Adoe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 235
- 68
Ni siku nyingine tena, mwenzetu Mh. Mabumba alipokuwa amekalia kiti cha Bunge alijitelezesha na kujiingiza katika tope lililomchafua na baadaye akashindwa kutoka humo hadi watani zetu wakaanza kutucheka na mbaya zaidi wananchi tunaowategemea wanaanza kutuona kuwa sisi hatuna watu makini na kwamba pengine tupo si kwa ajili ya haki na maendeleo yao.
Mh. Mabumba: Hivi ulipomwambia Mh. Mnyika kuwa anawashwa, akae chini ulimaanisha nini na ulitumia kanuni ipi kuachilia tusi hilo na kwa faida ya nani. Unafikiri kuwa CCM tunapata sifa kwa kutoa matusi au kujibu kwa matusi Wapinzani wakati umepewa dhamana ya kuongoza kikao cha juu sana katika nchi- cha muhimili wa Taifa? Yaani mwangwi wa sauti yako ya Kaa chini!!... cheap popularity !!.... imekuexpose kuwa huwezi kuongoza vikao vya namna hiyo wala ku-controll heated debates. A Moderator will never dream to be defamatory.
Mh. Eng. Manyanya: Ulianza vyema kumpa pole Dr. Ulimboka na pia si vibaya ulipoonyesha masikitiko ya Wananchi kukoswa huduma muhimu za Afya tokana na mgomo. Lakini imeshangaza ulimwengu, kwa heshima uliyonayo kama Msomi, Mbunge na Mkuu wa Mkoa kujiingiza katika kauli tata na za mipasho hadharani.
Ni kitu gani kilikupeleka uendelee hadi kufikia kutamka waziwazi ndani ya Bunge hitimisho kuwa CHADEMA wanahusika katika kumteka na kumjeruhi Dr. Ulimboka? Ukasema kwamba wao ndio wenye magandwa kama wale waliomteka Daktari. Aidha ulijisukumiza katika shimo hatari kwa kuanza kumbeza Dr. Ulimboka aliye katika matibabu ya kuokoa maisha yake kwa kumfananisha hadharani na Muuaji Hitler; Eng. what a scrawny analysis, fallacious, insalubrious talk & dodgy statements!
Injinia, je huwezi kufikiri kwa nini hata katika speech ya Rais, aliongelea mgomo usio halali lakini aliwaomba Madaktari warudi kazini na kuhusu Ulimboka alitoa kauli za kuagiza vyombo vya dola kuwatafuta wahusika (wawe ni wa CCM, CHADEMA, CUF au wasio na Chama sisi hatujui) na shauri hilo lifikishe mbele ya haki. Wewe unaanza kumhukumu mtu kama huyo aliyepona kuuawa na kumwita Muuaji katika hali aliyo nayo sasa kwa faida ya nani? Unafikiri kuwa wananchi wataipenda CCM zaidi kwa kuongea hivyo wakati wananchi wote wanalaani kwa namna yeyote mtu kutekwa na kupigwa au kuuwawa hata kama ana makosa maana kwa nini asifikishwe katika vyombo vya dola kama ana kesi ya kujibu?
Mh. Mwigulu: Ulishashauriwa siku za nyumakuwa kwa level yako kama Mbunge na Kiongozi wa Kitaifa wa CCM (NEC Uchumi & Fedha), kabla ya kuongea ebu tulia na kufikiri kidogo. Ile statement uliyo quote Bungeni ya Wapinzani wakisema endeleeni kudai haki zenu sisi tunawaunga mkono, huwezi kuitumia kuthibitisha kuwa CHADEMA wamehusika na tukio la kumteka Daktari wala kuongoza migomo isiyo halali! Hata mimi na wengi wetu wana CCM tunasema kuwa moja ya majukumu yetu ni kuwaunga mkono Wananchi kudai haki zao. Rejea Lengo namba 5 la CCM;
Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya masiha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria na pia namba 7 ;
Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kuwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.
Mh. Mwigulu, kwa utetezi au upingaji wa kauli hiyo tu, Wananchi wataweza kutofautisha kuwa ni nani yuko kwa ajili ya haki zao na ni yupi hayuko nao. Hakika mnasababisha watu kutuchukia na Chama chetu bila kujua maskini! Taarifa yako Bungeni leo tena haikuwa na mashiko. Sikilizeni, Kazi yetu CCM inatakiwa kuwa kusukuma kwa ushawishi Madaktari & Serikali kukutana na kutatua mgogoro uliopo. Pili, ni kuhakikisha kuwa yeyote aliyeshiriki jaribio la kumwondoa uhai Dr. Ulimboka anafikishwa mbele ya haki. Kama tuna madai juu ya Ulimboka tuyafaili afikishwe polisi na mahakamani ayajibu. Na kamwe iwe marufuku yeyote mwana CCM kushabikia dhuluma, vitisho, utekaji wa wananchi na kujichukulia sheria mkononi hata kama ana hatia. Anayebisha basi avuliwe uanachama wa CCM maana yu kinyume na lengo letu la CCM namba 16.
Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi , rushwa , uonevu na au upendeleo. Halafu tuelewe kuwa kuwa na nia ya kusikiliza madai ya madakrari ni tofauti na kwamba yametekelezwa.
Nauliza hivi ni Madaktari wangapi leo hii wameshapewa hayo magari au hata kujaza fomu za mikataba hiyo nchini kote, waliokwisha pewa makazi, ambao wameshaanza kupokea hiyo allowance mpya wanazosema na mishahara ya juu wakati tunajua kuwa kuna Madaktari wengi sana kote nchini (hii si issue ya Muhimbili tu) ambao bado wana madai ya arrreas za mishahara yao ya toka mwaka jana!
Kwa nini mnapenda sana kumpa taarifa zisizo kamili Rais wetu eti yote kasoro mawili tu ndiyo yametekelezwa? Wabunge muitishe taarifa za ma- RMO's kama hawana madai ya Madaktari ya siku nyingi tena ya vile viwango vya zamani na hayajalipwa? Ndani ya CCM tupo wengi ambao hatuvumi lakini tupo. Msituharibie CCM yetu- Arhrhghh!!
Jueni kuwa CHADEMA wanapoona tunakubali kuvaa viatu walivyotuazima wanafurahi sana! Watch out our role & strategies are completely different:yawn:!
Intelligente, Gracias!