands some kind of bitartisanship...Unanegotiate na wafanyakazi unaenda kuongea na wazee wasio na kazi ama kustaafu ni out of touch
 
Halafu naona ukitoa Personal Income Tax ya mishahara (Sijui ni percent gani, lakini yote inaishia Hazina aka Serikalini), hesabu itapungua zaidi, au siyo?
 
Kwa kweli sikupata nafasi ya kuisikia audio ya hiyo hotuba,hivyo mpaka sasa ninaungaunga tu yale ambayo yamekuwa yakinukuliwa na media pamoja na members wa hapa jamvini.Baada ya kusema hayo,nataka nijaribu kwenda nje ya box ili kupata kile ambacho mr prez alitaka kumaanisha.Kwa uelewa wangu ni kuwa kati ya hao wafanyakazi let say laki tatu na nusu,sio WOTE ni wa kima cha chini.Hivyobasi,itakapokubalika kuwa kima cha chini kiwe hiyo laki 3 na kumi na tano elfu then tutegemee kuwa yule anayelipwa laki 3 kwa sasa atadai ongezeko pia(% ngapi,sijui!) hivyo kama wafanyakazi wa madaraja mbalimbali ya mishahara watadai a proportional increament then hesabu za jumla ya kiasi kinachohitajika kuwalipa hakitakuwa kama hiki alichokionesha Dr.
Mkulu angeweza kuiweka kisomi kama angekuwa walau ametoa breakup ya % ya wafanyakazi katika ngazi mbalimbali za mishahara at least kwa range tu,kisha angetoa projection ya namna mishahara itakavyokuwa baada ya ongezeko.
Pia,katika kuifikia hiyo jumla wasisahau kuwa kuna PAYE ambayo inarudi kwao,hivyo ni kipato kwa serikali.
 
Halafu naona ukitoa Personal Income Tax ya mishahara (Sijui ni percent gani, lakini yote inaishia Hazina aka Serikalini), hesabu itapungua zaidi, au siyo?

On top of that sio wote hawa 400,000 workers ni kima cha chini kuna kama 10% ya hii idadi mchanganuo hauwahusu!
 
Watu kama ndugu Bakari na yule Bibi aliyesafiri ni vielelezo tosha kabisa kuwa si miafrika yote ndivyo ilivyo ni miongozi inakaa madarakani kwa vitishoo!Huwezi kuwaambia wafanyakazi ambao kodi yao ndiyo inayolipa mshahara wako eti mimi ni mwajiri acheni kazi kama hamtaki,kauli gani hio kutoka kwa kiongozi mkuu wa nchi nayesimamia mali zetu kwa niaba yetu?ama ukiwa raisi unamiliki nchi ama unatawala?Bibi amenifurahisha sana kumkumbusha kuwa uongozi ni dhamna?

Usinifanye nianze kwenye hili la Miafrika maana hapatakalika hapa. You know how passionate I am about it....Miafrika Ndivyo Tulivyo ni zaidi ya unavyodhania wewe....

Back to the point,kudanganywa kuhusu facts vs usahuri mbaya ni vitu tofauti,na kwenye maelezo yako haukuwa clear,uligenerelize,ungekuwa more specific kwa sababu umejumuisha matokeo yote aliyoboronga kwa kublame ushauri na wakati kwenye issue hii hapa ni udangayifu wa facts,sasa sijui kisichoeleweka hapo ni ni kipi?maana ni wazi kama angechanganya na zake,basi angedouble check na si kuendesha mabo way too ina partisan way in issue tat demands some kind of bitartisanship...Unanegotiate na wafanyakazi unaenda kuongea na wazee wasio na kazi ama kustaafu ni out of touch
Nadhani nilikuwa wazi kabisa kuhusu yule niliyekuwa namjibu dhidi ya kile alichokiandika. Tatizo labda ni uwezo wako wa kuelewa au ulisoma kwa juu juu na haraka au pengine labda ulikuwa umelewa mbege....
 
Chairman Mao Zedong’s Calligraphy ;
Unique legacy

Even now, Mao's words are quoted frequently among many Chinese people, especially those of middle-age: Mao's term for imperialism, “ Paper tiger [FONT=&#23435]纸老虎
(zhi laohu)”, refers to something that appears fierce and threatening, but is actually harmless; “the early morning sun at 8 to 9 [FONT=&#23435]八九点钟的太阳[/FONT] (ba-jiu dianzhong de taiyang)” refers to young people; “no research, no right to speak [FONT=&#23435]没有调查研究[/FONT] (meiyou diaocha yanjiu), [FONT=&#23435]就没有发言权[/FONT] (jiu meiyou fayan quan)” refers to the necessity of doing investigation when working.
[/FONT]
 
