Mh.Agrey Mwanri waziri TAMISEMI utaandikiwa Ripoti Ngapi??Chukua Hatua Mbwembwe za nini?

bushman

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,411
743
Mimi nilikuwa nafurahishwa sana na utendaji wa waziri agrey mwanri tamisemi,mpaka nikafikia hatua kusema na kuamini kama baraza la mawaziri litavunjwa saizi,basi awe waziri mkuu kwa sababu hajui kutafuna maneno tatizo akiliona.lakini nimegundua kuwa sehemu zote katika ziara zake anakopita amegundua matatizo/kasoro nyingi hasa ubadhirifu katika miradi mbalimbali ya serikali.mimi nachoka na kauli zako tu hasa unapotakiwa kuchukua hatua unasema "niandikie ripoti niipate ofisini kwa mara moja-utakuwa na ripoti ngapi ofisini kwako?kwa nini usiwawajibishe ili wengine wajifunze kutokana na adhabu hizo?kwa mfano kilolo umeagiza ukasanyiwe vyeti vya engineer uletewe wizarani ili ufanyie nini?chukua hatua mbwembwe za nini halmashauri karibu zote hali ndio hiyo.
 
Debe tupu haliachi kutwika. Mwanri is a show man, big time! Kama alikuwa ni mtendaji makini inakuwaje anajitokeza wakati majengo (anayosema yana hitilafu) yameshakamilika? Na tangu aanze hizo mbwembwe kwenye TV sijasikia watu wanafukuzwa kazi au kupelekwa mahakamani, anaishia kusema anataka barua, maelezo etc. Usanii!
 
Mima nahisi akipiga bit kwenye tv ,baadae wahusika wa matukio wanampelekea kitu kikubwa badala ya riport ndio maana hakuna hatuwa zinazo chukuliwa ina kuwa ni biashara yake
 
Kwa kweli jamaa anapenda show sio mchezo! Na hao makanjanja wanamfuata kila aendako! Ni stori juu ya stori! Let's hope atapata msg hii
 
debe tupu haliachi kutwika. Mwanri is a show man, big time! Kama alikuwa ni mtendaji makini inakuwaje anajitokeza wakati majengo (anayosema yana hitilafu) yameshakamilika? Na tangu aanze hizo mbwembwe kwenye tv sijasikia watu wanafukuzwa kazi au kupelekwa mahakamani, anaishia kusema anataka barua, maelezo etc. Usanii!
mimi kashanichosha anavuta hisia za watu kelele nyingi anaishia kuomba vyeti na ripoti wakati kwa macho yake kaona jengo bovu mengine mpaka anafikia hatua ya kugoma kufungua jengo kwa sababu ni mabovu kupindukia.
 
Mwanri uwa anatumia hisia na jazba sana,na hii itamsababishia kutoa matamko mengi ambayo kwa hakika hawezi kuyafatilia.Na unapofanya kazi ili watu wakuone au waseme unafanya kazi basi kuna hatari ya kuharibu.Nilitegemea huyu waziri afanya kazi kwasababu ni wajibu wake,ila kinachoonekana ni tabia ya mawaziri wengi sasa kufanya kazi na vyombo vya habari badala kufanya kazi kwa kulingana na wajibu wao.

Juzi nilimuona naibu waziri wa elimu nae akitoa tamko la kumshusha mwalimu mkuu kuwa mwalimu wa kawaida,na kuna siku chache tulimuona waziri wa elimu nae akipambana na wamiliki wa shule binafsi kule DSM,haya huku kuna Pombe nae kila siku haishi vituko.Nadhani ningewashauri mawaziri na viongozi wetu,wafanya kazi kwa mujibu wa mgawanyo wa kazi na sio kutafuta sifa na ujiko usio na tija.
 
Kumbe na nyie mmeona, mi nilijua huyu jamaa bonge la mtendaji baada ya kumfatilia nikagundua ni mtu anaeongea ongea tu ili watu wamuogope ila HANA LOLOTE, huyu mpaka amalize miaka mitano tutakuwa tunamzomea akija kwenye ziara huku
 
Mh.Agrey Mwanri, ana mkwara wa Beberu ya kusimama kupiga kicha kisha anaacha! kila mkutano wake yeye ni kufoka tu! Je mbona hatuoni tofauti na mabadiliko? Naye nikama wakuu wake Debe tupu Haliachi Kutika!
 
Hakika ili suala la kuomba vyeti na cv inawezekana kunakupelekeana bahasha ofisini,haiwezekani mtu apige mkwara wa kipuuzi.
 
