Mgomo wa madaktari: Kituo cha sheria na haki za binadamu chatoa tamko kali!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,599
Katika taarifa ya habari ya Radio Clouds ya saa 12 jioni, Kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu (LHRC) kimetoa tamko kali kuhusu mgoma wa madaktari. Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wake Mama Helen Kijo-Bisimba ambaye amesema kuwa serikali inatakiwa kumaliza huu mgogoro mara moja. Na kama serikali haiwezi kutatua hili tatizo basi ijiuzulu mara moja. Amesema endapo ikifika kesho na hili tatizo halijatatuliwa, basi watalazimika kuitisha maandamano.Source: Clouds FM!!
 
hili tangazo lao lilikaa kiwoga sana,wanarukia topic na hawana maamuzi.tanzania bado sana!
 
na hii ndio solutiona..na wale madaktar kutoka china hawajawasili tu?


Ila nimesikitika kwamba baadhi ya media ambazo nimefuatilia hadi sasa ikiwemo TBC na BBC hawajarusha tena tamko hilo!!

Anyway, ngoja serikali iendelee kujifariji kwa kulindwa na media,....siku zao zimebaki kiduchu tu!!

Babu DC!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nyie Kituo cha sheria mlikuwa mnangoja nini mnakuja kubweka kama mbwa koko?

Too late for you.

Nyie ni wanaharakati au ni nani?

Siwaelewi.

Nchi inaangamia nyie ndo leo mnaamka?
 
nimeshachoshwa na matamko yasiyo na kichwa wala miguu yule jamaa anapenda sana kuonekana kwenye tv basi
 
Bus lishafika na abiria washashuka nyie ndio mnakumbuka safaei??

Anyways kipindii hii hatutaki hiyo maneno yenu, kama kweli mu wanaharakati fanyeni kweli hiyo kesho
 
Bus lishafika na abiria washashuka nyie ndio mnakumbuka safaei??

Anyways kipindii hii hatutaki hiyo maneno yenu, kama kweli mu wanaharakati fanyeni kweli hiyo kesho
tatizo wanachonga sana bila vitendo kama kweli wanamaanisha wakaweke kambi wizara ya afya.
 
Asaaaaanteeeeeee tuingie barabaraniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Nyie Kituo cha sheria mlikuwa mnangoja nini mnakuja kubweka kama mbwa koko?

Too late for you.

Nyie ni wanaharakati au ni nani?

Siwaelewi.

Nchi inaangamia nyie ndo leo mnaamka?

utasikia Kibamba naye anaropoka halafu siku ikifika anaingia mitini
 
Wanaharati wa Tanzania na kudakia mambo hasa ya kisiasa....mazungumzo tayari yanaendelea then taarifa itapelekwa Bungeni sasa wanaharakati mnataka serikali ikawakamate madaktari na kuwarudisha mahospitalini kwa nguvu?
 
Kujiuzulu ni swala la busara kwa mwenye hekima ila hapa imekula kwetu labda tuwatoe mamba masikioni that is the ony way
 
Back
Top Bottom