Huu uchambuzi utawauma sana na wataanza kuuliza kuwa Mhadhiri anafanya kazi kwa mkataba baada ya umri wa kustaafu kufika au bado anafanya kwa ,ujibu wa sheria, kitakachofuata ni Mkuu wa chuo kutumiwa ujumbe amuonye kijana wake. Hawa ndiyo CCM aliowachambua, wanajua kabisa kuwa Tanzania yenye watu walioelimika ni tishio kwa mustakabali wao ndiyo maana wanaua viwango vya elimu kwa sera mbovu.
Kinyume chake ndiyo sahihi. Dr. Bakari amesadia kutoa sura nzuri ya chuo kikuu cha Mzumbe. Kwa hivyo mkuu wa Chuo atamchukulia kama mfanyakazi bora aliyepandisha hadhi ya chuo. Unakumbuka kulikuwa na habari za wahadhari feki chuo kikuu cha Mzumbe? Ni sifa kwa mkuu wa Chuo cha Mzumbe kuwa na Mhadhiri safi kitaaluma kama Dr. Bakari.
 
It dont make no difference,i stand with my post.
Jamani mwenzenu lugha ya kigeni imenipita kushoto, lakini hapa naona maluweluwe tu, wataalam wa lugha hii ya kigeni nisaidieni. It dont make no difference? Jamani si tutumie tu lugha yetu ya taifa na hasa ukizingatia Dk Bakari ameandika habari yake kwa Kiswahili.
 
Tukuulize mwenyewe hivi unaweza kuishi kwa laki moja kwa mwezi Dar es Salaam? Hiyo laki tatu tu kwa mwezi haitoshi hebu tafakali hili mshahara sh. 315,000/= familia ya watu 6 yaani Baba Mama na watoto wa 4 wanaosoma shule ya msingi na sekondari. Nauli ya baba kwenda kazini (posta) ni sh.700*21=14,700, watoto nauli pamoja na hela ya kupunguza njaa shuleni ni sh.400*4=33600, chakula kwa siku asubuhi mikate sh.2,1200*30=36000, Mchana dash! Usiku unga sh.800, mkaa sh. 500, mafuta ya kupikia sh.300, nyanya sh.300, vitunguu sh.200, maharage nusu kilo sh.600, dagaa fungu sh.300, ndimu sh. 200 hesabu hii jumlisha kisha zidisha mara 30 utapata (800+500+300+300+200+600+300+200)*30=105000. Hii jumlisha na nauli ya baba na watoto wa nne: 105000+36000+33600+14700=189300!

Yaani hapo umeishi kimkanda ile mbaya lakini matumizi yameshazidi mshahara wa laki moja! Na hapo hatujaingiza gharama za maji, umeme,na kodi ya nyumba ya kutosha watu 6. Hebu tujaribu kidogo. Kwa nyumba ya kupanga yenye umeme,bei ya chini ni sh.20,000 kwa chumba hivyo vyumba viwili na sebule ni sh.60,000 bei za mbezi mwisho makabe huko au mbagala ndani ndani (kumbuka ukienda nje ya mji pia nauli zaongezeka!. Maji ya kununua tuseme ndoo shilingi sh.50(kawaida ni sh.150-400 maeneo mengi jijini) unatumia ndoo takribani 8 yaani lita 160 tu! za maji kupikia,kuoshea vyombo, kuogea na n.k itaenda sh.12000 kwa mwezi. Umeme utakugharimu say sh.16000 tu kwa mwezi hapo itakuwa sh. (60,000+12,000+16,000=88,000/= ) ukijumlisha na ile nyingine unapata sh. 277,300/=, hapo unadaiwa sh.37,700 tu ili ufikie kima cha chini alichogomea Rais.

Kumbuka pia hela hiyo ie 315,000 itakatwa kodi PAYE (sh.27,525/=) baada ya makato ya mifuko ya hifadhi (mfano NSSF ni 10% ya "Gross salary",) jaribu kuingiza
hapa hiyo hela utapata kodi, pia kuna makato ya nayoenda mifuko ya hifadhi ya jamii (eg NSSF ni 10% ya mshahara kabla ya kodi ie31500 ) Ukitoa mshahara 315,000 unapata (315000-31500-27525) shs.255,975 huku matumizi yakifika sh.277,300/ na hapo Baba uache pombe, sigara, na familia msimiliki simu ya mkononi wala msiumwe au kununua nguo, wala kupaka mafuta, kuoga na sabuni au kusugua meno kwa dawa za meno vinginevyo hesabu itapanguka kabisa.

Mheshimiwa Rais hebu tuombe radhi sisi wafanyakazi wako maana hukututendea haki kwa kutukorome kiasi kile kwani madai yetu ni ya Msingi mno.
Wakuu katika pita pita zangu kwa mithupu nimeona comment hii.

Haya ndo maisha halisi ya MTZ mwenye kipato cha chini.
 
Ni dhahiri rushwa, wizi, utendaji mbovu, madili kazini nk havita koma. Nawaonea huruma walimu wananafasi ndogo mno kutengeza madili.
 
Back
Top Bottom