Mh Mnyika, ARE you serious? ni serikali ipi unaiongelea

Honorable Mnyika,

I applaud your courage. However, I feel that you engage yourself in activism politics as if you aren't an elected official. I don't understand why you called a press conference in order to beg the government to improve the well being of its people. Leave this to politicians who have no mandates or leave to activists who don't desire higher offices.

As a member of parliament, I expect you to call a press conference and spell out your policies. Tell them in details so we can differenciate your policies from those of the ruling party, and you don't need to wait until the next election. Basically, we want to hear the actions you would have taken if you were a president, prime minister, or member of the cabinet.

To ask the president to formulate new economic policies with the help of his cabinet and economic council indicates that you know the problem, but You lack solutions or you don't want to take political risks.

Anyway, you are a party of the current government albeit in opposition. The Tanzanian government has three branches of government: Executive, Judicial, and legislative. As a member of parliament you are in the legislative branch, and I expect you to use your legislative power. Why don't you ask the government to cut it expenses?
 
Anachokisema Mnyika ni realistik, we washawishi wenzako waiondoe CCM madarakani ndio utathibitisha kauli za mnyika kama ni realistic au la.
Nachelea kusema wanachama woote wa ccm ni vilaza naishia kusema huenda wamelogwa hawa watu.
Wajiangalie walikuwa wanapataje wanachama wake.
 
[h=2]wana JF kuna wakati naona huwa tunatumia vibaya uhuru wa kuongea tulio nao. NI mejaribu kuosma hii excerpt kutoka kwenye gazeti la Guardian Online version la tarehe 23 Januari. Mh mbunge John Mnyika anajaribu kutoa maoni kuhusu hali ya uchumi, hebu soma kidogo......

"Serikali ilete mpango wa kunusuru uchumi: Mnyika"[/h]
Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, aliitaka Serikali kupeleka mpango wa dharura wa kuimarisha uchumi na kupunguza gharama za maisha kwa wananchi katika vikao vya kamati ya bunge vinavyoendelea kabla ya kuwasilisha katika mkutano wa bunge unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Mnyika aliitaka Serikali kuongeza uzalishaji na usambazaji wa vyakula katika soko la ndani pamoja na kuwawezesha wazalishaji wadogo na wa kati katika kilimo na viwanda ili kuongeza mauzo nje ya nchi.

“Serikali inapaswa kuharakisha matumizi ya gesi asilia na utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme…itekeleze mkakati wa kupunguza manunuzi yake ya nje kwa bidhaa na huduma ambazo zinapatikana nchini,” alisema Mnyika.


Hivi kweli anayoongea Mh Mnyika ni realistic? Nani atamsikiliza? Ni kweli serikali yetu kupitia waziri wa fedha Mustafa Mkullo ina uwezo wa kuja na plan ambayo inayoweza kurescue uchumi wetu? NI kweli serikali inaweza kuongeza uzalishaji na usambazaji wa chakula katika soko la ndani? Ni wapi serikali inakozalisha chakula? Au ndio yale ya kuongea jukwaani na kuwataka wananchi walime heka mbilimbili za mahindi bila kujali uwezo wao, hali ya hewa, shughuli zai kiuchumi au hata kama wtu wenyewe wanataka kufanya hivyo au la.

Anaposema serikali "itekeleze mkakati wa kupunguza manunuzi yake ya nje kwa bidhaa na huduma ambazo zinapatikana nchini" ni manunuzi gani yanayofanywa na serikali kwa bidhaa za nje zinazopatikana nchini?

Ukiangalia kwa undani inaonekana kuwa baadhi ya hoja zinatolewa na waheshimiwa wetu bila kuwa makini. Hivi kweli kwa serikali hii tuliyonayo sasa ambayo imeshindwa kuplan hata katika wakati usio emergency, inaweza kuplan nini cha dharura? katika full article mheshimiwa pia ameongelea issue ya umeme, sijui kama kweli anaelewa ni nini kinaendelea serikalini kuhusu issue nzima ya umeme. Serikali imeshindwa ku deal na suala la umeme toka day one, hivi kweli anaamini kuwa serikali hii inaweza kudeal na tatizo la umeme?

My point here is naona mheshimiwa anaongea vitu ambavyo ni unrealistic. Mh Mnyika najua unasoma hii post naamini utaifanyia kazi.
Mkuu hapa mbona hueleweki vema,unamlaumu mh.Mnyika kwa kuonesha njia na suluhu ya kufikia maisha bora kwa kila mtanzania?unamkosoa kwamba apaswi kuikumbusha serikali iliyo madarakani njinsi ya kuimarisha uchumi kwa manufaa ya watanzania?au unamsifia mh .Mnyika kwa kuikumbusha serikali isiyo sikivu jinsi ya kuwatoa watanzania hapa tulipo kuelekee maisha bora?Unataka kutuambia anayoyasema Mnyika ni vitu vya ukweli na vya msingi ila kwa serikali kiziwi,bubu,kipofu,walafi kwa hiyo anapoteza muda wake bure?make me clear
 
ulitaka asemeje?

Hapo ameitaka/ameishauri /amekumbusha serikali wajibu wake katika kutumia rasilimali na kuboresha uchumi.

