Mgomo chuo cha mwenge moshi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kuna mgomo unaendelea chuo cha mwenge moshi sasa hivi wanafunzi wako mbele ya jengo la utawala chuoni hapo na wengine geti wakizuia askari wa kutuliza fujo wasiingie kwenye maeneo ya chuo hicho
 
Nimeongea na Lecturer mmoja hapo chuoni ameconfirm kuwa ni kweli wamegoma kwa sababu ya faculty requirements hawajapewa. wana maandaano ya amani ndani ya chuo ndo maana wamezuia polisi wasiingie chuoni kwani wanasema polisi wakiingia ndo wataanzisha fujo wakati wanachuo hawana mpango wa kuanzaisha fujo. Wamekuwa na mazungumzo na uongozi wa chuo tangu wiki ilopita!
 
Najua hiki chuo kina wanafunzi wengi mapadre na masista. Ina maana nao wamegoma!?
 
polisi wanavihere sana wakati watu wako kiamani wanafuata nini ? badala na wao wakaangalie namna ya kugoma kuendelea kujihelp kwa foleni kwenye makambi yao au wenyewe hawaoni ni udhalilishaji ukiumwa tumbo la kuhara mpk watoto wa jirani wanajua kwani unapita na mkopo wa chooni mara kwa mara hivyo wanakwambia pole baba mura amkeni mdai haki si kuzuia watu kutimiza haki zao za kikatiba za kushinikiza kupewa haki zao
 
Tatizo la wabongo hasa viongozi huwa hawasomi alama za nyakati! Akiona kwa mwenzie kunaungua hajui hata kwake kunaweza kuungua siku moja!
 
Mgomo umekwisha walikuwa ni wanachuo wa mwaka wa tatu (education) na walikuwa wakidai hela za faculty requirements ambazo ni 60000 kwa kila mwanafunzi, walikuwa wamecheleweshewa ila wamepewa mwendo wa saa tano hivi. Chuo kimebidi kutumia administration fund kwa ajili hiyo kwani serikali haijatoa pesa za madenti
 
Amakweli, viongozi wa bongo shule wamekwenda ila tatizo lao kubwa ni uzito wa kufikiri na upofu wa kuona mbali.

Huo ni mfano mdodgo tu, hivi kama hiyo administration fund ilikuwepo kwa nini haikutolewa mapema mpaka watu waanze mgomo?

Kumbe altenative ya ku-settle madai ya wanafunzi ilkuwepo ila mllikuwa mnanapima maji!


Ole wenu, ipo siku watu hawatajali makunyanzi,wataondoka moja kwa moja na shingo zenu kwa uzembe wenu na urasimu usio na tija!

Viongozi wa aina yenu siku zenu zinahesabika katika tanzania ya leo.
 
Back
Top Bottom