Kwa kweli jamaa anapenda show sio mchezo! Na hao makanjanja wanamfuata kila aendako! Ni stori juu ya stori! Let's hope atapata msg hii
Kweli watanzania mmeamka, mko macho kweli kweli. Ni rahisi tu kumjua mpiga kelele. Kwa nafasi yake kama naibu waziri anapaswa kuwahoji wakuu wa wilaya wa maeneo hayo kwanini kazi haziendi au angewauliza wakurugenzi. Kwenda ku harass watumishi wa kada za chini ni kuvuruga serikali. By the way anazunguka kujenga himaya ya EL na kukusanya pesa za kampeni za kujiimarisha kichama.
 
Sijajua JF tunataka nini. . . Wakienda kwa Speed ya Kikwete na Pinda, ooh wapole sana, hawaganyi kazi. Wakipiga kazi

kama magufuli na Mwanri wanashow off. Ndo mana wengine wamepiga kimya kama kina Nagu. . . .
 
Kweli watanzania mmeamka, mko macho kweli kweli. Ni rahisi tu kumjua mpiga kelele. Kwa nafasi yake kama naibu waziri anapaswa kuwahoji wakuu wa wilaya wa maeneo hayo kwanini kazi haziendi au angewauliza wakurugenzi. Kwenda ku harass watumishi wa kada za chini ni kuvuruga serikali. By the way anazunguka kujenga himaya ya EL na kukusanya pesa za kampeni za kujiimarisha kichama.

Sipati pich Dr Slaa angekuta ****** anaokuta Mwanri angefanya nini! Unakuta ****** kama ule wa Iringa juzi, ukae kimya

tuu! Lazima uonyeshe power, watu wajue there is someone superior over them. Cha muhimu tungemtaka alete report ya

hayo maagizo yake. Hakuna mtu anayeniudhi kama Pinda na Jk! Pinda akikuta sehemu kuna ****** utaskia '. . . mimi

naomba hawa watendaji wajirekebishe. Nimemwagiza wasiri wa Tamisemi/CAG kufanya uchunguzi. . . ' ndo habari imeisha.

JK nae anapiga Kimya mambo yakizidi utaskia '. . . mimi nadhani tujirekebishe, hili jambo, . .enh hili jambo si zuri hata kwa

marafiki zetu. . ." . . Habari imeisha! Sidhani kama tunataka ujinga huu. Kwa Tanzania ya sasa we need The lion to roar

and make sure it eats something
 
Mimi nilikuwa nafurahishwa sana na utendaji wa waziri agrey mwanri tamisemi,mpaka nikafikia hatua kusema na kuamini kama baraza la mawaziri litavunjwa saizi,basi awe waziri mkuu kwa sababu hajui kutafuna maneno tatizo akiliona.lakini nimegundua kuwa sehemu zote katika ziara zake anakopita amegundua matatizo/kasoro nyingi hasa ubadhirifu katika miradi mbalimbali ya serikali.mimi nachoka na kauli zako tu hasa unapotakiwa kuchukua hatua unasema "niandikie ripoti niipate ofisini kwa mara moja-utakuwa na ripoti ngapi ofisini kwako?kwa nini usiwawajibishe ili wengine wajifunze kutokana na adhabu hizo?kwa mfano kilolo umeagiza ukasanyiwe vyeti vya engineer uletewe wizarani ili ufanyie nini?chukua hatua mbwembwe za nini halmashauri karibu zote hali ndio hiyo.

Mimi naangalia tofauti. Jamaa ana bosi wake ambaye yeye anaripoti kwake. Hawa watendaji anaopambana nao wengi wao wamewekwa au ni watu wa mtu/ watu fulani. Nafikiri anaposema andika ripoti niletee nitafuatilia anataka kujua huyu ni mtu wa nani ili asikanyage pabaya. Ila yeye na waziri wa wizara husika bora nani?
 
Debe tupu haliachi kutwika. Mwanri is a show man, big time! Kama alikuwa ni mtendaji makini inakuwaje anajitokeza wakati majengo (anayosema yana hitilafu) yameshakamilika? Na tangu aanze hizo mbwembwe kwenye TV sijasikia watu wanafukuzwa kazi au kupelekwa mahakamani, anaishia kusema anataka barua, maelezo etc. Usanii!
Ndo tatizo la waTz manungayembe.
Mtu akifanya kazi yake kwa bidii mnalalamika,asipifanyakazi ndo m a riot.undeni nchi yenu ya kupiga soga na kunywa chai.
 
Back
Top Bottom