Kufuata au kutofuata ni weakness ya serikali husika, na si Mnyika
 
Bongolander,

Asante kwa maoni yako, sisi hatuongozi serikali kwa sasa kwa maana ya kuwa na Rais na mawaziri hivyo ili kutoa mchango wetu kwa taifa kusukuma maendeleo katika kipindi hiki mpaka uchaguzi mwingine utakapofanyika ni lazima tutimize vizuri wajibu wa kuisimamia hii serikali iliyopo madarakani. Ndio wajibu ambao naufanya.
Itakumbukwa kwamba Tarehe 28 na 29 Oktoba 2011 Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo alinukuliwa na vyanzo mbalimbali akieleza kwamba mpango kabambe unatarajiwa kupitishwa na baraza la mawaziri kuboresha uchumi na kupunguza gharama za maisha. Kauli hiyo ya Waziri Mkullo aliitoa siku chache baada ya mkutano wangu na waandishi wa habari wa tarehe 23 Oktoba 2011 ambao nilitoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kuitisha kikao cha dharura cha tume ya mipango na baraza la mawaziri kupanga mpango wa dharura na wa muda mrefu wa kupunguza gharama za maisha kwa wananchi kwa kudhibiti mfumuko wa bei pamoja na kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania. Aidha, nilitoa mwito pia kwa bunge kuingilia kati kupitia kamati zake za kisekta na hatimaye kwa serikali kuwasilisha bungeni mpango wa kukabiliana na matatizo husika ya kiuchumi ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi na maisha ya wananchi.

Miezi zaidi ya miwili imepita toka Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo
atoe ahadi kwa niaba ya serikali kuwa mpango kabambe unatarajiwa kupitishwa kuboresha uchumi na kupunguza gharama za maisha; ndio maana nimeendelea kuibana serikali ieleze mpango huo umefikia wapi ili kunusuru maisha ya wananchi.

Ikishindikana kwa njia za kawaida za kibunge itabidi tuelekee katika hatua za kuunganisha nguvu ya umma, ndio kazi mliyotutuma ya kuwawakilisha na kuwatumikia.

JJ

Mh Mnyika umeeleza vizuri na umeeleweka vizuri, naona baadhi ya wachangiaji hapa wana mawazo ya Uchadema na Uccm, lakini mimi naangalia zaidi Tanzania. Kwenye aya ya pili kabla ya mwisho umemnukuu Mkullo akisema mpango kabambe. Toka nianze kuwasikia mawaziri wa serikali zetu mbalimbali wakiongea, wanatumia sana hilo neno mpango kabambe, lakini ukiangalia utendaji unaona kuwa hakuna kitu chochote kinachofanyika. Na wewe mwenyewe umesema ni miezi miwili sasa imepita tangu autaje huo mpango kabambe, kutokana na uzoefu ni kwamba itapita miaka miwili na hata karne mbili kama watanzania tutaendelea kufuata old timie politics za kumsikiliza waziri na kusubiri atekeleze ahadi.

Nakubaliana na wewe na kukupongeza kwa juhudi zako kuendelea kufuatilia serikali imefikia wapi na mpango huo "kabambe" ambao nakuhakikishia kuwa hautapunguza ugumu na gharama za miasha kwa mtanzania, kwa kuwa tangu aseme ugumu unaendelea kuongezeka. Lakini hiyo aya ya mwisho naona ndio inayotakiwa zaidi na haswa ndio maana tuliwachagua kama ulivyosema, that is more realistic and brings hope. Ikifanikiwa ndio italeta mabadiliko ya kweli.....otherwise it will still be talk talk and talk.
 
Mh Mnyika una mawazo mazuri na yenye mguso kimantiki, lakini hawa jamaa unaowapa huo ushauri ni muflisi kabisa, hatua waliyofikia hawawezi by any means kuimarisha uzalishaji na usambazaji wa gesi, hawana na hata wakiwa na plani ya umeme wa dharura hawawezi kutekeleza. wamekata tamaa kila mmoja anajiandaa kuondoka au kuondolewa katika nafasi aliyopo maana kwanza hawaamini kwa uvundo huu bado baraza la mawaziri lipo! wanachofanya ni kutumia kila upenyo kuchukua vya mwisho. DAWA NI MOJA TUJIPANGE TUNAIONDOAJE CCM MAPEMA IWEZEKANAVYO?
 
Kwa nini nchi nyingine "tajiri" wabunge ndio wanaandika na kupeleka hizi plan bungeni? I guess sisi ni "masikini" wa vichwa, na wabunge hawawezi ku afford printing paper na computer.

Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007,

Kipengele 81 ( 1 ):

Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha Bungeni Muswada Binafsi wa Sheria.


Halafu kanuni zinarudia tena!

Kipengele 82 ( 2):

Muswada Binafsi wa Sheria unaweza kuwasilishwa Bungeni na
Mwenyekiti wa Kamati yoyote ya Kudumu ya Bunge au Mbunge
yeyote ambaye si Waziri.


Nilidhani kizazi kipya cha Bunge la kumi la kina Mnyika na January ndio watakuwa trailblazers wa mambo mapya bungeni, kumbe wapi, kazi kuimbisha waandishi wa habari mitaani tuuu, no! Put that stuff down on paper, send it up to the house!
 
Naona unalienzi jina lako, sidhani km wapinzani ni wasema chochote, mifano ipo wazi kwa njinsi walivyoichachafya serikali kwa maslahi ya umma na yakatekelezwa waliyokusudiwa, hvyo basi ni jukumu la upinzani kuikumbusha na kuikosoa serikali iendapo ndivyo sivyo.

  • :juggle:
 
Back
Top Bottom